MOI yawaaga wajumbe wa Menejimenti waliohamishwa

MOI yawaaga wajumbe wa Menejimenti waliohamishwa

Taasisi ya Mifupa-MOI

Senior Member
Joined
Apr 15, 2025
Posts
118
Reaction score
211
Watumishi wanne waliokuwa wajumbe wa Menejimenti ya Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Ubongo Muhimbili (MOI) wameagwa rasmi baada ya kupangiwa majukumu na Serikali katika taasisi nyingine za Umma.

Watumishi hao ni Dkt. Veronica Nyahende aliyekuwa Mkurugenzi wa Fedha na Mipango, Dkt. Paul Kazungu aliyekuwa Meneja Udhibiti Ubora, Florah Masami aliyekuwa Meneja Ukaguzi wa Ndani na Amiri Mkapanda aliyekuwa Meneja Utawala.

Hafla hiyo fupi imefanyika leo Ijumaa Mei 23, 2025 katika Ukumbi wa MOI Phase III ambapo viongozi hao walitunukiwa vyeti na tuzo ikiwa ni ishara ya kutambua mchango wao katika Taasisi ya MOI.

Akizungumza wakati wa hafla hiyo, Mkurugenzi Mtendaji wa MOI, Mhe. Balozi Dkt. Mpoki Ulisubisya amewapongeza wajumbe hao kwa kazi nzuri waliyoifanya kwa ufanisi mkubwa katika kipindi cha utumishi wao MOI.

"Kwanza niwapongeze kwa kazi nzuri mliyoifanya mkiwa katika taasisi hii, kiukweli mmefanya kazi kwa bidii na ufanisi mkubwa, tumeambiwa kwamba matokeo chanya ya sasa ni pamoja na mchango wenu wa kiutumishi... Asanteni sana" amesema Dkt. Mpoki

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimaliwatu wa MOI, Bw. Orest Mushi amewasihi wajumbe hao kuendelea kushirikiana na watumishi wa taasisi hiyo kwa mambo mbalimbali ya kiutumishi hata kijamii, kwani walifanya kazi kwa umoja na ushirikiano.

Kwa upande wake, Bi. Florah Masami aliyekuwa Meneja Ukaguzi wa Ndani wa MOI, ameushukuru uongozi wa taasisi hiyo kwa kuandaa hafla hiyo ya kutambua mchango wao kwa kuwapa vyeti na tuzo.

IMG-20250523-WA0094.jpg
IMG-20250523-WA0109.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom