Movie (Film) - Daudi Mwangosi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Movie (Film) - Daudi Mwangosi

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Challenger, Sep 13, 2012.

 1. Challenger

  Challenger Member

  #1
  Sep 13, 2012
  Joined: Sep 5, 2007
  Messages: 53
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Wana JF,

  Baada ya kuugukia kwa muda sasa kifo cha Mwandishi wa Habari - Mwakilishi kwa Kituo cha Television cha Ch.10 - Marehemu Mwangosi. Na pia kwa kwa kina kusoma thread mbali mbali za wadau ndani ya mtandao huu Uliosimama - nimekuja na idea moja ambayo. Nitawaombeni Maoni yenu.

  Kuna haja sasa kutengeneza movie/Film ili kudocument hili suala ambalo limevuta hisia za watanganyika wengi - si kwa sababu Mwangosi alikuwa Mwandishi wa habari - la hasha bali ukatili wa uuaji uliofanyika dhidi yake akiwa kazini. Wanahabari wengi wamekuwa wakidhuriwa kwa aina moja ama nyingine, kama sio kupigwa basi kudhuriwa mwili kama vile alivyotokea kwa aliyekuwa mhariri wa gazeti la Mwanahalisi - Said Kubenea.

  Hii Movie itabakia kuwa hazina kwa vizazi vilivyopo na vijavyo - Structure yake ibebe scene za ukweli kutokana na picha mbali mbali zilichukuliwa wakati wa matukio wakati wa uhai wake - halafu ichanganywe na matukio ya kuigiza huku ikizingatiwa theme zima ya presentation.

  Tuna wataalamu wazuri wa kuandika script- waongozaji wazuri, na pia waigizaji wazuri. Picha ianzie mbali kidogo kabla haijatua kwenye press conference iliyofanyika kabla ya tukio la mauti lilimkuta jioni yake - na pia iendelee kwenye mazishi yake na pia ikishusha matukio baada ya mazishi (kama hoja za serikali, maandamano ya wanahabari n.k).

  Haya mamabo yamekuwa yakifanyika - kwa wale ambao wamekuwa kwakifuatilia sana movies watakumbukuka kuwa baada ya mauaji ya kimbari yalikifanyika kule Rwanda, movie ana documentary mbali mbali zilifanywa - picha kama HOTEL RWANDA, SHOOTING THE DOGS, AFTER 14TH APRIL. Pia hata matukio ya mauaji ambayo yalikuwa yakifanywa na Utawala wa makaburu Afrika Kusini - Tumeiona documentary and movies mbali mbali zikitengenezwa. LETS Tanzanian try do do this.

  Sijajua upinzani utakaopatikana kutoka kwa Serikali. Lakini hii ni wazo langu

  Wana JF - (waandaji wa filamu, waongozaji, waigizaji, wanahabari n.k) hebu itupieni macho hoja hii

  Nawakilisha
   
 2. King Kong III

  King Kong III JF-Expert Member

  #2
  Sep 13, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 25,153
  Likes Received: 2,402
  Trophy Points: 280
  Good idea sema tatizo hilo swala lipo mahakamani.
   
 3. Kaka Sam

  Kaka Sam JF-Expert Member

  #3
  Sep 13, 2012
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 543
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  gooooood idea, itabidi tumtafute mtu atakae vaa uhalisia wa Mpiganaji Mwangosi... sura na umbo vifanane kidogo, eneo la tukio liwe kule kule nyololo
   
 4. Challenger

  Challenger Member

  #4
  Sep 13, 2012
  Joined: Sep 5, 2007
  Messages: 53
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Mdau Kama Sam,

  Baadhi ya sehemu ya hiyo movie kufanyikia Nyololo ni muhimu kubeba kile nilichokiita uchanganyaji wa hii movie ya matukio na sehemu HALISIA na zile za kuigiza. Iwapo usalama utakuwa mdogo basi tutapitisha kopo la mchango ili tu-sponse hata ikafanyikia nje ya nchi
   
 5. kisugujira

  kisugujira JF-Expert Member

  #5
  Sep 13, 2012
  Joined: Aug 13, 2012
  Messages: 769
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Good and presentable idea. Wadau lifanyieni kazi suala hili haraka iwezekanavyo na iwe ni kwa manufaa ya familia ya Mwangosi, chama cha waandishi wa habari na taifa kwa ujumla. Katika hili kusifanyike usanii wowote ule.Nafasi ya RPC Kamhanda niwekeni mimi.
   
Loading...