Morogoro: Shida ya maji ya kutumia majumbani

Morogoro: Shida ya maji ya kutumia majumbani

nyembeason

Member
Joined
May 4, 2009
Posts
44
Reaction score
21
Wadau,

Tuna miezi kama minne hivi, baadhi ya mitaa ya mji wa MOROGORO, Bigwa, kolahili, kigurunyembe, etc, tukiwa hatuna maji ya kutumia majumbani.

Mwokozi pekee ni vijimito vilivyokauka vinavyotoka mlimani. Milima yenyewe imejengwa majumba-uoto na vyanzo vya maji vimevamiwa.

Tunachimba chini, kama wanavijiji wengine wa Tanzania. Tunasubiria vimeee, tunachota kwa zamu (angalia picha).

Wenye uwezo, ndoo moja yauzwa TZS 500, na magari ya maji ya kuuza wanataka ununue kuanzia lita 2000!

Kazi hapa tu...
 

Attachments

  • NTANDU12 - WIN_20161212_085030.JPG
    NTANDU12 - WIN_20161212_085030.JPG
    306.6 KB · Views: 93
  • NTANDU12 - WIN_20161212_084541.JPG
    NTANDU12 - WIN_20161212_084541.JPG
    273.3 KB · Views: 90
  • NTANDU12 - WIN_20161212_084743.JPG
    NTANDU12 - WIN_20161212_084743.JPG
    387.5 KB · Views: 67
Poleni sana wakati watu wa moshi tuna maji mpaka tunamwagia barabarani mpaka bomba zinapasuka

dawa ni kuchagua chadema chagua maji chagua maendeleo nyie na kijani yetu mbele nyinyi nyuma. next time chagua maendeleo usichague umaskini.


lakini cha ajabu 2020 mtakuwa kwa kijani badala ya kuwa kwa khaki
 
Wadau,
Tuna miezi kama minne hivi, baadhi ya mitaa ya mji wa MOROGORO, Bigwa, kolahili, kigurunyembe, etc, tukiwa hatuna maji ya kutumia majumbani.

Mwokozi pekee ni vijimito vilivyokauka vinavyotoka mlimani. Milima yenyewe imejengwa majumba-uoto na vyanzo vya maji vimevamiwa. Tunachimba chini, kama wanavijiji wengine wa Tanzania. Tunasubiria vimeee, tunachota kwa zamu (angalia picha). Wenye uwezo, ndoo moja yauzwa TZS 500, na magari ya maji ya kuuza wanataka ununue kuanzia lita 2000!
Kazi hapa tu...
Tunamuomba mhe rais atembelee mkoa wa moro idara ya maji inastahili kutumbuliwa
 
Tunamuomba mhe rais atembelee mkoa wa moro idara ya maji inastahili kutumbuliwa
Morogoro kwa kweli inapaswa imfukuze mkurugenzi wake. Ni wavivu, wazembe, wezi, hawajitumi. Moro maji ni tatizo kubwa sana tena sana
 
Mji umezungukwa na milima lakini wananchi wana shida ya maji hatari.

Kuna habari niliona kuwa kipindipindu nacho kinashika kasi morogoro.
 
Mmewasiliana na mamlaka husika. Yaana idara ya maji. Uongozi wa halmashauri. Uongozi wa Wilaya na Mkoa? Wamesemaje?

Kwa nini ni mitaa yenu tu ndipo pawe na ukosefu wa maji huko yanakopatikana kuna nini?

Isijekuwa nyie ni wale wasiolipa bili za maji
 
Poleni sana wakati watu wa moshi tuna maji mpaka tunamwagia barabarani mpaka bomba zinapasuka

dawa ni kuchagua chadema chagua maji chagua maendeleo nyie na kijani yetu mbele nyinyi nyuma. next time chagua maendeleo usichague umaskini.


lakini cha ajabu 2020 mtakuwa kwa kijani badala ya kuwa kwa khaki
Usipotoshe. Hayo maji yapo kabla ya kuanzishwa kwa CHADEMA.
 
Alafu rais amenunua ndege wakati watu wake hawana maji!!

Lakini nyie si ndio mlichagua ccm kwa kishindo??? Sasa isomeni namba
 
Wenzenu wanapewa bodaboda(chdma) nyie hamna maji yaani uhai(ccm)....halafu hamjiongezi.??..Poleni sana
 
Inasikitisha kuona mji kama morogoro hauna maji wakati umezungukwa na milima ya kila aina. Wenzetu wanachimba mabwawa juu ya vilima (mfano Norway) kwa hiyo inakuwa rahisi kuvuna maji ya mvua ambayo hutumiwa wakati hakuna mvua. Sisi sijui tumerogwa na nani?

Juhudi kubwa zinapelekwa kwenye mambo ya hovyo kama kuhangaika na wapinzani badala ya kujenga miundo mbinu ya wananchi
 
Pole sana,ila hamko peke yenu.NCCR hapo hapo Morogoro dumu moja la maji linauzwa 1,000!

Jamani mimi labda ni taahira,sijui.Lakini nadhani sio taahira ila kuna tatizo kubwa kwa viongozi wetu.Mara nyingi nimesikia viongozi wetu wakisema asilimia themanini (80%) ya Watanzania wana maji safi na salama.TAKWIMU HIZI zina walakini mkubwa. jamani, yaani out of ten nane wana maji safi na salama?I don't think so.

Katika eneo ninaloishi very few people have reliable water,let alone safe water.Kwa bahati nzuri nimetembea sehemu nyingi za Tanzania,hali ndio hiyo hiyo kila mahali, tena in most areas the situation is worse.Kwa hiyo hili la kwenu haliji kama surprise.

Maji ni muhimu kuliko kitu kingine chochote , kwa hiyo ni vema serikali ikatoa kipaumbele katika tatizo hili.Tukumbuke kwamba maji safi yanachangia pia katika kuboresha afya za watu.Kama tutafanikiwa kuwapa watu wetu maji safi na salama tutapunguza kwa kiwango kikubwa sana magonjwa yanayoambukizwa kwa kutumia maji yasiyo salama kama Typhoid,Dysentry nk.
Wadau,

Tuna miezi kama minne hivi, baadhi ya mitaa ya mji wa MOROGORO, Bigwa, kolahili, kigurunyembe, etc, tukiwa hatuna maji ya kutumia majumbani.

Mwokozi pekee ni vijimito vilivyokauka vinavyotoka mlimani. Milima yenyewe imejengwa majumba-uoto na vyanzo vya maji vimevamiwa.

Tunachimba chini, kama wanavijiji wengine wa Tanzania. Tunasubiria vimeee, tunachota kwa zamu (angalia picha).

Wenye uwezo, ndoo moja yauzwa TZS 500, na magari ya maji ya kuuza wanataka ununue kuanzia lita 2000!

Kazi hapa tu...
 
Mmewasiliana na mamlaka husika. Yaana idara ya maji. Uongozi wa halmashauri. Uongozi wa Wilaya na Mkoa? Wamesemaje?

Kwa nini ni mitaa yenu tu ndipo pawe na ukosefu wa maji huko yanakopatikana kuna nini?

Isijekuwa nyie ni wale wasiolipa bili za maji
Wakati mwingine jamani tusijiabishe kwa kauli zetu na kujifanya great thinker, hivi inawezekana kijiji kizima kisilipe bili ya maji. Mimi ni mkazi wa moja ya eneo alilotaja mleta uzi, tumeshafuatilia sehemu husika lakini hali bado ni tete.
 
Mkuu sio hayo maeneo tu,nilikua Moro kwa shughuli za kimaisha kuanzia mwezi wa 6 mpaka wa 11,nilikua nikizungukia mitaa ya Falk land, Kididimo, Misufuni na Vibandani na huko kote kulikua na shida kali ya maji kwa kipindi hicho chote na shida ilikua kali zaidia sept-Nov.
Na cha kushangaza zaidi hata barabara za falk land na kididimo ni mashimo matupu kama vile sio Moro town.

Nikawa najiuliza kama hapo ndio mjini na kuna shida ya maji na barabara je huko vijijini hali ikoje?

Ila nasikia madiwani wa Moro twn wote ni wa chama chakavu[emoji23][emoji23][emoji23]

Poleni sana wapogoro, 2020 msirudie makosa.
 
Sasa kama mmejenga vinyumba kwenye vyanzo vya maji nani alaumiwe?
 
Kuna kaujenzi ka barabara kanaendelea kutoka njia panda kuelekea kisaki, ndo angalau ma 'excavator 'yanavyotindua yanapasua mipira ya MORUWASA raia wanapata maji
 
Back
Top Bottom