Morogoro: Wanaokwamisha ujenzi wa stendi ya Mikumi kuondolewa

Morogoro: Wanaokwamisha ujenzi wa stendi ya Mikumi kuondolewa

Bawabu wa pili

Senior Member
Joined
Nov 14, 2025
Posts
147
Reaction score
432
📍MOROGORO - Mkuu wa Mkoa, Adam Malima, amesema hatua zitachukuliwa dhidi ya Watumishi wote wanaokwamisha utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa stendi ya magari ya mizigo (malori) ya Mikumi, Wilayani Kilosa, unaotarajiwa kuanza hivi karibuni.

Malima ametoa kauli hiyo wakati wa kikao kazi cha tathmini ya utendaji kazi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilosa, kilichofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa FDC, Kilosa.



Amesema kuwa Wilaya ya Kilosa inaingiza mapato makubwa yanayopaswa kuakisiwa katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo, hata hivyo kumekuwapo na kusuasua katika ukamilishaji wa baadhi ya miradi, ikiwemo ujenzi wa stendi ya Mikumi, hivyo kuwataka viongozi wa Halmashauri hiyo kuongeza ufanisi katika usimamizi wa miradi ili ikamilike kwa wakati na kuongeza mapato ya Halmashauri.

Aidha, Malima amesema Kituo cha Treni ya Kisasa (SGR) cha Kilosa kimejengwa kimkakati tofauti na vituo vingine, kwa lengo la kukuza utalii na kurahisisha usafirishaji wa mazao. Kutokana na hilo, amewataka viongozi wa halmashauri kuhakikisha wanatumia fursa hiyo kikamilifu kwa kuweka mikakati madhubuti ya kukuza utalii pamoja na usafirishaji wa mazao ya mbogamboga kupitia reli ya mwendo kasi.

Kwa upande wake, Katibu Tawala wa Mkoa wa Morogoro, Dkt. Mussa Ali Mussa, amewataka viongozi wa Halmashauri kuhakikisha wanatekeleza kikamilifu maagizo yote wanayopewa na viongozi wa Mkoa, kwa lengo la kukaa na kutatua changamoto za Wananchi. Amesema hatua hiyo ni sehemu ya kujali utu wa Mtanzania.

Aidha, amewahimiza kuwa na mikakati katika kilimo cha mazao ya kimkakati na kutumia vyanzo vya mapato kwa ubunifu ili kuongeza mapato ya Halmashauri.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Kilosa, Shaka Hamdu Shaka, amesema Halmashauri hiyo imetenga jumla ya ekari 48,000 kwa ajili ya shughuli za kilimo na ufugaji.

Ameongeza kuwa katika kuhakikisha reli ya mwendo kasi inanufaisha Wananchi wote bila kuleta matabaka, Halmashauri inaendelea kusimamia uanzishwaji wa chumba cha kuhifadhia mazao (cold storage room) ili kuhifadhi mazao yatakayokuwa yanasafirishwa kupitia SGR.
 
Back
Top Bottom