Moto wawaka kati ya Viongozi wa CCM manispaa ya Tabora vs Mkuu wa Wilaya ya Tabora Komaya Kitwala

Kasegela

Senior Member
Mar 24, 2019
127
261
Chanzo ni vitambulisho vya mjasiliamali (vile vya 20,000/=

Mkuu wa wilaya kafanya kikao na bodaboda na waendesha bajaji na wale waendesha baiskeli(daladala baiskeli) kuwa kila mmoja lazima alipe sh.20000 ya kiparata(Kitambulisho cha mjasiliamali.

Vijana wa bajaji wamegomea kulipa kwa madai kuwa tayari wanazo leseni za TRA,wanazo leseni za Manispaa,na wanalipa pesa ya Tarura Tsh 500/= kila siku,iweje walazimishwe na Mkuu wa wilaya kulipa kitambulisho?

Pamoja na hayo Mkuu wa wilaya analazimisha watumishi kutumia mabavu kuuza kitambulisho,kuwa mtu akiutwa anauza chochote basi anyang'anywe bidhaa zake mpaka atakapo lipia 20,000/=

Mama Ntilie wanatozwa kitambulisho na wala hawana tatizo,lakini cha ajabu wanaambiwa kama ana waosha vyombo wawili basi na wao sharti awalipie na DC anapita kukagua kama kweli wamelipa

Watendaji kata wanaoshindwa kukamata watu na. Kutupa ndani wao ndio wanatupwa ndani,wanaitwa mpaka vikao vya Saa 4 usiku na kuwatishia kuwafukuza kazi.

Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Tabora kwa muda mrefu kimemlalamikia huyu Mkuu wa wilaya,lakini Dr.Bashiru anamkingia kifua ,chama leo kimafanya press ili kujihami na uchaguzi kwakuwa wananchi wengi wanamlalamikia lkn DC kavamia kikao akaiwa na vyombo vya dola kuwatisha viongozi wa CCM hasa katibu wa chama.

Kitwala Komanya anaichonganisha Serikali na wananchi,hajui kushauri yeye anajua vitisho na kutukana watu.

Watumushi wanadhalilishwa kila siku sasa kahamia kwenye chama.

Video
 
Shamba la bwana kheri,mbuzi wa bwana kheri yote kheri,,,,,,,Amini nakwambia ukimaliza shule ndio utaanza masomo
 
Shamba la bwana kheri,mbuzi wa bwana kheri yote kheri,,,,,,,Amini nakwambia ukimaliza shule ndio utaanza masomo
 
500 ni ushuru wa tarura, yaani kuchangia kuboresha miundombinu ya barabara siyo TRA kwani wana leseni za biashara za TRA na leseni za ushuru wa manispaa.
haya maushuru yalishakatazwa ndio maana kukawa na vitambulisho.
 
Kama Lissu alijua kuwa hiyo ndio kero ya wanyonge wengi maana kila akifika mahali hiyo ndio fimbo yake na watu kwasababu wanaichukia hiyo ya vitambulisho vya 20000 basi wanashangilia na kupiga makofi aisee lisu ww ni kiboko mbona utazizoa kura za wanyonge hawa
 
Tulieni tu tuliwaambia toka mapema huyo mkuu wa wilaya ni utoko mkasema tuna wivu ,wavivu .Twendeni tu.
 
Back
Top Bottom