Mount Ukombozi Hospital mnahatarisha maisha yetu, Waziri wa Afya tusaidie

Koala

Member
Aug 28, 2011
97
107
Habari za leo wanajamii.

Mie ni mtumiaji mzuri wa usafiri wa mwendokasi. Na kituo changu kikuu ni Morocco. Kuna hospitali iko hapo pembezoni mwa daraja upande wa kushoto. Kila siku huchoma taka taka na uchafu wa hospitalini sehemu ya wazi kabisa ambapo wasafiri tunashukia kutoka darajani. Hii ni hatari maana taka taka hizi zinachomwa sehemu ya wazi kabisa,na moshi unasambaa kila mahali.

Kwa uelewa wangu vitu hatari kama hivi hutakiwa kuchomwa sehemu ambayo hakuna watu au makazi na watakiwa kuwa na kijumba nadhani kinaitwa incinerator kwa ajili ya kuchomea uchafu huo hatari. Naomba wahusika wa wizara ya Afya walifuatilie jambo hili. Maana ni hatari kwa sisi wapita njia na hata kwa watoto kuokota taka zinazosalia bila kuungua zikaisha.
 
Back
Top Bottom