Motorola wamerudi bhana!

Teknolojia ni Yetu sote

JF-Expert Member
Apr 28, 2020
445
763
Motorola miaka ya nyuma walikua wanakimbiza sana Kwenye soko la kuuza simu ulimwenguni Kuna kipindi upepo ukakata na kushuka Kwenye soko siku ya Jana Motorola wamerudi tena ulimwenguni.

Unachokiona hapo sio saa aina ya smartwatch hapana ni simu ya smartphone toka Motorola. Kupitia onyesho la Lenovo Tech world 2023 Motorola walionyesha simu mpya.

Motorola%20%E2%80%93%201.jpg


Ni simu ambayo unaweza sema ni foldable lakini ni smartphone ya kawaida ila imekuja na maajabu yake unaweza kuikunja utakavyo Yani unaweza ifanya saa pia unaweza tumia kama simu bila shida yoyote.

kioo chake ni Poled display kikiwa ni full Hd , unaweza kutumia ikiwa imenyooka kama zilivyo smartphone Zingine pia unaweza kutumia kwa kuikunja na kuiweka Kwenye meza nk.

Matilio yaliyojengewa nayo inakupa uwezo wa kuiweka Kwenye mkono na kuiva kama saa alafu ukatembea nayo bila kuanguka.

Pia Motorola wametambulisha akili bandia ambayo inakupa uwezo wa kutengeneza mitindo Tofauti kupitia picha uliyopiga au kuiweka labda umevaa vazi Fulani basi itakusaidia kukuletea style tofauti utaweza kuiweka Kwenye wallpaper ya simu yako.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom