Movie ya Exam

Johnny Sins

JF-Expert Member
Nov 4, 2019
2,538
3,833
96644814_1374484012734898_9015398330129186816_n.jpg

..Alternate Britain..mahali ilipopandwa mizizi ya jengo lenye watu wasomi..na wahusika wanaohitaji kazi ndani ya jumba hili elimu ndo kipaumbele cha kwanza..

..Walipatikana watu nane wanaohitajika kufanyiwa interview..wakapewa siti wakakaa..wakakabidhiwa askari awalinde..

..ni kama mtihani wa shule..kasoro huu ulikuwa wa kazi..ulianza hivo na haukuisha hivo..

..Kila alipo mtu mmoja kwenda kwa mwenzie kuna mita moja..na kila dawati lina karatasi na peni moja..

..Akaingia kiongozi wa interview..akatangaza masharti ya kufanikiwa kupata kazi..masharti ni matatu tu..ndio ni matatu tu..

...La kwanza hakuna mfanyaji wa mtihani kuongea na askari wala kumuuliza msimamizi...

...la pili marufuku kuichora ile karatasi wala kuichana kwa bahati mbaya au makusudi

..na mwisho hakuna mtu kutoka kwenye chumba cha interview mpaka muda uishe..

..Ni dakika 80 ndo zilitakiwa kuamua nani anapata kazi na nani hapati..ni dakika hizo ndizo zilizozaa mauaji ya wenyewe kwa wenyewe ndani ya chumba cha mtihani!..

....Bado hujaelewa!!!..ni hivi..

...Kila mtu ndani ya chumba kile alihitaji kazi kwa gharama yoyote..na karatasi za interview zilikuwa hazijaandikwa chochote..

....Sio kama interview nyingine unaulizwa swali we ujibu..hii ilimtaka anaefanyiwa interview alitafute kwanza swali kabla ya jibu..

...Interview ilikuwa ni kutafuta swali utaloulizwa kwenye interview..

..Walikatazwa kuongea na askari lakini waliruhusiwa kuongea wenyewe kwa wenyewe..iliwalazimu waungane ili walitafute swali kutoka kwenye kila karatasi ya mmojawao..

...Karatasi ina swali moja tu! kwa mujibu wa msimamia mtihani.....Na halijaandikwa..inapaswa litafutwe ndani ya dakika 80..

..Ni dakika nyingi kwa kutamka lakini hazikutosha kwa akili za watu nane mpaka movie inakwisha..ni kisanga...

...Na swali lilikuwepo..

..#EXAM
 
White mzinguaji, ila sikupenda lile suala lilivyofichwa na namna linavyokuja kutambulika na yule mshiriki wa mwisho. Movie ilivyokwisha haikua poa sana.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom