Watanzania siasa zinatudanganya. Hivi kwa mawazo yako, kama kuna ajali imetokea hospitalini, daktari na mgonjwa asiye daktari, unadhani jitihada za uokozi zitaelekezwa wapi? Jeshini wakati wa vita tunasema ni aheri kupoteza askari 1000 kuliko kumpoteza brigade commander mmoja, na ni aheri kupoteza raia 100 kuliko kupoteza askari mmoja. Hapa thamani ya binadamu inapimwa katika uwezo wa kupigana na kupiganisha. Na katika tiba, thamani ya ubinadamu hupimwa katika uwezo wa uokoaji wa maisha. Katika uhalisia, ni aheri kupoteza wagonjwa 100 kuliko daktari mmoja. Kuokoa maisha ya daktari mmoja ni kuokoa maisha ya raia wengine zaidi ya 1000, lakini kuokoa maisha ya mgonjwa mmoja ni kuokoa maisha ya mtu mmoja.