Moshi: Mwenyekiti adaiwa kumshambulia Mjamzito

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
3,877
6,326
Mwenyekiti wa kijiji cha Samanga Wilaya ya Moshi mkoani Kilimanjaro, Wilfredy Minja anadaiwa kumshambulia na bakora Asha Rajabu (28) na kumsababishia maumivu huku polisi wakitangaza kuanza msako wa kumkamata mtuhumiwa.

Asha ambaye amelazwa katika hospitali ya Kilema inadaiwa alikuwa ni mjamzito ambao uliharibika kutokana na kipigo hicho kile kinachodaiwa cha mwenyekiti huyo, ambaye pia inadaiwa alikuwa na bastola na alifyatua risasi hewani.

Kaimu Kamanda wa polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Ronald Makona alithibitisha kutokea kwa tukio hilo ambapo, alisema binti huyo alishambuliwa kwa bakora na mtuhumiwa huyo sehemu za makalio na mapajani na kumsababishia maumivu makali mwilini.

“Ni kweli tukio hili lilitokea Januari 24 saa 6:00 usiku eneo la Marangu Maua ambapo mwenyekiti wa kijiji alimshambulia kwa kumchapa bakora sehemu mbalimbali za mwili na kumsababishia maumivu makali,” alisema.

Kuhusu mwenyekiti huyo kutumia silaha, Kamanda Makona alisema wanamchunguza kwani tukio hilo limefika ofisini kwake jana na upekuzi unaendelea.

“Jitihada za kumtafuta na kumkamata mtuhumiwa zinafanyika na chanzo cha tukio hilo bado tunachunguza, tayari nimeshatuma timu yangu kwenda Marangu ili kujua ni kweli alikuwa na silaha hiyo na tutampekua,” alisema

Mkuu wa wilaya ya Moshi, Rajabu Kundya alikiri kupokea taarifa za tukio hilo na kwamba, amelielekeza jeshi la polisi kuchukua hatua kwa mujibu wa sheria.

“Nimewaelekeza polisi kuchukua hatua kwa mujibu wa sheria ili kila anayehusika na tukio hilo achukuliwe hatua zinasostahili,” alisema na kuongeza

“Nimesikia kuna bastola ilitumika, hilo ni kosa na polisi wazuie silaha hiyo kwanza mpaka tujiridhishe kama ni halali na kama anaitumia inavyotakiwa, kisha mengine yatafuata,” alisema Kundya.

===

Hakuna watu wanateseka kama wana kijiji wa marangu samanga,kuna dada yuko kilema hospital kapigwa na mwenyekiti wa kijiji anaitwa MC MINJA mpaka mimba imetoka anatakiwa kusafishwa,mwili mzima una makovu kama jambazi na mwenyekiti kamnyang'anya shilingi laki 3 faini yakuchelewa kufunga ofisi yake na hakuna risiti,mbaya zaidi anataishia watu na bastola hakuna kuhoji,bastola yake anaishika kama manati kila mtu anaiona,sio wakwanza huyu waandishi waje marangu samanga watetee wananchi wanateseka mpaka wazee wanapigwa balaa.
lulunation__20210208_2.jpg
 
CCM mbele kwa mbele na nasema mitano kujumlisha miwili tena.

Hawa wenyeviti hawakuchaguliwa na wananchi. Walijipitisha kwa hiyo wameota mapembe kwa sasa hamna wa kuwagusa kila mmoja anatoa matamko anavyojisikia.
 
Back
Top Bottom