MOU iliyosainiwa Tarehe 26 Oktoba 2014 ni Sanda ya Marehemu UKAWA baada ya kifo chake

Wengi tulijua UKAWA utakoma tu baada ya Bunge la katiba kuikabidhi ile Rasimu yetu kwa Mwenyekiti wetu wa chama Taifa - ala kumbe mambo yamebadilika kabisa, kinachotustusha zaidi ni kwamba ushirikiano wao huu eti utaenda hadi uchaguzi Mkuu mwakani - kweli hili limetuchanganya mno.

Hapa inabidi tutafute kauli mbiu mzuri itakayowavuta wananchi watuamini kwa mara nyingine kuwaongoza - Ile dhana tuliyotumia kuwatokomeza hawa wapinzani ya udini, ukabila, ukanda naona watanzania wameshaishtukia tayari.

Inabidi tujipange haraka mno ndugu zangu, tutajaribu pia harakati ya kuwagawa hawa jamaa kwa mbinu mbali mbali ili wafarakane kabla ya June 2015 - Hili jambo kweli limetuchanganya sana, jamaa wanataka kutupiga counter attack dakika hii ya 89. Hatuwezi kukubali kiurahisi - tutapambana.
 
wewe ni mmoja wao wasiojitambua. Ni sheeeddaaa!!! Kuwepo watu kama wewe

Una kila sababu ya kuendelea kuishi kwa wazazi wako au mashemeji zako, bado hujakua, hivyo hata maana ya maisha huijui. Mtu mzima, mwenye busara zake, aliyecomitted kwenye maisha, mwenye familia, hawezi kutumia maneno hayo.
 
Kujua kama ni za uso au kapiga ukuta, subiria wakati utoe matokeo. Usiwe mganga wa kienyeji.
Mkuu, mbona hata kwenye bunge la katiba mmepigwa za uso licha ya tambo zenu kuwa akidi haitapatikana?
 
Mpwa wangu Chabruma, kwa hali ilivyo hata kichaa hawezi kuuliza CCM inakufaje, only that anayekufa hawezi kukubali kuwa anakufa. Niko tight kwa sasa but natamani ningetafuta thread mbali mbali za failed state, niikipata nitakuwekea hapa au jkuna thread niliwahi kuandika pia kuhusu stage za mtu anayekaribia kifo na uhusiano wake na CCM

Siwezi kuzibeza sana hoja za Chabruma kishabiki tu lazima tuangalie na logic zilizomo kwenye uzi wake. Kwa kweli kuunganisha nguvu kupigana na adui ni jambo jema. Kwa kipindi kirefu wananchi walipiga kelele vyama viungane ili vishinde chaguzi badala ya ya kugawa kura za upinzani. Ila upinzani wasibweteke kuungana kwao tu. Lazimq wafanye kazi usiku na mchana kueleza kwa wananchi haswa wa vijijini uzuri wa sera zao na watakachowafanyia wakiwaamini kuwapa dola (Elimu ya uraia). Wafungue matawi kila kata,tarafa na wilaya na ruzuku za vyama zielekezwe huko kusaidia kutoa elimu ya uraia kwa wananchi. Wabunge wao waishi na wapiga kura wao kwenye majimbo na sio kujichimbia Dsm. Ni ukweli ukawa wanapendwa na vijana wengi sasa wahakikishe wote wanaandikishwa kwenye daftari la wapiga kura na wanahamasishwa kwenda kupiga kura. Wasisahau kuwa nao ccm watatumia mbinu hizo hizo kujiongezea wapiga kura na kwamba wao tayari wana nyenzo na uwezo mkubwa kifedha. Mawazo ya kujiaminisha ccm imechokwa hayasaidii na yanalemaza na kudumaza. Uchaguzi mkuu wa 2010 wapiga kura ml.13 walioandikishwa hawakujitokeza kupiga kura. Hapa ndipo viongozi wa ukawa na ccm wanapotakiwa kujikita. Miongoni mwao walikosa elimu ya uraia kwa wapiga kura na wengine waliona hata wakipiga kura bado ccm itashinda tu. Sababu zao za wakati ule zinaweza kubadilika kwa kuamini baada ya muungano wa ukawa wakiwapa kura wanaweza kushinda. Hii ni advantage kwa ukawa wakilifanyia kazi vizuri. Ukawa wajiepushe sana na usaliti miongoni mwao. Teuzi za wagombea kwenye majimbo zifanyike kwa uangalifu mkubwa na maridhiano.Wasimamizi wao wa kura wachujwe kwa umakini mkubwa kwani eneo hili ni hatari sana na ikieleweka kwa sasa atakuwepo mwakilishi mmoja tu kwenye chumba cha kura. Viongozi watakaosimama kwenye majukwaa ya kampeni watumie lugha laini kwa wananchi. Ukawa waelewe kuitoa ccm madarakani ni kazi nzito na hata kama hawatafanikiwa ngazi ya uraisi watakuwa wamejiongezea majimbo na viongozi wa vijiji,mitaa na vitongoji na ni mwanzo mzuri kwao.
 
Stupidity is when you talk a lot but say nothing.

Maelezo yako yamekaa zaidi kiutabiri (kama ule wa nyota wa Yahaya) kuliko uchambuzi. Tusubiri tuone utimilifu wa uganga wako. Yawezekana unatamani iwe hivyo hata kama haitakuwa hivyo.

Ungekuwa japo una uwezo wa kufanya utafiti angalao hata kwa kiwango cha 10% ungeleta hapa angalao matokeo ya uchaguzi wa 2010 katika majimbo ambayo yalichukuliwa na CCM. Ungejumlisha kura walizozipata CUF, CHADEMA, NCCR na NLD halafu ungelinganisha na zile walizozipata CCM. Hapo ungeweza kusema kuwa kwa kumbukumbu hizo, hata hawa wakiweka kura zao pamoja hazitafikia zile za wafia CCM. Japo nayo haiwezi kuwa msingi wa hoja kwa 100% maana watu hubadilika kutokana na wakati lakini angalao ungeonekana una basis, siyo hii takataka uliyoiweka hapa.

Kuna maeneo ni dhahiri kuwa CHADEMA na CUF, kila kimoja bila ya ushirikiano kitashinda. Hayo ndiyo maeneo uliyoyataja. Lakini kuna maeneo ambayo CHADEMA au CUF pekee yake ni vigumu kuishinda CCM lakini wanaweza kushinda kiurahisi sana CCM kwa kushirikiana.

Unapoonekana wa ajabu ni pale bila aibu unaposema viongozi ndiyo wameamua wakati kila chama kimefanya mikutano na kamati kuu zao kabla ya kufikia hayo makubaliano. Kuna ushabiki unaofanyika huku ukilinda haki ya kufikiri lakini pia kuna huu ushabiki unaoleta upofu wa akili na macho.

Well said.. na cha kuongeza ni kwamba chabruma anashindwa kuelewa kuwa umoja huu ndio utakaoondoa hizo tofauti alizozitaja automatically kwa sababu sasa watazungumza kama wapinzani(UKAWA) na sio chadema wala cuf. Akumbuke hata Nyerere alisema kuwa ndani ya muungano kuna watanganyika na wazanzibari, na bila ya muungano kuna waunguja na wapemba! mi nadhani move yao ni nzuri kama wana nia ya dhati.
 
Stupidity is when you talk a lot but say nothing.

Maelezo yako yamekaa zaidi kiutabiri (kama ule wa nyota wa Yahaya) kuliko uchambuzi. Tusubiri tuone utimilifu wa uganga wako. Yawezekana unatamani iwe hivyo hata kama haitakuwa hivyo.

Ungekuwa japo una uwezo wa kufanya utafiti angalao hata kwa kiwango cha 10% ungeleta hapa angalao matokeo ya uchaguzi wa 2010 katika majimbo ambayo yalichukuliwa na CCM. Ungejumlisha kura walizozipata CUF, CHADEMA, NCCR na NLD halafu ungelinganisha na zile walizozipata CCM. Hapo ungeweza kusema kuwa kwa kumbukumbu hizo, hata hawa wakiweka kura zao pamoja hazitafikia zile za wafia CCM. Japo nayo haiwezi kuwa msingi wa hoja kwa 100% maana watu hubadilika kutokana na wakati lakini angalao ungeonekana una basis, siyo hii takataka uliyoiweka hapa.

Kuna maeneo ni dhahiri kuwa CHADEMA na CUF, kila kimoja bila ya ushirikiano kitashinda. Hayo ndiyo maeneo uliyoyataja. Lakini kuna maeneo ambayo CHADEMA au CUF pekee yake ni vigumu kuishinda CCM lakini wanaweza kushinda kiurahisi sana CCM kwa kushirikiana.

Unapoonekana wa ajabu ni pale bila aibu unaposema viongozi ndiyo wameamua wakati kila chama kimefanya mikutano na kamati kuu zao kabla ya kufikia hayo makubaliano. Kuna ushabiki unaofanyika huku ukilinda haki ya kufikiri lakini pia kuna huu ushabiki unaoleta upofu wa akili na macho.
yametimia aliyotabiri
 
Mmeshaanza kuweweseka na UKAWA. UKAWA mnadai ni mfu sasa iweje tena muanze mashambulizi dhidi ya mfu anayeandaliwa mazishi!? Kila lenye mwanzo halikosi mwisho na mwisho wa Serikali hii dhalimu inayong'ang'ania madaraka kwa mabavu umewadia. Ole wenu mafisadi wote ndani ya hii Serikali dhalimu.
?? nani anaongoza serikali
 
Back
Top Bottom