Moto sasa walipuka ushuru wa forodha | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Moto sasa walipuka ushuru wa forodha

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Msharika, Jul 9, 2010.

 1. M

  Msharika JF-Expert Member

  #1
  Jul 9, 2010
  Joined: May 15, 2009
  Messages: 936
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Yetu macho, katika hili na hawa ndugu wenye asili ya kihindi , tiba itapatikana?


  SAKATA la ufisadi katika kitengo cha ushuru wa forodha cha Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kwenye Bandari ya Dar es Salaam linalohusisha ukwepaji kodi wa mabilioni limeingia sura mpya, Raia Mwema likithibitishiwa kuwa hatua zimeanza kuchukuliwa na tayari baadhi ya maofisa wameenguliwa kwenye nyadhifa na kutakiwa kujieleza ndani ya siku 14.

  Katika maelezo ya uthibitisho kwamba hatua zimechukuliwa, Mwenyekiti wa Bodi ya TRA, Dk. Marceline Chijoriga, amelieleza Raia Mwema mapema wiki hii kuwa, aliyekuwa Kamishna wa Ushuru wa Forodha ameengeliwa katika wadhifa huo ili taratibu za uchunguzi dhidi ya tuhuma zinazomhusu pamoja na wahusika wengine kukamilishwa.

  Kwa mujibu wa habari za uchunguzi wa muda mrefu wa gazeti hili, ufisadi wa mapato ya serikali katika Bandari ya Dar es Salaam imekuwa ukihusisha kampuni moja inayojihusisha na uuzaji wa vifaa vya nyumbani iliyoanza shughuli zake hizo mwaka 2004, ikiendeshwa na wafanyabiashara wenye asili ya kiarabu wanaotajwa kushirikiana na baadhi ya viongozi na watendaji waandamizi wa TRA kuiibia nchi mapato.

  Katika matoleo yake ya mwishoni mwa Mei na mwanzoni mwa Juni, mwaka huu, gazeti hili liliandika habari inayohusu wizi wa mapato kwenye Bandari ya Dar es Salaam, ambapo kampuni moja binafsi imekuwa ikisaidia wafanyabiashara wengine kukwepa mapato kwa mabilioni.

  Lakini katika mazungumzo yake na Raia Mwema, katika umakini mkubwa unaozingatia wigo wa sheria za kazi, Dk. Chijoriga alisema; “Tumeanza kuchukua hatua…ingawa ni za kukamilisha uchunguzi wetu kwa sasa huwezi kusema moja kwa moja fulani ni mhusika wa matatizo hayo…bado ni mtuhumiwa,” alisema na kuongeza kuwa;

  “Internal Audit TRA (kitengo cha ukaguzi wa ndani-TRA) ilifanya kazi yake tangu Aprili na kuwasilisha ripoti yake kwangu kuhusu upotevu huo wa mapato…sasa kuna wahusika wanatajwa ambao wako katika maeneo mawili tofauti ya ajira. Wapo wahusika ambao ni wafanyakazi wa TRA lakini waajiriwa wa bodi hawa ni makamishna na naibu makamishna na hata mameneja, lakini wapo pia wahusika wengine ni walioajiriwa na menejimenti ya TRA,”

  “Sasa kwa taratibu za kazi, mimi ambaye ni mwenyekiti wa bodi nashughulikia hawa ambao mikataba yao ya ajira wamepewa na bodi na menejimenti inashughulikia wengine. Hatua tulizokwishachuku hadi sasa ni kuitaka menejimenti imwondoe kamishna wa forodha Bateyunga impangie kazi nyingine tofauti wakati uchunguzi unaendelea.

  “Lakini pia Bateyunga tumempelekea tuhuma zinazomhusu kama zilivyoainishwa na Internal Audit Report ili azijibu ndani ya siku 14 kama sheria za kazi zinavyotaka, baada ya majibu yake tutajua nini cha kufanya. Kwa hiyo kwa sasa hatuwezi kusema ni kweli amehusika hadi tupate maelezo yake na wenzake wote,” alisema Dk. Chijoriga.

  Alipoulizwa ni kwa nini mtuhumiwa anaendelea kufanya kazi ingawa katika majukumu tofauti ndani ya mwajiri wa awali na hatari iliyopo ya kuharibu ushahidi, alisisitiza wanazingatia sheria za kazi. Sehemu ya mazungumzo hayo kati ya Dk. Chijoriga na mwandishi wa gazeti hili yalikuwa hivi.

  Raia Mwema: Kwa nini mtuhumiwa anapewa majukumu mengine na mwajiri yule yule anayemtuhumu na ambaye pia anamchunguza?

  Dk. Chijoriga: Ni lazima tufuate sheria za kazi zinavyotaka si utashi wangu binafsi au bodi. Sheria za kazi zinatutaka kutomchukulia hatua kali zaidi bila kujiridhisha kwa kusikiliza maelezo yake. Kumbuka ripoti yenye maelezo ambayo anatakiwa kuyajibu sio hukumu isipokuwa imebeba tuhuma tu.

  Raia Mwema: Huoni anaweza kutumia mwanya huo kushinikiza kuvuruga ushahidi na hasa ikizingatiwa kuwa mtandao wa watuhumiwa ni mkubwa ndani na nje ya TRA…kwa nini mmeshindwa kumsimamisha kazi pengine kama ilivyotokea kwa ofisi ya Ardhi Wilaya ya Kinondoni?

  Dk. Chijoriga: Sisi hatuwezi kufunga ofisi ghafla tunahitaji mapato ndiyo maana tumemwondoa pale alipokuwa mwanzo. Lakini hiyo ni sehemu moja ya hatua zinazoweza kuchukuliwa baadaye.

  Katika hatua nyingine, alipoulizwa kuhusu hatua dhidi ya wafanyabiashara waliohusika kukwepa kodi halali kupitia kampuni hiyo ya vifaa nyumbani, Dk. Chijoriga alisema uchunguzi utafanywa na kwamba wahusika watapaswa kulipa kiasi chote cha kodi walichokwepa tangu walipoanza mchezo huo hadi sasa.


  source:Moto sasa walipuka ushuru wa forodha
   
 2. M

  Mkandara Verified User

  #2
  Jul 9, 2010
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  TRA kwa ujumla kumeoza huyu ni Bangusilo tu!...
   
 3. B

  Bulesi JF-Expert Member

  #3
  Jul 9, 2010
  Joined: May 14, 2008
  Messages: 6,447
  Likes Received: 414
  Trophy Points: 180
  Mara nyingi Bodi na management ya taasisi wakikaa kwa muda mrefu matokeo yake ndio hayo!! Watu huzoeana na inakuwa business as usual. Hawa viongozi wa TRA ni wateule wa viongozi ambao walikuwa mafisadi kwahiyo wao ni masalia ya hao mafisadi waliowateua ambao wengine bado wana kesi mahakamani. Mafisadi bado wanawatumia kwa shuhuri zao na hizo ndizo zinaikosesha nchi mapato. Serikali hii isingekuwa mifukoni mwa Mafia ya Tanzania hawa jamaa wangefukuzwa kazi siku nyingi.
   
Loading...