Moro vs Iringa

Moro vs Iringa

Vitalis Msungwite

JF-Expert Member
Joined
May 11, 2014
Posts
3,311
Reaction score
7,955
Kwa mliotembea au kukaa kwenye hizi manispaa tupeane uzoefu. Binafsi nilipita morogoro wakati naenda Dar, nilipaona hapako vizuri sana ukilinganisha na Iringa.

Mnaopafahamu hapo moro, ni sehemu gani nzuri ya kuifunika Iringa kuanzia, miundo mbinu ya barabara, mpangilio wa makazi, majengo makubwa na mazuri n.k.

Naona Iringa ipo mbali sana sijui kwa wengine mnalionaje hilo.
 
Kwa mliotembea au kukaa kwenye hizi manispaa tupeane uzoefu. Biafsi nilipita morogoro wakati naenda Dar, nilipaona pakichoko sana ukilinganisha na Iringa.

Mnaopafahamu hapo moro, ni sehemu gani nzuri ya kuifunika Iringa kuanzia, miundo mbinu ya barabara, mpangilio wa makazi, majengo makubwa na mazuri n.k.

Naona Iringa ipo mbali sana sijui kwa wengine mnalionaje hilo.
Ni mikoa miwili inayosifika kwa chakula kingi. Mingine sijui bhuaana
 
Moro kupo fresh Sana,sema Kwa vile huwa unapita.siku jalbu kukaa ata wk hv utembeee ujionee.
 
Moro ipo vzr, basi halipiti mjini... linaishia msamvu tu
 
Moro pako poa sana, inaonekana uliishia msamvu tu hukupita kule town
 
Ulipoandika pakichoko sana ndipo ulipoharibu uzi wako
Ila Usijaribu kuifananisha Moro na vitu vya kijinga Kama uliwahi kusikia "mji kasoro bahari "utaelewa maana yake
 
32. MWANA ASO MTEMBEZI
Kwa jina Mwanzamkwao, ulo mwingi wa mbawazi,
Mgawa haki kigao, ni barika ya Azizi,
Ukwapi hata utao, ziumane beti hizi,
Mwana aso mtembezi hachi kusifia kwao.

Hachi kusifia kwao, mwana aso mtembezi,
Maneno kila uchao, mamaye ndiyo mjuzi,
Humsifu kwa matao, aupikavyo mchuzi,
Mwana aso mtembezi hachi kusifia kwao.

Hachi kusifia kwao, yamemziba maozi,
Hatoki nyumbani mwao, thama kangiwa ubozi
Angauza wapitao, apate masimulizi,
Mwana aso mtembezi hachi kusifia kwao.

Hachi kusifia kwao, yamemlevya malezi,
Amepigwa mzumbao, mengine hajamaizi,
Walisema mtu kwao, sikuacha utembezi,
Mwana aso mtembezi hachi kusifia kwao.

Hachi kusifia kwao, ja vile msimaozi,
Aliyeona mng'ao, unapo andama mwezi,
Haumwishi mshangao, kwenye yake maongezi,
Mwana aso mtembezi hachi kusifia kwao.

Hachi kusifia kwao, nafanya ukomelezi,
Ni mvuli niwambao, mfungue masikizi,
Msambe ino ni mwao, nafanya uelekezi,
Mwana aso mtembezi hachi kusifia kwao.
MKANYAJI
HAMISI A.S KISSAMVU
kutoka (Baitu shi'ri)
MABIBO * DSM.()
 
hata miaka 300 ijayo Iringa haiwezi kuikaribia Morogoro....Iringa ni sawa tu na Kilosa ambayo ni wilaya katika mkoa maarufu wa Morogoro
 
Dahh... Sasa mbona umeitukana Moro.. Imekukosea nini!!!
 
JokaJeusi ni miongoni mwa Vijana waliotembea hapa na pale katika taifa hili.

Huwezi ifananisha Moro na Iringa. Moro ni zaidi ya Iringa kwa mambo mengi sana.

1. Moro ina idadi kubwa ya watu kuzidi Iringa. Hapa tunazungumzia Morogoro manisipaaa na Iringa Manisipaa.

2. Moro inamakazi mengi kuliko Iringa.
3. Moro inaunganisha Majiji mawili Ambayo ni Dsm na Dodoma.
4. Moro mpaka jioni kuna magari ya kwenda mikoani Wakati Iringa ikifika saa saba mchana unaweza kosa mabasi ya kwenda Dsm labda upande malori.
5. Moro ni Mji wenye hali ya hewa ya kati yaani Moderate inayoruhusu mtu yoyote kuishi. Wakati Iringa kuna baridi kali hasa maeneo ya Mafinga.
6 Moro mji mzuri kijiografia kutokana na eneo kubwa kuwa tambarare Kuanzia eneo la Bwawani unapotokea Dsm Mpaka mikumi unapoelekea Iringa. Wakati Iringa eneo kubwa ni vilima ambavyo si rafiki kwa baadhi ya watu.
7. Moro ni mji wa watu angalau wenye Exposure kuliko Iringa. Huwezi fananisha mtu aliyetoka Moro kwa ujanja na yule aliyetoka Iringa.
 
Kwa mliotembea au kukaa kwenye hizi manispaa tupeane uzoefu. Biafsi nilipita morogoro wakati naenda Dar, nilipaona pakichoko sana ukilinganisha na Iringa.

Mnaopafahamu hapo moro, ni sehemu gani nzuri ya kuifunika Iringa kuanzia, miundo mbinu ya barabara, mpangilio wa makazi, majengo makubwa na mazuri n.k.

Naona Iringa ipo mbali sana sijui kwa wengine mnalionaje hilo.
Punguza ukali wa maneno mkuu,Heshima ni kitu cha bure.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom