Moyo wangu si wachuma, nimsamehe Mara ngapi!

Niambieni ndugu zangu makosa yangu yako wapi?

Niambieni kama mikono yangu haijatakasika na dam yake kama bado Ipo katika viganja vyangu!

Kama upendo wake ni wakweli nami nimefanya makosa niambieni nikamuombe radhi!

Amina wangu nilimpenda toka ndani ya moyo wangu, hakika sikumtamani kwa rangi yake yakuvutia, sura yake ya mdoli wala umbo lake linalomvutia kila mwanaume atakaye mtia machoni, Bali nilimpenda kutoka ndani tena ndani ya moyo wangu!

Nilikutana naye nikiwa kidato cha sita , macho yangu yalipo mwona hakika mapigo ya moyo yalisimama, nikamwomba mawasiliano amina wangu na bila hiyana akanipatia!

Looooh! Sikujua naingia katika tanuri la moto mkali!
Nilianza uhusiano na amina wangu baada tu yakunikubalia kuwa pamoja nae katika mahusiano ya kimapenzi, licha ya kwamba nilikua shule nilichanganya mambo mawili , mapenzi na shule.

Nikaendelea kuwa na amina wangu mpaka matokeo yakatoka na nikafanikiwa kujiunga na chuo kilichopo DSM, hakika nilifurahi sana maana nilikua nakuja kua karibu zaidi na amina wangu , mwanzo mm nilikua KlMNJR naye alikua DSM.

Mwaka wa kwanza nikauanza chuoni kwa furaha pasipo kujua karaha haikua mbali, mpaka pale amina wangu alipo kuja kunitembelea hostel na akakutana na rafiki yangu niliyekua nalala nae deka moja na hakika amina wangu alilisaliti penzi langu kwa mtu huyu,

Nikapiga moyo konde nikaendelea na maisha yangu, amina wangu penzi lile baada ya miezi miwili likamshinda na akarudi kwangu akaniangukia na kuniomba radhi, moyo wangu mdogo sana, nikampokea amina wangu na tukaendelea na safari kwa kuanzia pale ilipoishia!

Siku zikasogea wiki zikakatika miezi ikajongea mwaka wa pili nikaingia! Nikiwa na imani na amina wangu!

Maskini Mimi , kumbe nilikua pazia, umuhimu wangu hauzidii mlango, amina wangu akapewa mimba na mtu wake aliekua anampenda zaidi yangu! Mtu yule kaikataa mimba ile, nyumbani kwa amina wangu kukawa kwa moto, shangazi yake aliyekua anamstiri hakumtaka tena,

umuhimu wangu ukaonekana, amina wangu akaniomba ushauri ninini afanye kwa wakati ule, aue kiumbe kile kilichopo katika tumbo lake au afe yeye pamoja na kiumbe chake? Moyo wangu mdogo sana, nilimshauri alee mimba yake ili azae kiumbe kile kisicho na hatia!

Alihaha mchana na usiku kutafta mahali pa kuishi ili alee mimba ile, mungu si athumani mamaye mkubwa akampa hifadhi mkoa Fulani unaopakana na Dodoma ,

Kalea mimba mpaka kajifungua pasipo kuwasiliana nami, ila punde tu alipo maliza kunyonyesha alinitafuta ,

amina wangu, akaniomba radhi kwa nguvu zote na kunihakikishia hatorudia makosa kamwe maana ulimwengu umemfunza!

Maskini moyo wangu mdogo sana, nilimsamehe amina wangu na nikamrudisha ndani ya moyo wangu!

Nikajitambulisha kwao na nikaanza kuishi na amina wangu , sikusubiri mambo ya ndoa kwa huruma yangu na kwa kumuonea moyo wa imani amina wangu aliyekua anaishi katika mazingira magumu sana,

Sikio la kufa ni lakufa tuu, kupambana nalo utajipa shida, amina wangu nikazaa nae mtoto mmoja! Na tabia zikabadilika , zarau, majivuno, kujiskia na matusi ukawa in utamaduni wake ndani ya nyumba,

Nikamkumbuka mola wangu na kumuuliza ni wapi nilimkosea mpaka napitia mitihani hii yote!

Nikaamua kujaribu kutafta nini chanzo cha vurugu zote hizo ndani ya nyumba? Nilitokwa na ufahamu na hakika moyo wangu ulipasuka vipande nilipogundua amerudisha uhusiano na bwana yule aliyemzalia mtoto wa kwanza ambae nilikua naishi nae kama mwanangu!

Wanawake mna moyo wa ajabu sana! Nikaona isiwe tatizo ni bora nikae mbali nimuache afanye Yale ayatakayo kwa amani, nikaondoka na suruali zangu na mashati yangu vitu vyote nikamwachia! Pamoja na watoto , mmoja wangu na mwingine wa huyo mume mwenza.

Niliacha duka pia ambalo natumai uji wa mwanangu utatoka hapo!

Kinachonisumbua ni kwamba tangu niondoke ananisumbua sana katika sim kasha tuma Meseji zisizo na idadi akiniomba msamaha, akipiga sim huwa sipokei Bali huwa najisikia vibaya sana kuona calls zake.

Ndugu zangu naomba ushauri wenu, ni nini nifanye! Nimsamehe Mara ngapi mtu Huyu? Kama kuna mahala nimekosea niambieni pia.

Haya si masihara wala hadithi ya kusadikika ndugu zangu, haya ndio magumu ninayo yapitia , naomba ushauri wenu.

Yeye nimemuacha huko mkoani nami nipo DSM.
Umefanyiwa yoote hayo bado unaomba ushaur ww unampenda bado huyo mtu mrudie
 
Namuheshimu sana mwanamke katika maisha yangu ! Huwa naumia sana pia napomuona huyo single mom akihangaika na mtoto au watoto , wakati aliesababisha yupo na anaishi kwa amani some where else! Kuna vitu vingine mtu huwa vigumu kuuelewa ukweli wake, hiyo haikua point yangu ya msingi , principle girl , this is real na nimeyatoa yanayousumbua moyo wangu.
Kama ni kweli uyasemayo pole ila Mungu anakuona.
 
Duh! Kweli JF inataka kugeuzwa Fb.....maana sio kwa stahili hii!
Inaonekana wewe ni member wa muda mrefu na unaijuma vema jf kuliko yeyote maana si kwa kusema hivo,kwani kinachofanya igeuzwe fb ni kipi hasa?
 
Niambieni ndugu zangu makosa yangu yako wapi?

Niambieni kama mikono yangu haijatakasika na dam yake kama bado Ipo katika viganja vyangu!

Kama upendo wake ni wakweli nami nimefanya makosa niambieni nikamuombe radhi!

Amina wangu nilimpenda toka ndani ya moyo wangu, hakika sikumtamani kwa rangi yake yakuvutia, sura yake ya mdoli wala umbo lake linalomvutia kila mwanaume atakaye mtia machoni, Bali nilimpenda kutoka ndani tena ndani ya moyo wangu!

Nilikutana naye nikiwa kidato cha sita , macho yangu yalipo mwona hakika mapigo ya moyo yalisimama, nikamwomba mawasiliano amina wangu na bila hiyana akanipatia!

Looooh! Sikujua naingia katika tanuri la moto mkali!
Nilianza uhusiano na amina wangu baada tu yakunikubalia kuwa pamoja nae katika mahusiano ya kimapenzi, licha ya kwamba nilikua shule nilichanganya mambo mawili , mapenzi na shule.

Nikaendelea kuwa na amina wangu mpaka matokeo yakatoka na nikafanikiwa kujiunga na chuo kilichopo DSM, hakika nilifurahi sana maana nilikua nakuja kua karibu zaidi na amina wangu , mwanzo mm nilikua KlMNJR naye alikua DSM.

Mwaka wa kwanza nikauanza chuoni kwa furaha pasipo kujua karaha haikua mbali, mpaka pale amina wangu alipo kuja kunitembelea hostel na akakutana na rafiki yangu niliyekua nalala nae deka moja na hakika amina wangu alilisaliti penzi langu kwa mtu huyu,

Nikapiga moyo konde nikaendelea na maisha yangu, amina wangu penzi lile baada ya miezi miwili likamshinda na akarudi kwangu akaniangukia na kuniomba radhi, moyo wangu mdogo sana, nikampokea amina wangu na tukaendelea na safari kwa kuanzia pale ilipoishia!

Siku zikasogea wiki zikakatika miezi ikajongea mwaka wa pili nikaingia! Nikiwa na imani na amina wangu!

Maskini Mimi , kumbe nilikua pazia, umuhimu wangu hauzidii mlango, amina wangu akapewa mimba na mtu wake aliekua anampenda zaidi yangu! Mtu yule kaikataa mimba ile, nyumbani kwa amina wangu kukawa kwa moto, shangazi yake aliyekua anamstiri hakumtaka tena,

umuhimu wangu ukaonekana, amina wangu akaniomba ushauri ninini afanye kwa wakati ule, aue kiumbe kile kilichopo katika tumbo lake au afe yeye pamoja na kiumbe chake? Moyo wangu mdogo sana, nilimshauri alee mimba yake ili azae kiumbe kile kisicho na hatia!

Alihaha mchana na usiku kutafta mahali pa kuishi ili alee mimba ile, mungu si athumani mamaye mkubwa akampa hifadhi mkoa Fulani unaopakana na Dodoma ,

Kalea mimba mpaka kajifungua pasipo kuwasiliana nami, ila punde tu alipo maliza kunyonyesha alinitafuta ,

amina wangu, akaniomba radhi kwa nguvu zote na kunihakikishia hatorudia makosa kamwe maana ulimwengu umemfunza!

Maskini moyo wangu mdogo sana, nilimsamehe amina wangu na nikamrudisha ndani ya moyo wangu!

Nikajitambulisha kwao na nikaanza kuishi na amina wangu , sikusubiri mambo ya ndoa kwa huruma yangu na kwa kumuonea moyo wa imani amina wangu aliyekua anaishi katika mazingira magumu sana,

Sikio la kufa ni lakufa tuu, kupambana nalo utajipa shida, amina wangu nikazaa nae mtoto mmoja! Na tabia zikabadilika , zarau, majivuno, kujiskia na matusi ukawa in utamaduni wake ndani ya nyumba,

Nikamkumbuka mola wangu na kumuuliza ni wapi nilimkosea mpaka napitia mitihani hii yote!

Nikaamua kujaribu kutafta nini chanzo cha vurugu zote hizo ndani ya nyumba? Nilitokwa na ufahamu na hakika moyo wangu ulipasuka vipande nilipogundua amerudisha uhusiano na bwana yule aliyemzalia mtoto wa kwanza ambae nilikua naishi nae kama mwanangu!

Wanawake mna moyo wa ajabu sana! Nikaona isiwe tatizo ni bora nikae mbali nimuache afanye Yale ayatakayo kwa amani, nikaondoka na suruali zangu na mashati yangu vitu vyote nikamwachia! Pamoja na watoto , mmoja wangu na mwingine wa huyo mume mwenza.

Niliacha duka pia ambalo natumai uji wa mwanangu utatoka hapo!

Kinachonisumbua ni kwamba tangu niondoke ananisumbua sana katika sim kasha tuma Meseji zisizo na idadi akiniomba msamaha, akipiga sim huwa sipokei Bali huwa najisikia vibaya sana kuona calls zake.

Ndugu zangu naomba ushauri wenu, ni nini nifanye! Nimsamehe Mara ngapi mtu Huyu? Kama kuna mahala nimekosea niambieni pia.

Haya si masihara wala hadithi ya kusadikika ndugu zangu, haya ndio magumu ninayo yapitia , naomba ushauri wenu.

Yeye nimemuacha huko mkoani nami nipo DSM.
Hi story kama ya kweli bas ni wanaume wachache wenye moyo huu wakusamehe, weng wanaume c wavumilivu, huyo hafai kabisa umemsitir ila bado hajitambui na haoni uliyomtendea, kitendo chakurudiana na aliyemzalisha hilo kosa kubwa acha dunia imfunze
 
moyo wako mdogo msamehe tena mpaka akikuua kwa presha, ama ugonjwa ndo umuache ukiwa tayari kaburini.
 
Shukuru hamkufunga ndoa (uzinzi c mzuri lkn Mkuu ) hyo ndo imekuwa salama yako achana nae huu sio muda wa kuhangaika na wanawake, au wanaume au mapenzi, chukua mtoto wako ye muache aendelee kulaanika... pole mwaya!
 
Yani mpaka kutuletea hapa ni kwamba hata wewe bado upo njia panda ila sijui ya wapi..umsamehe au umpige chini.. Sikiliza sauti ya moyo wako kwakwel, lla Amina ni nyo.ko aiseee daaa
 
Kula ngada mkuu
am sure hautakuwa na moyo mdogo tena wa kusamehe hovyo.
Teh teh teh teh.....
 
Mwanamke msamehe yote ila akilala na mwanaume mwengine katu usimsamehe ,tabia zote vumilia kasoro ukahaba maana hauna dawq
 
Mkuu......
Huyo mwanamke atakusumbua hata ukirudiana nae cha msingi mchukue mwanao umlee na kumpa malezi bora yanayo stahili kupewa kama haki yake,
Mtunze na umlee vizuri,
Kwa upande wa huyo mwanamke ( amina ) nakushauri achana nae endelea na maisha yako naamini mwenyezi mungu atakupigania na kukuwezesha utafanikiwa,
Usikate tamaa endelea kupambana ili wewe na mwanao muishi vizuri.
Kuhusu huyo mwanamke muache aendelee na maisha yake.
Na usiwe mdhaifu kukubali kusamehe makosa ambayo ni makusudi, lazima uoneshe msimamo wako kama mwanaume rijali na mwanaume anayejitambua kumbuka mwanaume anaonekana kichwa katika familia na kuonekana kama msaada kwa wana jamii ukiwa huna msimamo na kujielewa utayumbishwa na kila mwanamke kwa udhaifu huo.

Muombe mungu akusaidie uendelee vyema na maisha yako na mwanao, huyo mwanamke muache hapo itakuwa salama kwako.

duh moyo wako ni mashine . haya muhimu huyo kasha geuza moyo wako uwanja wa mapambano ila mfungaji mwingine.. chukua mwanao lea huku ukiendelea kutafakari je unahitaji kuendelea na amina au lah
 
Hahahahaaa shigongo anakuhitaji siyo kwa simulizi iyo,,,,,,,,,,,,,,mpaka nmeshindwa kuelewa ni kweli au umemkop shigongo,,,,,,,,[HASHTAG]#napita[/HASHTAG] tuu.
 
Nafsi yako dhaifu sana, hivi nini hasa unachotafuta kwake zaidi ya hayo aliyokutendea? anyway wewe ndo mwenye maamuzi ya mwisho, kama umekubali na kuridhika na ujinga huo endelea ila mwisho wa siku tutakuja na kauli " Bwana alitoa na Bwana ametwaa jina la Bwana lihimidiwe, au Sisi tulikupenda ila Bwana amekupenda zaidi ustarehe kwa amani"
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom