(e) Wakuu wa mikoa na wakuu wa wilaya wasiteuliwe na raisi bali wagombee kama wabunge.
Wakati wa maneno matupu umepitwa na wakati, lazima tuweke vitendo.
Hii mada yaweza kuwa ndio chanzo cha mabadiliko kama tutaweka shime, na ili kupata mtiririko mzuri ningependa mada hii tuijadili kipengele kwa kipengele, ni vyema tukaipitia katiba ili michango yetu iwe ni ya kujenga.
Admin. naomba uingilie kati ili mwisho wa siku, kama sheria inaruhusu tuoa draft ya katiba iliyoandaliwa na JF kisha tuisambaze kwa wadau wachangie zaidi na kuiboresha. katiba hii itawekwa wazi kama watawala wakiamua kuchukua sawa, wakigoma iko siku tutapata kiongozi atakeyeifanyia kazi.
Mfano, sura ya pili ya katiba yetu inazungumzia Serikali ya jamuhuri ya Muungano, hapa tunaweza kujadili kwa undani muundo wa serikali tunataka uweje, uteuzi wa viongozi, miiko ya uongozi.
Vili vile kazi mke wa rais zitamkwe wazi kwenye katiba
Kichuguu,
Nipo nawe bega kwa bega! safi sana.
Kazi ndio kipimo cha Utu,
Hoja yako kuhusu waziri mkuu ni muhimu sana kwa sababu inaonyesha hakuna sheria inayombana waziri mkuu kutokuwa mbunge akiwa bungeni ila bado hujisikia kama serikali ipo juu ya bunge wakati wote na kuwa bunge sio baraza huru ila chini ya serikali.
Inatakiwa sheria ama utaratibu ambao unahakikisha kuwa waziri mkuu ni mwakilishi wa serikali bungeni. nadhani pia nguvu yake ktk kujibu hoja itapungua sana kama mawaziri wote walioteuliwa hawatakuwa kati ya wabunge.
Sam,
Mjomba hilo swala la wakuu wa mikoa na wilaya kusema kweli gumu sana kulipatia dawa. Nadhani kuchaguliwa na wananchi inaweza kuwa sii mbaya sana ikiwa huyu RC lazima awe na kiwango fulani cha ELIMU, pia sharti kubwa zaidi ni mkazi wa sehemu hiyo. Kuwepo na sifa fulani ambayo wababaishaji sii vigumu kuwa nayo.
Invisible,
Mimi nakubaliana na ushauri wa Mgumu, ila tu tuwe makini tusije poteza baadhi ya maelezo yaliyotangulia. Mwanakijiji, bingwa wetu weka mavituz!
Invisible, hapo zamani kulikuwa na duka la vitabu vya serikali somewhere along Samora Ave... ukienda hapo bila ya shaka unaweza kupata nakala ya Katiba.. ila sijui kama Samora Avenue bado ipo, kama bado haijauzwa kwa wachimba madini!