Moyo wangu si wachuma, nimsamehe Mara ngapi!

antidot

Member
Dec 30, 2016
96
195
Niambieni ndugu zangu makosa yangu yako wapi?

Niambieni kama mikono yangu haijatakasika na damu yake kama bado ipo katika viganja vyangu.

Kama upendo wake ni wa kweli nami nimefanya makosa niambieni nikamuombe radhi.

Amina wangu nilimpenda toka ndani ya moyo wangu, hakika sikumtamani kwa rangi yake yakuvutia, sura yake ya mdoli wala umbo lake linalomvutia kila mwanaume atakaye mtia machoni, bali nilimpenda kutoka ndani tena ndani ya moyo wangu.

Nilikutana naye nikiwa kidato cha sita, macho yangu yalipo mwona hakika mapigo ya moyo yalisimama, nikamwomba mawasiliano amina wangu na bila hiyana akanipatia.

Looooh! Sikujua naingia katika tanuri la moto mkali! Nilianza uhusiano na amina wangu baada tu yakunikubalia kuwa pamoja nae katika mahusiano ya kimapenzi, licha ya kwamba nilikua shule nilichanganya mambo mawili, mapenzi na shule.

Nikaendelea kuwa na amina wangu mpaka matokeo yakatoka na nikafanikiwa kujiunga na chuo kilichopo DSM, hakika nilifurahi sana maana nilikua nakuja kua karibu zaidi na amina wangu, mwanzo mimi nilikua KlMNJR naye alikua DSM.

Mwaka wa kwanza nikauanza chuoni kwa furaha pasipo kujua karaha haikua mbali, mpaka pale amina wangu alipo kuja kunitembelea hostel na akakutana na rafiki yangu niliyekua nalala nae deka moja na hakika amina wangu alilisaliti penzi langu kwa mtu huyu.

Nikapiga moyo konde nikaendelea na maisha yangu, amina wangu penzi lile baada ya miezi miwili likamshinda na akarudi kwangu akaniangukia na kuniomba radhi, moyo wangu mdogo sana, nikampokea Amina wangu na tukaendelea na safari kwa kuanzia pale ilipoishia!

Siku zikasogea wiki zikakatika miezi ikajongea mwaka wa pili nikaingia! Nikiwa na imani na amina wangu.

Maskini mimi, kumbe nilikua pazia, umuhimu wangu hauzidii mlango, amina wangu akapewa mimba na mtu wake aliekua anampenda zaidi yangu! Mtu yule kaikataa mimba ile, nyumbani kwa Amina wangu kukawa kwa moto, shangazi yake aliyekua anamstiri hakumtaka tena,

Umuhimu wangu ukaonekana, Amina wangu akaniomba ushauri ni nini afanye kwa wakati ule, aue kiumbe kile kilichopo katika tumbo lake au afe yeye pamoja na kiumbe chake? Moyo wangu mdogo sana, nilimshauri alee mimba yake ili azae kiumbe kile kisicho na hatia.

Alihaha mchana na usiku kutafuta mahali pa kuishi ili alee mimba ile, Mungu si athumani mama yake mkubwa akampa hifadhi mkoa wa Dodoma

Kalea mimba mpaka kajifungua pasipo kuwasiliana nami, ila punde tu alipo maliza kunyonyesha alinitafuta.

Amina wangu, akaniomba radhi kwa nguvu zote na kunihakikishia hatorudia makosa kamwe maana ulimwengu umemfunza.

Masikini moyo wangu mdogo sana, nilimsamehe Amina wangu na nikamrudisha ndani ya moyo wangu.

Nikajitambulisha kwao na nikaanza kuishi na Amina wangu, sikusubiri mambo ya ndoa kwa huruma yangu na kwa kumuonea moyo wa imani Amina wangu aliyekua anaishi katika mazingira magumu sana.

Sikio la kufa ni lakufa tuu, kupambana nalo utajipa shida, Amina wangu nikazaa nae mtoto mmoja! Na tabia zikabadilika, zarau, majivuno, kujisikia na matusi ukawa in utamaduni wake ndani ya nyumba.

Nikamkumbuka mola wangu na kumuuliza ni wapi nilimkosea mpaka napitia mitihani hii yote.

Nikaamua kujaribu kutafuta nini chanzo cha vurugu zote hizo ndani ya nyumba? Nilitokwa na ufahamu na hakika moyo wangu ulipasuka vipande nilipogundua amerudisha uhusiano na bwana yule aliyemzalia mtoto wa kwanza ambae nilikua naishi nae kama mwanangu.

Wanawake mna moyo wa ajabu sana! Nikaona isiwe tatizo ni bora nikae mbali nimuache afanye yale ayatakayo kwa amani, nikaondoka na suruali zangu na mashati yangu vitu vyote nikamwachia! Pamoja na watoto, mmoja wangu na mwingine wa huyo mume mwenza.

Niliacha duka pia ambalo natumai uji wa mwanangu utatoka hapo!
Kinachonisumbua ni kwamba tangu niondoke ananisumbua sana katika simu kasha tuma Meseji zisizo na idadi akiniomba msamaha, akipiga simu huwa sipokei bali huwa najisikia vibaya sana kuona calls zake.

Ndugu zangu naomba ushauri wenu, ni nini nifanye? Nimsamehe Mara ngapi mtu Huyu? Kama kuna mahala nimekosea niambieni pia.

Haya si masihara wala hadithi ya kusadikika ndugu zangu, haya ndio magumu ninayoyapitia, naomba ushauri wenu.

Yeye nimemuacha huko mkoani nami nipo DSM.
 
Kumbuka kuwa bahati mbaya inayojirudia mara nyingi ni makusudi.

Kosa lako ni kumsamehe kila sku wakati unajua kabisa huyo ni kunguru hafugiki. Jikaze halafu move on ashakuona wewe weak sana kwake. Alikuletea mimba umemsamehe sasa subiri akuletee magonjwa ya ajabu kama vile Ukimwi.
 
Hapo lengo ni kuwasema single mom japo umezunguka saaanaa.
Namuheshimu sana mwanamke katika maisha yangu ! Huwa naumia sana pia napomuona huyo single mom akihangaika na mtoto au watoto , wakati aliesababisha yupo na anaishi kwa amani some where else! Kuna vitu vingine mtu huwa vigumu kuuelewa ukweli wake, hiyo haikua point yangu ya msingi , principle girl , this is real na nimeyatoa yanayousumbua moyo wangu.
 
Back
Top Bottom