Morocco yaadhimisha miaka 26 ya siku ya Mfalme. Waziri Kombo amempongeza Mfalme Mohamed VI

Morocco yaadhimisha miaka 26 ya siku ya Mfalme. Waziri Kombo amempongeza Mfalme Mohamed VI

Ojuolegbha

JF-Expert Member
Joined
Sep 6, 2020
Posts
1,770
Reaction score
1,173
MOROCCO YAADHIMISHA MIAKA 26 YA SIKU YA MFALME

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mahmoud Thabit Kombo amempongeza Mfalme Mohamed VI wa Morocco, Serikali na Watu wa nchi hiyo kwa kuadhimisha miaka 26 ya Siku ya Mfalme, kwa kueleza kuwa miaka 26 ya Ufalme imekuwa ya maendeleo, ustahamilivu na kufanya mabadiliko.

Balozi Kombo ametoa kauli hiyo wakati anahutubia wageni waalikwa katika hafla ya kusherehekea Siku ya Mfalme iliyofanyika jijini Dar Es Salaam Julai 30, 2025.

Waziri Kombo amebainisha kuwa miaka 26 ya Ufalme, Morocco imefanya mabadiliko makubwa katika nyanja ya siasa, uchumi na huduma za jamii kiasi kwamba, Taifa hilo limekuwa kigezo chema cha mabadiliko, demokrasia na maendeleo jumuishi yaliyotokana na uwekezaji wa kimkakati na ubunifu, na kulifanya taifa hilo kuwa lango la Afrika.

Morocco ikiwa inaadhimisha Siku ya Mfalme, Waziri Kombo alisema uhusiano baina ya Tanzania na nchi hiyo ulioanza kabla ya ukoloni umekuwa imara na kuimarika zaidi kufuatia ziara ya Kitaifa ya Mfalme Mohamed VI aliyoifanya nchini mwaka 2016 ambayo imeshuhudiwa uwekaji saini wa Hati za Makubaliano 22 katika nyanja za biashara, uwekezaji, kilimo, utalii, usafirishaji, afya, elimu, utamaduni, michezo, ulinzi na usalama.

Waziri Kombo amewakumbusha jumuiya ya wanadiplomasia kuhusu sera ya mambo ya nje ambayo Tanzania imeizindua hivi karibuni na kubainisha dhamira ya Tanzania kushirikiana na wadau wote duniani kwa kuimarisha ushirikiano wa kimkakati na kupigania maslahi ya Tanzania kupitia diplomasia.

"Kupitia Sera hii, Tanzania imedhamiria kuimarisha ushirikiano na mataifa marafiki kama Morocco, Taifa ambalo kwa pamoja tunashirikiana katika kuhamasisha amani, mshikamano na ustawi wa pande zote mbili", Waziri Kombo alisema.

Alihitimisha hotuba yake kwa kuiomba Morocco kushirikiana na Tanzania katika kuhamasisha matumizi ya lugha na
utamaduni wa Kuswahili nchini Morocco, lugha ambayo ni ya kazi katika Umoja wa Afrika na sio tu ni daraja kwenye mtangamano wa Kikanda lakini pia ni chombo cha kuunganisha utamaduni wa kiafrika.
 

Attachments

  • publer-1753963255249.jpg
    publer-1753963255249.jpg
    57.5 KB · Views: 15
  • publer-1753963253691.jpg
    publer-1753963253691.jpg
    84.3 KB · Views: 16
  • publer-1753963256278.jpg
    publer-1753963256278.jpg
    74 KB · Views: 18
  • publer-1753963258116.jpg
    publer-1753963258116.jpg
    48.4 KB · Views: 17
  • publer-1753963261668.jpg
    publer-1753963261668.jpg
    38.7 KB · Views: 15
  • publer-1753963277353.jpg
    publer-1753963277353.jpg
    58.9 KB · Views: 18
  • publer-1753963264627.jpg
    publer-1753963264627.jpg
    86.9 KB · Views: 18
Back
Top Bottom