Moyo wangu una majonzi, yako wapi mapenzi ya dhati?

Moyo wangu una majonzi, yako wapi mapenzi ya dhati?

GJHariohay

JF-Expert Member
Joined
Oct 24, 2013
Posts
1,041
Reaction score
1,161
Ndu zangu wana jamvi....

Naomba nieleweke hivi, nimechoka, sijui tatizo langu ni kwamba napenda sana bila kiasi, nimepitia kwenye mahusiano kama matatu sasa toka nijue mapenzi ni nini, mwanamke wa kwanza aliniumiza sanaa, nililia mwanaume machozi ya kila aina, sikuwa tayari aniache, nilikuwa naona kam maisha yangu yatakuwa magumu sana nikiachana na huyo dada.
Niliteseka kwa zaidi ya mwaka mmoja nambembeleza turudiane, alinitesa mno, siwezi kuelezea. Siku moja nilijifungia chumbani kwangu saa 11 jioni hadi kesho yake, nilifunga simu, nikapiga magoti, nilisali sana, nilimlilia Mungu moyo wangu upate amani, nikamshi Mungu kama sio mapenzi yake amuweke mbali na mimi yule binti, kweli siku ya pili nilikuwa mwepesiii, sikuwa hata na hamu ya kumtafuta, nilimshukuru sana Mungu maisha yangu yanaanza kubadilika mwishowe nikafuta mpaka namba zake japo hata leo ninazo kichwani....

Nikaanza mahusiano mengine, nikaona picha ni zile zile, nilikimbia mapema nilivoona tabia za mwanamke wangu wa kwanza zimeanza kujirudia kwa mwanamke huyo wa pili....nikamuomba Mungu nisiingie tena kwenye mahusiano kama vinginevyo iwe ni mwanamke wangu alieniandalia, nilikaa kwa karibu mwaka mmoja na nusu bila kuwa na mahusiano ya serious......

Mwaka huu mwezi wa Tano nilikutana na Binti mmoja mrembo kweli, ni mzuri kuanzia kutembea kwake, kuongea kwake, anapenda sana kanisa, kila Jumapili yuko kanisani ibada ya kwanza. Binti huyu kwa mara ya kwanza alikuja kwenye eneo langu la kazi, alikuja kumtembelea rafiki yake ambae pia staff mwenzangu, nilivyomuona kiukweli nilimpenda, nikajaribu kumuuliza yule rafiki yake, akanipa briefing kidgo kuhusu huyo binti, nilimuomba appointment ya kutoka nao wote wawili ili atleast nipate picha halisi na kujuana nae kidogo. Kwenye hiyo out tulibadilishana mawazo kidogo, tukabadilishana na mawasiliano pia, nikaanza kujenga nae urafiki, tukafahamiana vizuri then nikaona ni mtu ambae yuko smart kweli, siku moja nikamuomba appointment ya kutoka nae somewhere for lunch, hakukataa alikuja then tukaongea sana then nikamruhusu aende nyumbani mapema ili awahi mapishi ya jioni. Yote tisa, kumi huyo binti nilianza nae mahusiano baada ya kila mmoja kumfaham mwenzake,,,,ni takriban miezi 5 sasa toka tumeanza mahusiano rasmi, professionaly yeye ni mwalimu, mimi ni Muhasibu, tumekuwa tukiwasiliana vizuri sana, kinachonipa wakati mgumu kwake ni majibu yake, mara nyingi nikichat nae huwa ana majibu mkato sana (shortcuts), unaweza ukawa unamuuliza kitu sensitive yeye akakujibu majibu ambayo like she dont care. Kingine huyu binti amekuwa mgumu sana kushare nae muda, kama mpenzi wangu muda mwingine naweza muomba lunch tule sehem moja lakini akakataa bila sababu, nikimuliza sababu nini atakujibu niko busy ... hii statement ya niko busy imekuwa ikini disappoint sana, ukimuuliza busy na nini atakujibu sorry niko busy. Guys nisaidieni mtu kama huyu kweli bado anaweza kuwa na mapenzi ya dhati kwako? Katika chatting yake mara nyingi tumevutana sana, huwa ni mtu mwenye majibu ambayo yanaonyesha hajali kabisaa,,,

Tukiachana na hayo yote , wiki iliyopita wakati napiga nae story kwenye simu alichomekea agenda yake kuwa anataka kurudi chuo kwa miaka 3 kuanzia mwaka ujao kwa hiyo nikimhitaji maswala ya ndoa nisubiri mwaka 2020. Hili jambo limenikatisha sana tamaa guys, yaani nikae mtaani nimsubiri yeye anaenda chuo kwa miaka minne kuanzia sasa....moyo wangu uliumia sana kiukweli, bado naendelea kuumia, muda mwingine nawaza na kumwambia Mungu kwanini unanipitisha kwenye majaribu magumu kiasi hiki? Kweli ni binti niliempenda sana ila yeye kutokuwa na care inanikatisha tamaa, majibu yake mara nyingi ni " Poa, sawa, K, P n.k.
Guys wenye experience naombeni ushari, naumia kweli maana tayari nilishaingia kwake miguu yote, dalili ya kuumia tena naiona.

Sio dhihaka , sio utani napitia kwenye wakati mgumu, ambao tayari mko kwenye ndoa naomba mtusaidie mlipitia katika wakati kama huu?
Muda mwingine huwa namwambia Mungu mapenzi ya kweli yale ya wazazi wetu yako wapi? Kiukweli vijana wa kiume tunapitia wakati mgumu sana pindi unapomtafuta binti wa kuwa nae kimaisha.

Naamin sipo mwenyewe, tusaidiane kwa ushauri na kufarijiana.
 
Pole duniani hapa hamna mapenzi ya kweli mi najua mapenzi ya dhati yalikuwapo enzi za kina Yesu na huwa naamini ukivalue mapenzi utapata partiner ambae ni pasua kichwa hasa ila siwezi semea watu wote naambiwa bado wenye mapenzi ya kweli wapo endelea kuomba maana kwa MUNGU yote yawezekana
 
Mkuu unamchosha tuu mungu unazidisha foleni za maombi yetu huko na sisi tulegezewe vyuma kidogo, kisa kuomba mambo yako ya ajabu.

Sasa Kama hakutaki wewe si mwasibu wekeza nguvu na mdaa wako kwenye carrier yako mke ulopangiwa haitaji nguvu kubwa kumpata atakuja tuu na utaona kabisa mambo yanaenda smooth kabisa hautumii nguvu nyingi mpaka ulie lie hapa.
 
Pole duniani hapa hamna mapenzi ya kweli mi najua mapenzi ya dhati yalikuwapo enzi za kina Yesu na huwa naamini ukivalue mapenzi utapata partiner ambae ni pasua kichwa hasa ila siwezi semea watu wote naambiwa bado wenye mapenzi ya kweli wapo endelea kuomba maana kwa MUNGU yote yawezekana
Naamini hivo, for sure nitamwomba sana Mungu, najua kila jambo kwake linawezekana
 
Hahahahahahhaaaaaa ngoja nicheke kwanza!!! Umenisikitisha sana mbaya zaidi wewe ni mwanaume unaongea hivo......duuuuhhhh
 
Usioneshe kwamba unampenda sanaaaa....akijua unampenda sana atakutesa mkuu...ignore he sometimes uone anavyo crave your attention
Ahsante mkuu. Hicho ndio nimefikiria hata mimi
 
Mmmhhh pole mkuuu .

Weee nimwanamme ikiwa utafuauli kuzishinda nyakati ngumu Basi maishan mwako hutokua nakitu chakupoteza .

Sijui kwa wanaume wenzangu ila Mimi Putin,, sijawahi kuumia kwamambo aloyasababisha mwingine ,,, ukiona naumia huwa naumia sababu ya jambo nilomtendea Mimi sasa nafsi inanisuta.

Embu jifunze kutotoa nafasi za watu ( mahusiano )kukuumiza nautambue ,,mapenzi nikitovu chauzembe ,,mapenzi yanaweza kukuharibia kazi nahata kukuaa.

AISEEE KWA AJILI YA MOYO WANGU MAMAISHA YANGU ,,NIBORA WAENDELEE KUNIONA MKOLONI !!!.ILA UPUUZI SITAKI...
Element moja wapo yamtu Kukupuuza huwa nimajibu yake .

Mfano am charting with you then unanipa a One word answer wakat nmekutext so as to have a conversation with you !!! Aiseeeee embu kua nahii moja ya sheria zangu "fire-fight-fire" ..... Akijifanya anakuigizia maisha as if km ni WIDOW ,naww jifanye ni WIDOWER.

MKUU KIUKWELI NAMSHUKURU MUUMBAJI WANGU KWA KUNIPA MOYO MGUMU ,,MOYO WAKUJIAMINI ,, NINA SURA MBAYA LKN HUWA NAJUA HUYU AKINIZENGUA TUUU ,,NAAMSHA NATAFUTA MWINGINE NABADO NIKAPENDWA NA KUAMINIWA !!!.

Viumbe hawa ,, kama anakuzengua alafu naww unaendelea kushikilia Uzi Wa " nakupenda tu " Basi jiandae kua Mnunuzi mzuri Wa vitambaa,,, Dawa za maumivu ,,,kutafuta ushauri Sanaaa,, n.k.

MKUUU USIRUHUSU MWANAMKE KUIFANYA ROHO YAKO KUA REHANI !!.
 
Mkuu unamchosha tuu mungu unazidisha foleni za maombi yetu huko na sisi tulegezewe vyuma kidogo, kisa kuomba mambo yako ya ajabu.

Sasa Kama hakutaki wewe si mwasibu wekeza nguvu na mdaa wako kwenye carrier yako mke ulopangiwa haitaji nguvu kubwa kumpata atakuja tuu na utaona kabisa mambo yanaenda smooth kabisa hautumii nguvu nyingi mpaka ulie lie hapa.
Fact, umeanza vibaya but umenipa madini hapo chini
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom