Morogoro: Mkoa Wenye Fursa ya Kuilisha Tanzania na Afrika

ChoiceVariable

JF-Expert Member
May 23, 2017
43,076
49,784
Morogoro Mkoa ambao unatajwa kuwa ni ghala la chakula ambalo halijatumika vizuri Kwa sababu una fursa ya kulisha Tanzania na Afrika kiujumla.

Inasemekana ni Moja ya Mikoa yenye vyanzo vingi vya maji na Ardhi yenye rutuba inayofaa kustawisha mazao aina mbalimbali kuanzia mpunga Hadi miwa.

Mkoa huu ambao uko katika ya Majiji Makuu ya Dar na Dodoma unaweza kuwafanya watu matajiri endapo wataamua kutumia fursa hiyo vizuri.

View: https://www.instagram.com/p/C4gDe1VINCg/?igsh=MTVhN2VvcnExcWJyZQ==

My Take
Serikalini itenge Mikoa kadhaa ambayo italima mazao tofauti tofauti.

Mfano zao la Ngano-Mikoa ya Njombe,Mbeya,Manyara,Rukwa na Arusha.

Mpunga-Morogoro,Mbeya,Katavi,Shinyanga,Geita nk

Mahindi-Ruvuma,Rukwa,Mbeya,Songwe,Njombe,Dodoma,Kigoma na Manyara.

Utajiri upo kwenye Kilimo chenye Tija.
 
Back
Top Bottom