Morocco kufuta sera ya elimu bure inayotolewa na Tanzania

FikraPevu

JF-Expert Member
Jan 2, 2010
303
236
Wakati serikali ya Tanzania ikitekeleza sera ya elimu bure kwa shule za msingi na sekondari, serikali ya Morocco inakusudia kupeleka mswada wa sheria bungeni ili kufikia tamati ya kutoa elimu bure kwa wanafunzi nchini humo.

Kutokana na uamuzi huo wa serikali ya Morocco ambayo inaongozwa na Mfalme Mohammed VI imeibua hasira za wanafunzi, wasomi na wadau wa elimu nchini humo ambapo wabunge wa chama tawala na wale wa upinzani wameungana kuupinga mswada huo ambao unalenga kuongeza gharama za elimu nchini humo.

Mswada huo utaifanya elimu ya msingi kuendelea kuwa bure kwa Wamorocco wote lakini ada itakuwa inalipwa kwa wanafunzi wa sekondari na elimu ya juu ambao wanatoka kwenye familia tajiri. Wanaopinga mswada huo wameonya kuwa sheria hiyo ikipita itaathiri ubora wa elimu na mfumo mzima jamii.

Zaidi, soma hapa => Elimu bure ya Tanzania yatoa changamoto nchini Morocco | FikraPevu
 
Back
Top Bottom