redSilverDog
JF-Expert Member
- Sep 18, 2010
- 470
- 77
Utafiti nilioufanya NIMEGUNDUA watanzania takribani 70% hawajui KATIBA ya nchi inasema nini! 50% hawajawahi hata kuishika KATIBA hii tuliyonayo!.
Je, nini sababu za watanzania kutokuisoma KATIBA? Wakati inauzwa kwa Tsh 5000/=tu? Je, kuna haja ya kuwauliza kama wanataka KATIBA MPYA wakati iliyopo hawaisomii? Nini kifanyike ili kujenga UTAMADUNI wa kusoma KATIBA?
Mwaka huu tutayaona ya Kenya. Tume ya Uchaguzi itamtangaza JK mshindi usiku wa manane na hapo hapo ataapishwa hata kama atakuwa hospitali? Akishatangazwa na kuapishwa kazi imeisha, tunaye Rais. Hapo sasa!!! Tunanyamaza???
Pamoja na mahakama kupigwa "stop" na katiba kupokea, kusikiliza na kuamua migogoro ya kura ya Uraisi lakini uzoefu wa huko nyuma waonyesha mahakama kuu yaweza kuyapokea malalamiko ila ushahidi ndiyo huwa tatizo la kuendelea na utatuzi wa migogoro ya kura ya Uraisi.
Na ushahidi unaotakiwa ni wa kupinga utaratibu tu na wala siyo mambo mengineyo………………Ipo kazi…………………..
Tuombe Mwenyezi Mungu atuone huruma na haki itendeke
"When a candidate is declared by the Electoral Commission to have been duly elected in accordance with this Article, then no court of law shall have any power to inquire into the election of that candidate."
Ibara ya 41(7) yasomeka hivi:-
Hii Ibara haizuii Mahakama kuu kuchunguza kama taratibu za kisheria za kumtangaza mgombea kuwa Rais zilifuatwa. Huu ndio uamuzi wa Mahakama Kuu iliyoutoa mwaka 1995 wakati upinzani ulipokimbilia mahakamani.
Mfano kama NEC haikuheshimu matokeo yaliyopo machoni pao na kumtangaza mgombea ambaye alishindwa mahakama inao uwezo wa kutengua uonevu uliofanywa na NEC na kumtangaza yule ambaye ndiyo chaguo la watanzania walio wengi.
Hivi vifungu, usivisome haraka haraka ukafikiri NEC waweza kufanya watakavyo bali wanapaswa kutenda haki kulingana na sheria ya uchaguzi.
Sheria ya uchaguzi inaikataza NEC kumtangaza mgombea ambaye hakupata kura nyingi kuwashinda wenzie kuwa ndiye mshindi.
Katiba ya Jamhuri ya Muungano inasema.....
41. -(7) Iwapo mgombea ametangazwa na Tume ya Uchaguzi kwamba amechaguliwa kuwa Rais kwa mujibu wa ibara hii, basi hakuna Mahakama yoyote itakayokuwa na mamlaka ya
kuchunguza kuchaguliwa kwake.
42.-(1) Rais mteule atashika madaraka ya Rais mapema iwezekanavyo baada ya kutangazwa kwamba amechaguliwa kuwa Rais, lakini kwa hali yoyote itabidi ashike madaraka kabla
ya kupita siku saba.
Hii ndiyo fimbo ya CCM - wanajivunia "tume yao ya uchaguzi". Mpaka hapo tutakapokuwa na tume huru ya uchaguzi tuendelee kuhesabu maumivu!
Heshima mbele wana Jamvi.
Mimi naomba kufahamu katiba inasemaje kama mtu anataka kumchagua Rais mbali na kituo alichojiandikisha, Maana logically, Rais na wa Watanzania wote na anaruhusiwa kuchaguliwa na kila aliye na kadi halali ya kupigia kura.
Je kwa maana hiyo wanachuo hawawezi kutumia fursa hiyo kufanya uchaguzi wa Rais huko waliko?
Nijuavyo kuna watu wengi wanaweza kukosa kupiga kura kwa sababu mbalimbali, ikiwepo kusafiri kikazi, emergency, kwa wafanyabiashara na wanachuo ambao wanaelekea kunyimwa haki yao ya msingi.
Tafadhali naomba ufafanuzi kwa hili..sijui katiba inasemaje kwa hili.