oba
JF-Expert Member
- Oct 31, 2010
- 310
- 66
Wanajamvi,
Katika upekuzi wangu wa hapa na pale nimepata wazo kuwa viongozi wengi hasa wa bara la afrika wana IQ ndogo. Hii ni kutokana na kuwa watu wenye IQ ndogo tangu wakiwa wadogo au katika sule za awali na hata vyuo vikuu huwa ni wachakalikaji, ni watu wenye bidii ili watoke katika maisha, wanapenda kujipendekeza kwa watu na kwa watawala, ni vimbelembele, ni watu ambao wanapenda watambulike kuwa wapo popote waendapo.
Watu wa namna hiyo hufanya hivyo baada ya kugundua kuwa uwezo wao ni mdogo na kwamba imewapasa kutia bidii sana. wanapofikia umri wa utu uzima huwa wanaonekana wamefika popote walipo kwa uchakalikaji, kumbe walirubuni, walifoji vyeti au hata kuiba mtihani, ukubwani wanaonekana ni watu wenye bidii na kwa sababu ya kuwa vimbelembele watu huwaona kirahisi na bila kujua huwachagua kuwa viongozi.
Watu wenye IQ kubwa ni wataratibu, wanajiamini, wanaamini watatoka bila kutumia nguvu ya ziada, hawana papala na maisha kwasababu wanajua watatoka kwasababu uwezo wanao, huwa wanajidai kuwa vyovyote vile iwavyo watafanikiwa tu. Hawajipendekezi wala kumpigia magoti yeyote, ni watu wanaofanya mambo yao kwa ukimya bila kujionyesha na huenda kila waendapo wasitambuloke kuwa wapo.
Matokeo yake huwa hawajulikani na watu wengi na hata wakijulikana huonekana kuwa si wachakalikaji na hivyo hawapewi nafasi za kuongoza. Na iwapo wakipata nafasi za uongozi huwa hawawezi kuendana na mfumo wa watu wenye IQ ndogo, mawazo yao hupingwa, na wengine hufanyiwa fitina na baadhi huuawa.
Ndiyo maana nchi nyingi za Afrika hazina maendeleo kwasababu viongozi wake wengi ni wale wasio na uwezo, majanga hayakomi kwa nchi zao na hawana ubunifu wa kukomboa nchi zao na umaskin au maafa.
Je wadhani mtazamo huo ni sahihi ukichukulia mfano wa kwetu hapa?
Nawasilisha