Moshi: Binti amuua Mama yake mzazi kisa Mali. Mwili wagundulika ulipozikwa baada ya mwaka mmoja

Mama kila siku anasema "mwanangu nataka uoe", "japo unaishi Moshi ila sitaki uoe Mchaga" tena kwa msisitizo huku amekunja sura anasema "sitaki kabisaaa"

Nilikua simuelewi namwambia tabia ya mtu sio tabia ya kabila ila sasa kama namuelewa hivi
 
Eeh safi hii fundisho kwa wale wazazi wanaoendelea na ule msemo wa "hizi zangu katafute zako"
Kwani uongo?! Watafute zao kweli. Hata wakiendelea kuuwa wazazi ndio itasaidia?! Ni uvivu tamaa kukosa mbinu akili duni ndio inawafanya wawe majinga kutokutafuta zao. Na wafanyayo haya wafie jela au wafe kwa kamba tu
 
Kama ulishawahi kuishi Kilimanjaro maeneo ya uchagani na Wilaya zake....ukitazama kwa umakini harakati za Wana jamii, haiba na mienendo ya Wana jamii waliokuzunguka na mitazamo yao juu ya maisha unagundua kuwa kuna tatizo mahali.

Katika hali ya kawaida wachaga ni watu wastaarabu, waungwana na wenye kujitoa sana ila tu wapo obsessed na upatikanaji wa mali......wazee wa kichaga waliihamishia obsession hiyo kwenye kupambana kila Kona ya nchi hii.....na matokeo yameonekana.....ni dhahiri kuwa ni moja kati ya makabila yaliyo fanikiwa sana kiuchumi na kielimu.

Hilo halina ubishi ukikanyaga tu mji wa Moshi utajua kuwa nipo kwenye mji wa watu waliopiga hatua kimaendeleo kuanzia ubora wa makazi ya watu, huduma za kijamii na shughuli za kiuchumi.

Uharibifu umeanzia hapa kati kati baada ya kuzuka kizazi cha vijana wavivu wasiojituma kwenye kazi na wasio na nidhamu kwenye frdha kwa kuendekeza starehe za pombe na wanawake.

Kizazi hichi Cha watu wavivu kinachoamini katika njia ya mkato kwenye mafanikio ndio kimezusha na kuzalisha matendo yasiyokuwa ya kiungwana kibinadamu kwenye jamii za kichaga na kuipaka matope.

Haya matukio ni muendelezo wa harakati za hicho kizazi na yatakuja matukio mengine mengi mpaka pale watakapo rudi kwenye mstari kuwa mafanikio ni kujituma na kuwa na nidhamu katika matumizi ya pesa.
 
Wee sema hivyo tuu....sasa mali umahangaika kuzipa ila kwa sababu ya uchoyo watoto wako wenyewe wanakuondoa. Wazazi acheni ubinafsi gaweni mali hizo
Yaan mzazi kakukuza plus kukusomesha pengine kajinyima ili mwanae akuhudumie mpaka sasa umekuwa jitu lizima yaani fadhila zote hizo bado unasema ni mbinafsi aisee utakuwa una matatizo ya akili.
 
Ni bahati mbaya tu kajulikana ndo maana anaonekana mtu wa ajabu lakin Kuna watu wengi tu Leo hii wanaonekana mashujaa na watafutaji lakini nyuma ya mali zao Kuna unyama mkubwa wamefanya zaidi ya huyo Binti lakini kwakua binadam tumeumbiwa unafki watu wote watamlaumu kwa kujidai wao ni wema sana
Kuna unyama mkubwa zaidi ya kumchinja MAMA YAKO MZAZI na kumfukia kwenye nyumba hiyo hiyo mnayoishi ili Umiliki Mali alizozitafuta yeye mwenyewe?

Bro acha masikhara bhana,
Hebu taja unyama mwingine mkubwa zaidi ya huo tafadhali.
 
Eeh safi hii fundisho kwa wale wazazi wanaoendelea na ule msemo wa "hizi zangu katafute zako"
Kwani mulitafuta hizo mali pamoja na mzazi? Mzazi yuko sahihi kabisa, yeye ndiye aliyefanya kazi na kuteseka kwa hivyo hicho alichofanikiwa kukichuma ni chake.
 
Sasa atakataaje tena wakati mie ndio mtoto wake? Haoni kuwa hiyo ni rroho mbaya tuu? Yaani mtoto ateseke huko wakati mie ninauwezo wakumsaidia as long as haendi kufanya kitu kinyume na sheria za nchi....hapo sasa sioni faida ya kuwa mzazina mtoto nae hataona faida ya kuwa na mzazi mwenye uwezo kiuchumi.
Kweli kila mtu ana malezi yake, wengine yanawagharimu baadae na wengine hufaidika nayo
 
Mama mzazi kabisa kwa mikono na macho yako unamnyonga na unashuhudia akitapatapa kukata roho na unamfukia peke yako na unaendelea kuishi eneo Hilo Hilo!! Waume zenu je? Ndugu wa waume zenu? Watoto wa mumeo je,,,
Harafu mtu kama huyu ndo awe makamu wa rais kwa katiba ya tanzania? Siku 21 za bendera nusu mringoti inatuhusu

Sent from my TECNO K7 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom