Moja ya sifa kubwa za mwanamke bora ni kuweza kutunza siri

Jtee

Senior Member
Dec 27, 2022
186
297
1. Kuwa na kifua kipana cha kutunza SIRI za mambo yanayomuhusu na yasiyomuhusu.

Wanawake tunakumbushana,
Wanawake wengi wamezoea kuongea, hadi wanaona ni kawaida kuongea mambo yote wanayowahusu kwenye umati wa wanawake wenzao hata yale ya SIRI.

Ukiwa Public speaker kujihusu kwenye vigenge vya umbea, hutopewa tuzo ya uongeaji bora ila unashusha HESHIMA yako na utaharibu nyumba yako yote.

Siku hizi Mahusiano, ndoa nyingi zinaharibika sababu ya kukosa SIRI. Ni ngumu kupambana na kitu usichokijua
Na ni vyepesi kuharibu kitu unachokijua.

Wapenzi kinachowalinda watu ni SIRI..
Ndo maana nchi zina siri, na hauwezi kuivamia nchi usipojua siri zake. Na apo ndo maana kuna Wapelelezi.

Mwanamke kuwa na kituo kwenye maneno yako, kuongea sana ni kumpa adui silaha ya kukuweza. Mafanikio na kushindwa kwako yamejificha kwenye uwezo wa kutumia kinywa chako.

Taarifa zako sio mali ya umma, sio kila unachofanya kila mtu aone au ajue.

Vya thamani utunzwa Sirini na utakuwa mpumbavu ukiviachia nje.

Madam Tee nilitaka tukumbushane tu.

Nawapenda.
 
Kunywa Mojito glass mbili bili kwangu......
Akujie na hiii
IMG_2155.jpeg
 
Back
Top Bottom