Morogoro: Shida ya maji ya kutumia majumbani

Morogoro: Shida ya maji ya kutumia majumbani

Mji umezungukwa na milima lakini wananchi wana shida ya maji hatari.

Kuna habari niliona kuwa kipindipindu nacho kinashika kasi morogoro.
Morogoro ndio haswaa chimbuko na nyumbani kwa magonjwa ya kuhara na matumbo nazungumzia Typhoid,Amoeba na kuendesha kwa namana zake ukienda morogoro kunywa maji ya chupa tu kwa usalama wa afya yako
 
Wakati mwingine jamani tusijiabishe kwa kauli zetu na kujifanya great thinker, hivi inawezekana kijiji kizima kisilipe bili ya maji. Mimi ni mkazi wa moja ya eneo alilotaja mleta uzi, tumeshafuatilia sehemu husika lakini hali bado ni tete.
Pole kwa yanayowasibu. Wahusika wamesha pata taarifa.
 
Kuna kaujenzi ka barabara kanaendelea kutoka njia panda kuelekea kisaki, ndo angalau ma 'excavator 'yanavyotindua yanapasua mipira ya MORUWASA raia wanapata maji
Na mipira ya MORUWASA ikitinduliwa huko ilikokuwa inapeleka maji wanakosa maji.
 
Morogoro ndio haswaa chimbuko na nyumbani kwa magonjwa ya kuhara na matumbo nazungumzia Typhoid,Amoeba na kuendesha kwa namana zake ukienda morogoro kunywa maji ya chupa tu kwa usalama wa afya yako
Kuna mwanafunzi mmoja wa MUM alikuwa anaishi mafiga aliniambia kuwa kuna siku maji ya bomba yalitoka yana vitu kama kinyesi..
Inasikitisha.
 
Kuna mwanafunzi mmoja wa MUM alikuwa anaishi mafiga aliniambia kuwa kuna siku maji ya bomba yalitoka yana vitu kama kinyesi..
Inasikitisha.
Ni uchafu huo,kuna muda mpaka yanafanya kunuka.Ni kawaida sana,mindu inatoa tope.na si maji tena.
 
Mkuu sio hayo maeneo tu,nilikua Moro kwa shughuli za kimaisha kuanzia mwezi wa 6 mpaka wa 11,nilikua nikizungukia mitaa ya Falk land, Kididimo, Misufuni na Vibandani na huko kote kulikua na shida kali ya maji kwa kipindi hicho chote na shida ilikua kali zaidia sept-Nov.
Na cha kushangaza zaidi hata barabara za falk land na kididimo ni mashimo matupu kama vile sio Moro town.

Nikawa najiuliza kama hapo ndio mjini na kuna shida ya maji na barabara je huko vijijini hali ikoje?

Ila nasikia madiwani wa Moro twn wote ni wa chama chakavu[emoji23][emoji23][emoji23]

Poleni sana wapogoro, 2020 msirudie makosa.
eti chama chakavu...

Hata maeneo ya wilayani ambapo "chama machachari" kimeshika hatamu napo hoi. Hakuna penye afadhali.
 
Kigurunyembe tunachota chua ualimu morogoro na maji yako bweleleeeeeeee
 
Back
Top Bottom