PreGE2025 Mohammed Kawaida: Walionyimwa Haki ya Kugombea Msiogope, Karibuni CCM

PreGE2025 Mohammed Kawaida: Walionyimwa Haki ya Kugombea Msiogope, Karibuni CCM

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

Mkalukungone Mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
2,437
Reaction score
5,235
Kutokana na uwepo wa taarifa za Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kutoshiriki uchaguzi mkuu wa 2025 kulikosababishwa na kukataa kusaini kanuni za maadili ya uchaguzi, Mwenyekiti wa UVCCM Mohammed Ali Kawaida, amesema amepokea malalamiko mengi kutoka kwa vijana juu ya kunyimwa haki yao ya msingi ya kuchaguliwa

Kawaida amezungumza hayo wakati akizungumza na mamia ya vijana wa halmashauri ya mji wa Njombe ambapo amesema vijana wameumizwa na kitendo hicho lakini wapo tayari kushiriki uchaguzi kwa kupiga kura kwa viongozi watakaopeleka maendeleo kwenye maeneo yao.

Kupata matukio na taarifa zote kwa kila mkoa kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025 ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

"Wameniambia kunyimwa kitendo cha kupiga kura au kuambiwa wasiende kupiga kura huko ni kunyimwa haki yao ya msingi, sasa mimi niwatie shime kwa kuwa vyama vyao vimewanyima haki yao ya msingi kugombea sisi tunawakaribisha katika chama chetu" amesema Kawaida

 
Anavo wakaribisha watapewa nafas ya kugombea??
Au ni unafiki tuu
Yeye mwenyewe anatamani huo ubunge
 
Back
Top Bottom