Mohammed Hussein athibitisha kuondoka Simba

Mohammed Hussein athibitisha kuondoka Simba

Kama anaenda Yanga ,msimu ujao Yanga italua moto sana aisee inaweza fika Nusu au fainali Ya CAF
Hao ni wachezaji bado haijawa timu. Ili iwe timu lazima apatikane mwalimu mzuri wa kuwafanya wachezaji waweze kuelewana, kuwa na mbinu bora za kimchezo na la mwisho lazima waingie mapema pre season kwaajili ya maandalizi ya msimu.
 
Yanga timu tayari wanayo ila hapo wanafanya maboresho kwa muda mrefu sasa nchi yetu haijawahi pata beki bora wa kushoto kuliko Mo Hussein.

Bahati mbaya kila msimu timu yetu inaanza upya ona msimu huu ambao tunaambiwa kikosi kizuri tayari tushaacha wachezaji muhimu tena kikosi cha kwanza
 
Baada ya kutumikia Simba SC kwa takribani miaka 11, nahodha wa klabu hiyo Mohamed Hussein ameagana rasmi na Wekundu wa Msimbazi kufuatia mkataba wake kumalizika na kutoongezwa tena.

View attachment 3411217
Mohamed Hussein, maarufu kama "Zimbwe Jr", ameacha alama kubwa ndani ya kikosi hicho akichangia mafanikio lukuki ikiwemo ubingwa wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara, Mataji ya Kombe la FA na safari mbalimbali za kimataifa kwenye michuano ya CAF.

View attachment 3411216

Tetesi zinaeleza kuwa Mohamed Hussein huenda akatua Yanga SC baada ya kuondoka Simba, huku akihusishwa na ofa ya kuvutia iliyowekwa mezani na mabingwa hao wa kihistoria.

Kwa mujibu wa vyanzo vya kuaminika, Yanga SC inadaiwa kumpa Mkataba wa Miaka Miwili wenye masharti yafuatayo:
  • Pesa ya usajili: Shilingi milioni 300
  • Mshahara: TSh. Milioni 25 kwa Mwezi
  • Gari: Harrier Anaconda mpya
  • Tiketi za ndege: Vacation ya kifahari Dubai
Kanji alishindwa kumpatia haya?
 
Kwa milioni 900 acha tu aende, kuziacha hizo ni upuuzi
 
Tundu Antipas lissu pekee NDO atanitetemesha ikitokea akahama nchi wengine KILA la KHERI Hilo liko JUU ya uwezo wangu,🙏🙏🙏🙏🙏🙏
 
Baada ya kutumikia Simba SC kwa takribani miaka 11, nahodha wa klabu hiyo Mohamed Hussein ameagana rasmi na Wekundu wa Msimbazi kufuatia mkataba wake kumalizika na kutoongezwa tena.

View attachment 3411217
Mohamed Hussein, maarufu kama "Zimbwe Jr", ameacha alama kubwa ndani ya kikosi hicho akichangia mafanikio lukuki ikiwemo ubingwa wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara, Mataji ya Kombe la FA na safari mbalimbali za kimataifa kwenye michuano ya CAF.

View attachment 3411216

Tetesi zinaeleza kuwa Mohamed Hussein huenda akatua Yanga SC baada ya kuondoka Simba, huku akihusishwa na ofa ya kuvutia iliyowekwa mezani na mabingwa hao wa kihistoria.

Kwa mujibu wa vyanzo vya kuaminika, Yanga SC inadaiwa kumpa Mkataba wa Miaka Miwili wenye masharti yafuatayo:
  • Pesa ya usajili: Shilingi milioni 300
  • Mshahara: TSh. Milioni 25 kwa Mwezi
  • Gari: Harrier Anaconda mpya
  • Tiketi za ndege: Vacation ya kifahari Dubai
Mimi hata huwa siamini kama wachezaji wetu wamefikia stage ya kulipwa mishahara hiyo kuliko hata wabunge..

Hizo zinaweza kuwa ni mere speculation tu.
Mishahara ya wachezaji wa za timu za Tanzania huwa ni siri ya uongozi.
Na ukiona siri ujue na magumashi yapo.

Mswahili anavyopenda kuongeza sifuri mbele...alipe hivyo halaf msijue kweli.
 
Kwa milioni 900 acha tu aende, kuziacha hizo ni upuuzi
Hizo stori za jaba Yanga au timu yoyote ndani ya Tanzania hakuna atakayetoa 900M kwa Mo Hussein hasa na umri wake huo.
 
Wamemuachia valentine nouma na sasa huyu tena?
 
Back
Top Bottom