Moyo Ulioonja Maumivu

 
Naenda kulia mkuu ..hii long waiting sio ya nchi hii
Tumwite tartiiibu.. . .... ...

Atakuja tu...
Maana .... Tevie haongei ila wakati mwingine..
Itakuwa kazongwa ..mambo mengi na usawa huu wa jiwe... ... ngoma nzito...inabidi kujipinda!
 

Ubarikiwe sana Shunie
 
Tumwite tartiiibu.. . .... ...

Atakuja tu...
Maana .... Tevie haongei ila wakati mwingine..
Itakuwa kazongwa ..mambo mengi na usawa huu wa jiwe... ... ngoma nzito...inabidi kujipinda!
Naenda kulia mkuu ..hii long waiting sio ya nchi hii
kama ni me huko bafuni unaenda kulia machozi ya simba!
Kweli arosto .... acha nikajililie zangu bafuni mie
Toka mwanzo nilitoa taarifa hii ndio arosto yenyewe sasa mvumilie tu
 
Mkweee!! Nimekuja kimya kimya mpaka nimekukuta hapa,,vipi kwema? Ahsante Sana kwa rubudani
 
SEHEMU YA 37

Theo alibaki akimwangalia mke wake pale kitandani alipokuwa. Moyo wake ulimuuma mno, swali alilomuumiza likamfanya kuanza kukumbuka kila kitu kilichotokea. Machozi yalianza kujaa machoni mwake lakini hakutaka kuyaruhusu yatiririke mashavuni mwake kwa kuwa aliamini mke wake angegundua kila kitu.

Violeth aliendelea kumwambia mume wake kuhusu watoto wake, aliamini kwamba alijifungua salama kabisa lakini baada ya kutuliza macho yake usoni mwa Theo, akagundua kulikuwa na kitu kilitokea kwani lisingekuwa jambo jepesi kwa mwanaume ambaye mkewe alijifungua salama kuwa na muonekano ule aliokuwanao.

Akamuuliza tatizo lilikuwa nini, Theo hakutaka kumwambia ukweli, alibaki kimya lakini mke wake huyo hakutaka kunyamaza, alihisi kulikuwa na kitu na alikuwa tayari kuambiwa kwani hali ile ilimtia hofu mno.

“Kuna nini mume wangu?” aliuliza Violeth huku akimwangalia Theo.
“Hakuna kitu!” alijibu Theo kwa kujikaza.
“Mbona macho yako mekundu hivyo? Ulikuwa unalia ama?” aliendelea kuuliza mwanamke huyo.

Theo akashindwa kuvumilia kabisa, machozi yake yakaanza kutiririka mashavuni mwake kitu kilichomshtua mno Violeth ambaye alihisi kulikuwa na jambo fulani ambalo mume wake hakutaka kumwambia.

“Hapana! Kuna tatizo! Kwanza nataka kuwaona wanangu,” alisema Violeth huku akimwangalia mume wake, hakuishia hivyo tu bali akataka kuinuka, haraka sana daktari aliyekuwa pembeni akamsogelea na kumzuia.

“Violeth! Subiri, usiinuke,” alisema daktari kwani alijua kama angeinuka basi angeuchomoa mpira uliokuwa ukipitisha maji kwenda kwenye mishipa yake.
“Niambieni kuhusu wanangu!” alisema Violeth kwa sauti kubwa.


“Subiri kwanza...” alimtuliza daktari.
Ilikuwa vigumu sana kwa Violeth kutulia, alihitaji kitu kimoja tu mahali hapo, kuwaona watoto wake.

Alimwambia daktari kwamba asingeweza kutulia hata kidogo, alifika hospitalini hapo kwa lengo la kujifungua, kazi hiyo ilifanyika hivyo alihitaji kujua ni kitu gani kilikuwa kikiendelea.
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…