Moto wa kupima HIV ni balaa!

Moto wa kupima HIV ni balaa!

incredible terminator

JF-Expert Member
Joined
Aug 1, 2016
Posts
2,536
Reaction score
4,304
Habari zenu Wakuu.
Duu aseeh asikwambie Mtu vibe la kusubiria Majibu Ya Vipimo Vya HIV.

Ndo maana mwanzo nilikuwa nakataa hizi kazi
mimi wakuu kupima kwangu nilikuwa nawakilishwa na wife akipata ZAIGOT nilikuwa namsukumia akipima akileta majibu Basi freshi najijua kuwa na mimi miko freshi,

Nakumbuka kuna siku clinic walimlazimisha kuwa lazima niende nikwamwambie kawambie wewe ni single mother Baba wa mtoto hayupo, Kisa tu nisiende kupima asee....

Sasa leo nimeamini nguvu ya ushikaji, aseeh nimemsindika mshikaji kwenda kupima, Kufika sijui ilikuwaje nikajikuta nimekubali kutoa dam kwa ajili ya vipimo...

Duu wakuu vibe la kusubiria majibu nawambia asikwambie Mtu, leo nimekumbuka hadi yule beki tatu alienifundisha kugegedana, tulikuwa wapi saangapi na ilikuwa mda gani,

Yaani Mda wote nipo kwenye Benchi la kusubiria majibu nilijikuta nipo kama naangalia movie za porn vile...

Yaani nilijikuta nakumbuka video za migegedano ambayo nilishawahi kufanya, Mara linakuja hili, Mara lile, mara yule...Mara sjui huyu aseeh mungu atusamehe tu,

Yaani hadi nikajikuta namkumbuka yule comando alienikosa ngumi siku ile alionifuma na Dem wake kuwa kuwa kwanini asingeniua tu

Basi bana shetani nae anamaksudi hadi anakera, Si wazo likanijia kuwa naota pale kwenye benchi asee nikasema ngoja nirushe ngumi nione labda nipo usingizini asee nimeshtushwa na kilio cha Mtoto pembeni yangu,

Mungu wangu kumbe nilikuwa nimekaa kati kati ya Mama wenye watoto nao wanasubiria huduma,
Kumbe Ngumi yangu imetua kwenye kisogo cha mtoto aliebebwa na mama yake.

Aseeh yaani mda najitetea kusema uongo sory nilikuwa najinyoosha gafla naskia jina lagu ndo naitwa kuchukua majibu Aseeh, Hata sijui yule mama amenichukuliaje pale...

Ila ishallah, Good news nipo fresh licha ya kucheza ligi kibao za mchangani,

Hapa nimeamini ile ndoto yangu ya kuwa Mhubiri nikalitangaze neno la mungu kila kona ipo siku utatimia tu,

Saizi nasema wanawake wote Pita Kushoto[emoji125] [emoji125] [emoji125]
 
Ndoto inetimia hongera,
Poa tunasogeza siku best
ahsante,ni kweli mkuu walau ka msongo ka mawazo na sukari ya kupanda bila taarifa vinategea kidogo,ukisoma nyuzi za wadau mbali mbali jf kama hawa akina youngtozih
 
Mara ya kwanza pale muhimbili kitengo cha upimaji, sitasahau, yaani saa moja lkn ilikuwa sawa na mwaka. Baada ya majibu nilivuta pumzi moja hatarii na kunyoosha mikono juu ishara ya kumshukuru Aliyejuu hahaha
 
Mara ya kwanza pale muhimbili kitengo cha upimaji, sitasahau, yaani moja lkn ilikuwa sawa na mwaka. Baada ya majibu nilivuta pumzi moja hatarii na kunyoosha mikono juu ishara ya kumshukuru Aliyejuu hahaha
mkuu hii kitu aseeh....basi tu
 
Usiombe kuwa Wewe bola usikie. ila cha ajabu wanawake hili swala kwao ni rahisi sana kuliko kuchora O
 
Back
Top Bottom