ElPuto Jefe
JF-Expert Member
- Oct 16, 2015
- 5,286
- 19,463
Nimeandika nikafuta, hayo matusi mods wangeona ningelimwa ban ya mwaka..
Theo anazingua sana...
Utamu huu huu au mwingine.?Huo uoga wako tu japo kulia c issue waweza lia kilio cha utam ati!
Sent using Jamii Forums mobile app
Theo fala kweli kweli....SEHEMU YA 64
Walichukua dakika kadhaa, wakafika na kupelekwa ndani ya chumba cha upasuaji. Kitu cha kwanza kabisa kabla ya wote ni jopo la madaktari kumi kukutana na kuanza kuipitia ripoti kutoka katika hospitali aliyotoka nchini Tanzania, wasingeweza kufanya kitu chochote kile pasipo kuipitia ripoti hiyo ambayo ingewapa mwanga wa wapi pa kuanzia.
Wakati madaktari wakiendelea kujadili kuhusu hali ya mgonjwa ndipo Theo akarudiwa na wazo kuhusu Iyanya.
Alishtuka, alimuacha msichana huyo hotelini, hakujua ni kitu gani kilitokea baada ya yeye kuondoka chumbani na kuelekea hospitalini.
Alitakiwa kuwasiliana naye na kumwambia kila kitu ili kama ingewezekana basi afunge safari na kuelekea nchini India kumfuata.
Haraka sana akamuaga mke wake kwamba alikuwa akienda chooni ambapo huko akampigia simu kwa WhatsApp na kuanza kuongea naye.
Kitu cha kwanza kabisa kilikuwa ni kumuomba msamaha kwa kilichotokea, alimwambia alikuwa akipitia kwenye matatizo na familia yake hivyo angeomba sana amuonee huruma lakini penzi lao lilikuwa kama lilivyokuwa kipindi cha nyuma.
“When will you come back?” (utarudi lini?) aliuliza msichana huyo.
“I don’t know! I just want you to come here!” (sijui! Ninataka uje huku) alisema Theo.
“India?”
“Yaap!”
“Why?” (kwa nini?)
“I want to spend the time together. I really miss you my baby! Please, I want to see you,” (ninataka nitumie muda mwingi pamoja. Nimekukumbuka mno mpenzi! Nitaka kukuona, tafadhali) alisema Theo huku akionekana kumuhitaji mno mwanamke huyo.
“I got nothing in my pockets,” (sina kitu mfukoni)
“That’s not a problem!” (hilo si tatizo) alisema Theo.
Ilikuwa ni lazima kujitoa kwa mwanamke huyo, alimpenda kuliko hata mke wake, kwake, alimthamini na alikuwa tayari kufanya jambo lolote lile lakini mwisho wa siku aweze kuwa naye.
Alikuwa tajiri mkubwa, alikuwa na pesa, kwake, kumtumia pesa mwanamke huyo halikuwa tatizo hata kidogo hivyo haraka sana akafanya muamala na kumtumia kiasi cha milioni kumi kwenye akaunti yake.
yani ninahasira na huyo mwanaizaya kama vile mimi ndie anayenifanyia vile
yani ninahasira na huyo mwanaizaya kama vile mimi ndie anayenifanyia vile
Sent using Jamii Forums mobile app