SEHEMU YA 77
Hakutaka kujivunga, akazichukua na kuziweka kwenye mkoba wake, kijana huyo akampa na kikaratasi na kalamu.
“Amesema anahitaji namba yako!” alisema kijana yule.
“Ya nini?”
“Nadhani kuwasiliana!”
Iyanya hakutaka hata kuchelewa, akachukua kalamu ile na kuandika namba yake ya simu na kumpa kijana huyo ambaye akaondoka kuelekea kwa bosi wake ambaye hakumjua kabisa.
Kwake, akili yake ilimwambia kwamba mwanaume huyo alikuwa na pesa, isingewezekana kwa mwanaume wa kawaida kumpa dola elfu mbili halafu asiwe na pesa, ila ukiachana na hilo pia aliambiwa kwamba alikuwa na gari aina ya Lambornghin, moja ya magari gharama duniani, hivyo akajua kabisa kwamba alikuwa na pesa.
Baada ya kumaliza kula, wakaondoka na kurudi nyumbani.
Alipofika huko, hakukaa sana, mara simu yake ikaanza kuita, alipoagalia kioo, ilikuwa namba ngeni, alijua tu kwamba alikuwa mwanaume huyo, akaipokea.
“Halo!” ilisikika sauti ya mwanaume kutoka upande wa pili.
“Naonge na nani?”
“Mr Khone!”
“Ndiye nani?”
“Nilimtuma kijana wangu akuletee pesa, ulizipata?”
“Oh! Kumbe ni wewe! Asante sana, nilizipata!”
“Safi sana. Hivi unaihsi wapi? Naweza kuonana na wewe?” aliuliza mwanaume huyo kwenye simu.
“Kuonana na mimi? Kuna nini?”
“Nataka nizungumze nawe!”
“Zungumza nakusikia!”
“Kwenye simu?”
“Ndiyo!”
“Hapana bwana! Naomba tuonane sehemu yoyote ile,’ alisikika mwanaume huyo.
“Sawa. Nitakutaarifu!”
“Sawa!” alisema mwanaume huyo na Iyanya kukata simu.
|
|
|
Nipo bize kuandaa kukimalizia kitabu cha DILI LA DOLA BILIONI NNE ambacho kitatakiwa kuingia sokoni mwezi ujao. Kitakuwa sh. 10,000/= na kitakuwa na kurasa 380. Kama utahitaji kuweka oda yako mapema, njoo kwenye meseji za kawaida 0718069269.....USITUME KWA WHATSAPP KWA KUWA SIPO HUKO KWA MUDA.