Mkuu badilisha kauli hapo kwenye red..! Wote wamekalia kigogo kwa nyuma..! Sisi hali hii huwa tunaiita dhooful khali..!
Mou ashinde asishinde next season yupo EPL, nyepesi nyepesi zinadai RM wameshanza mazungumzo na Carlo AncellotiNajua Real Madrid bado wana nafasi kubwa ya kuingia fainali kuliko Barca lakini haya matokeo yatakuwa yamekata ngebe za Mourinho. Ile safari ya kukimbia Santiago Bernabeau imesharahasishwa kwa kipigo hiki. Sitokushangaa kibarua cha Mourinho kuota mbawa wiki ijayo.
Kwa tathimini yangu iliyoenda shule na ambayo imejitosheleza ni kwamba wote hawana nafasi ya kusonga mbele..! In terms of comparison na kwamba mpira huwa unadunda basi ni rahisi kwa barca kutinga fainali kuliko real..! Take it from me ule mziki wa Borusia dortmund unanikumbusha mbali sana na madrid wanagongwa tena mzigo at home ground..!Kuna kitu gani kigumu ulichoshindwa kuelewa nilichomaanisha mkuu? Real Madrid bado wana nafasi kubwa ya kuingia fainali kuliko Barca kwa sababu wanahitaji kushinda magoli 3-0 ndani ya Santiago Bernabeu wakati Barca wanahitaji kushinda 5-0 ndani ya Camp nou. Nadhani unajua kuhesabu 1 mpaka 5.