Mdutch
JF-Expert Member
- Nov 17, 2011
- 214
- 77
Moshi ni mji wenye sifa ya usafi Tanzania. Zaidi ya usafi ni mji wa Mlima Kilimanjaro (The town of Mt Kilimanjaro) hivyo ni mji wa kitalii barani Africa. Pia mji huu uko kwenye mchakato wa kufanywa kuwa jiji na ndio maana umeshaanza kupanuliwa kieneo kwa kuchukua maeneo ya Moshi vijijini kama vile mabogini na Kahe.
Kinachotia aibu ni ifikapo mida ya saa moja usiku mji huu unakua giza totoro mithili ya msitu. Ni aibu kwa wageni wa ndani na nje ya nchi waingiapo ndani ya mji huu wanakumbana na kiza hiki.
Nimefika hapa kwa sherehe za kufunga mwaka na nimeona kuna haja ya CDM wanaoongoza manispaa hii kuufanya mji huu kuwa katika hadhi yake wakatii wa usiku na sio kama ilivyo sasa.