Moses Machali: Askofu Kakobe siyo mchungaji wa kiroho

JINOME

JF-Expert Member
Joined
May 29, 2017
Posts
958
Reaction score
1,427
Anaandika
MOSES MACHALI

Ni Askofu gani Mtenda haki anayeweza kuwa mkosoaji wa upande mmoja tu? Ni Askofu gani aliyesimama kiimani anayeishi na kuhubiri kanisani huku akitengeneza vitu visivyokuwepo? Kwa mfano anasema Ipelekwe sheria Bungeni ikarekebishwe; Bungeni haipelekwi sheria kurekebishwa Bali mswada wa sheria ili kurekebisha sheria au kutunga sheria mpya.

Jambo la pili, Askofu Kakobe amekuwa mkosoaji wa serikali na CCM Kwa almost mara zote ktk mahubiri yake lakini huwa hakosoi Upinzani hata siku moja. JE, Askofu Kakobe haoni hata uovu wa viongozi wa CDM ulio wazi wenye wake wa ndoa lakini wanadharilisha wanawake wanaowapatia nafasi za Uongozi kama Ubunge wa viti maalumu kisha wanazaa nao? Au UKRISTU na uaskofu wa Kakobe unaona ni haki na sahihi viongozi wa CDM tena wakristu kutenda uovu huo? Je, huyu ni Askofu wa haki na mchungaji mwema anayefumbia macho uovu huo?

Askofu Kakobe, haoni wala kusikia kwamba Viongozi wa CDM wanawapotosha Watanzania ktk masuala mbalimbali? Mfano Kakobe anafumbia macho issue ya CDM kuuaminisha umma kwamba Lowasa ni Fisadi Kwa takribani Miaka Kumi lakini alivyojiunga CDM/Ukawa CDM wanasema Lowasa ni shujaa na mkombozi. Kimaadili Askofu Kakobe alipaswa kuwakemea Kwa kitendo hicho cha kuwahadaa Watanzania lakini kakaa kimya kama haoni kosa la ukosefu wa maadili miongoni wa viongozi wana CDM. Au naye Kakobe ndiyo wale CDM wanapotosha watu kwamba mtu ni Fisadi akiwa CCM lakini akishajiunga CDM ni msafi? kama jibu ni ndiyo basi Kakobe Hana sifa ya kuwa mchungaji mwema Bali mwanasiasa kanjanja wa CDM aliyejivika koti la Uaskofu.

Askofu Kakobe, anafahamu dhambi ya upotoshaji hadharani ya Kiongozi Mkuu wa CDM mbowe ya kuhadaa umma mwaka 2011 June Bungeni kwamba hataki matumizi ya magari ya kifahari aliyoyaita MASHANGINGI na kwamba ni ya gharama kubwa Sana na hivyo yeye mbowe kama Kiongozi wa Upinzani Bungeni alisema hatatumia gari la serikali la aina hiyo na aliahidi kulirejesha serikalini. Tujiulize leo Mbowe anatumia Shangingi alilolikataa au halitumii? Jibu analitumia wala hakulirejesha. JE, Askofu Kakobe haioni dhambi ya mbowe kuwahadaa watu Kwa sababu ya maslahi Binafsi ya kisiasa? Kwa nini Kakobe hakemei uovu huo wa CDM? Kakobe tangaza kwamba wewe ni Askofu mwenye maslahi Binafsi ndani ya Upinzani. Na Kwa mantiki hiyo unapoteza sifa ya kuwa Askofu au Mchungaji mwema.

Askofu Kakobe, Serikali kudhibiti siasa za hovyo kisheria miongoni mwa vyama vya siasa siyo dhambi hata kidogo. Na hivyo Rais Magufuli hapaswi kutubu ktk hilo lakini wewe Kakobe ndiyo unapaswa kutubu. Wala serikali hii haijazuia vyama vya upinzani pekee kufanya mikutano ya hadhara Bali hata CCM isipokuwa kwenye kampeni za Uchaguzi. Unaona hata sasa wapinzani wanaolilia mikutano ya hadhara wamekimbia kushiriki uchaguzi Mdogo wakati ilikuwa ndiyo fursa ya wao kueleza Watanzania masuala mbalimbali. Hawa wapinzania wamepinda. Hata hivyo wabunge na madiwani wameruhusiwa kufanya mikutano na hao ni wanasiasa. Serikali hii imepunguza utitiri wa mikutano ya vyama ambayo haina tija Kiuchumi na kijamii. Demokrasia ya vyama vingi siyo mikutano ya hadhara Tu. Askofu Kakobe kumbuka kwamba kila haki ina mipaka yake yaani limitations, Vyama vya siasa kuwa na Haki ya kufanya mikutano ya hadhara siyo kwamba haiwezekani kuwazuia pia iwapo kuna sababu za msingi. Wewe Kakobe na Watanzania wengine tunajua kwamba siasa za nchi yetu Kwa namna moja zimechangia kuchelewesha maendeleo Kwa sababu baadhi ya wanasiasa wanawapotosha Wananchi na hivyo serikali kama mlezi mkuu wa masuala yote ni sharti kuchukua hatua stahiki ikiwemo kudhibiti mikutano. Kwa mfano unamkana mwanasiasa anawaeleza watu kwamba Serikali Kutoa elimu bure ni jambo la hovyo. Kama vitendo vya namna hiyo vimeshamiri Kwa nini serikali isidhibiti vyama? Kakobe kuwa mkweli

Mwisho, Askofu Kakobe unasema kwamba Rais Magufuli aachee atukanwe Tu Kwa sababu haimpunguzii kitu na tena unaenda mbali Kwa kusema kwamba kikitokea kimwanafunzi cha UDOM kikamtukana yeye Magufuli anapungukiwa? Nimeshangaa Sana Askofu unatetea watu watukanwe na kisha wakae kimya!!! Wewe ukitukanwa utafurahi??? Mbona umeshindwa kukaa kimya ktk hilo la mikutano au vyama vingi tena ambalo hakikisha kama unavyokuwa; ukitukanwa so ndiyo utapata wazimu Baba Askofu??? . halafu unahubiri kuheshimu utawala wa sheria. Nadhani hapo busara imekutokaa na mahaba yako Kwa Ukawa yamekuzidi Baba Askofu. Badilika na ukatubu Kwa Mungu.

Askofu Kakobe tangazia umma kwamba wewe ni mpinzani kiitikadi na uache dhambi ya ubaguzi kupitia mahubiri yako kanisani. Wewe kama Askofu wa wote Hupaswi kuwabàgua Wana CCM ktk mahubiri yako. Ninaamini kwambà kanisani kwako Una waumini wa vyàma vyote. Acha ubaguzi tenda haki kama Askofu. la sivyo Acha kuhadaa watu uingie kwenye siasa ili tukutane Jukwaani.
 
Kwani Kakobe kasema jana ndio mwisho wake wa kuhubiri? Yaani unataka Kakobe amalize mambo yote tena mpaka mambo ya mapenzi kwa kutaja kiongozi mmoja mmoja kwa siku moja.
Rais Magufuli huenda hakuwahi kuagiza popote watu wajipendekeze ila kwa matukio ya kuteua wenye muelekeo wa kujipendekeza nakumsifia imesababisha kuwafanya vijana mazezeta.
Rais akisifiwa na viongozi wa dini basi wao hawafanyi siasa na wala sio CCM ila akikosolewa basi viongozi hao ni Ukawa, akili za aina hii zinapatikana CCM tu tena kwa watu wenye akili ndogo
 
Nimeshindwa kusoma habari yote, lakini kuna mambo mawili nitayagusia.
Moses Machali, awali ulikuwa Mbunge wangu.
Hivi unapoongelea viongozi wa Chademà na mambo ya ndoa zao wewe kwa ujana wako inakufaà nini? Ulikuwa Chadema ukaondoka kwenda NCCR Mageuzi nako ukaondoka kwenda ACT-Wazalendo, kwa hili tuu unaonyesha ulivyo debe tupu.
Mtu aliyeamini ktk itikadi, Sera na msingi mkuu wa chama hawezi kufanya upuuzi ulioufanya. Ulipokuwa Mbunge hakuna jambo la msingi kwa miaka 5 ulilofanya jimboni la kukufanya uonekane kuwa mwanasiasa. Leo umeshakatwa mkia, wewe ni mateka na sasa ni depe tupu.
Matendo yote yawezayo kuwa na negative impact kwenye jamii yetu huwezi tena kuyajua.
Jambo lingine ni kwamba ukosoaji kwa mamlaka huwa ni sehemu ya kuusaidia mfumo wa mamlaka hayo. Ni watu aina yako hawawezi kuelewa maana yake.
Wewe ungekuwa mtu wa busara na hekima ungeweza kulinda hadhi ya ubunge uliopata kama zawadi kutoka kwa wana Kasulu. Ni bahati mbaya kwamba kukatwa mkia huondoa uwezo wa mtu kutumia angalau sehemu ndogo ya uelewa anaokuwa nao.
 
Anaandika
MOSES MACHALI

Ni Askofu gani Mtenda haki anayeweza kuwa mkosoaji wa upande mmoja tu? Ni Askofu gani aliyesimama kiimani anayeishi na kuhubiri kanisani huku akitengeneza vitu visivyokuwepo? Kwa mfano anasema Ipelekwe sheria Bungeni ikarekebishwe; Bungeni haipelekwi sheria kurekebishwa Bali mswada wa sheria ili kurekebisha sheria au kutunga sheria mpya.

Jambo la pili, Askofu Kakobe amekuwa mkosoaji wa serikali na CCM Kwa almost mara zote ktk mahubiri yake lakini huwa hakosoi Upinzani hata siku moja. JE, Askofu Kakobe haoni hata uovu wa viongozi wa CDM ulio wazi wenye wake wa ndoa lakini wanadharilisha wanawake wanaowapatia nafasi za Uongozi kama Ubunge wa viti maalumu kisha wanazaa nao? Au UKRISTU na uaskofu wa Kakobe unaona ni haki na sahihi viongozi wa CDM tena wakristu kutenda uovu huo? Je, huyu ni Askofu wa haki na mchungaji mwema anayefumbia macho uovu huo?

Askofu Kakobe, haoni wala kusikia kwamba Viongozi wa CDM wanawapotosha Watanzania ktk masuala mbalimbali? Mfano Kakobe anafumbia macho issue ya CDM kuuaminisha umma kwamba Lowasa ni Fisadi Kwa takribani Miaka Kumi lakini alivyojiunga CDM/Ukawa CDM wanasema Lowasa ni shujaa na mkombozi. Kimaadili Askofu Kakobe alipaswa kuwakemea Kwa kitendo hicho cha kuwahadaa Watanzania lakini kakaa kimya kama haoni kosa la ukosefu wa maadili miongoni wa viongozi wana CDM. Au naye Kakobe ndiyo wale CDM wanapotosha watu kwamba mtu ni Fisadi akiwa CCM lakini akishajiunga CDM ni msafi? kama jibu ni ndiyo basi Kakobe Hana sifa ya kuwa mchungaji mwema Bali mwanasiasa kanjanja wa CDM aliyejivika koti la Uaskofu.

Askofu Kakobe, anafahamu dhambi ya upotoshaji hadharani ya Kiongozi Mkuu wa CDM mbowe ya kuhadaa umma mwaka 2011 June Bungeni kwamba hataki matumizi ya magari ya kifahari aliyoyaita MASHANGINGI na kwamba ni ya gharama kubwa Sana na hivyo yeye mbowe kama Kiongozi wa Upinzani Bungeni alisema hatatumia gari la serikali la aina hiyo na aliahidi kulirejesha serikalini. Tujiulize leo Mbowe anatumia Shangingi alilolikataa au halitumii? Jibu analitumia wala hakulirejesha. JE, Askofu Kakobe haioni dhambi ya mbowe kuwahadaa watu Kwa sababu ya maslahi Binafsi ya kisiasa? Kwa nini Kakobe hakemei uovu huo wa CDM? Kakobe tangaza kwamba wewe ni Askofu mwenye maslahi Binafsi ndani ya Upinzani. Na Kwa mantiki hiyo unapoteza sifa ya kuwa Askofu au Mchungaji mwema.

Askofu Kakobe, Serikali kudhibiti siasa za hovyo kisheria miongoni mwa vyama vya siasa siyo dhambi hata kidogo. Na hivyo Rais Magufuli hapaswi kutubu ktk hilo lakini wewe Kakobe ndiyo unapaswa kutubu. Wala serikali hii haijazuia vyama vya upinzani pekee kufanya mikutano ya hadhara Bali hata CCM isipokuwa kwenye kampeni za Uchaguzi. Unaona hata sasa wapinzani wanaolilia mikutano ya hadhara wamekimbia kushiriki uchaguzi Mdogo wakati ilikuwa ndiyo fursa ya wao kueleza Watanzania masuala mbalimbali. Hawa wapinzania wamepinda. Hata hivyo wabunge na madiwani wameruhusiwa kufanya mikutano na hao ni wanasiasa. Serikali hii imepunguza utitiri wa mikutano ya vyama ambayo haina tija Kiuchumi na kijamii. Demokrasia ya vyama vingi siyo mikutano ya hadhara Tu. Askofu Kakobe kumbuka kwamba kila haki ina mipaka yake yaani limitations, Vyama vya siasa kuwa na Haki ya kufanya mikutano ya hadhara siyo kwamba haiwezekani kuwazuia pia iwapo kuna sababu za msingi. Wewe Kakobe na Watanzania wengine tunajua kwamba siasa za nchi yetu Kwa namna moja zimechangia kuchelewesha maendeleo Kwa sababu baadhi ya wanasiasa wanawapotosha Wananchi na hivyo serikali kama mlezi mkuu wa masuala yote ni sharti kuchukua hatua stahiki ikiwemo kudhibiti mikutano. Kwa mfano unamkana mwanasiasa anawaeleza watu kwamba Serikali Kutoa elimu bure ni jambo la hovyo. Kama vitendo vya namna hiyo vimeshamiri Kwa nini serikali isidhibiti vyama? Kakobe kuwa mkweli

Mwisho, Askofu Kakobe unasema kwamba Rais Magufuli aachee atukanwe Tu Kwa sababu haimpunguzii kitu na tena unaenda mbali Kwa kusema kwamba kikitokea kimwanafunzi cha UDOM kikamtukana yeye Magufuli anapungukiwa? Nimeshangaa Sana Askofu unatetea watu watukanwe na kisha wakae kimya!!! Wewe ukitukanwa utafurahi??? Mbona umeshindwa kukaa kimya ktk hilo la mikutano au vyama vingi tena ambalo hakikisha kama unavyokuwa; ukitukanwa so ndiyo utapata wazimu Baba Askofu??? . halafu unahubiri kuheshimu utawala wa sheria. Nadhani hapo busara imekutokaa na mahaba yako Kwa Ukawa yamekuzidi Baba Askofu. Badilika na ukatubu Kwa Mungu.

Askofu Kakobe tangazia umma kwamba wewe ni mpinzani kiitikadi na uache dhambi ya ubaguzi kupitia mahubiri yako kanisani. Wewe kama Askofu wa wote Hupaswi kuwabàgua Wana CCM ktk mahubiri yako. Ninaamini kwambà kanisani kwako Una waumini wa vyàma vyote. Acha ubaguzi tenda haki kama Askofu. la sivyo Acha kuhadaa watu uingie kwenye siasa ili tukutane Jukwaani.
Huyu chizi kwani kakobe kaisema ccm au siasa zinazoendelea nchini ,faida na hasara zako yake maoni tu
 
Back
Top Bottom