Orketeemi
JF-Expert Member
- Feb 12, 2013
- 5,514
- 14,173
Baada ya kutumikia Simba SC kwa takribani miaka 11, nahodha wa klabu hiyo Mohamed Hussein ameagana rasmi na Wekundu wa Msimbazi kufuatia mkataba wake kumalizika na kutoongezwa tena.
Mohamed Hussein, maarufu kama "Zimbwe Jr", ameacha alama kubwa ndani ya kikosi hicho akichangia mafanikio lukuki ikiwemo ubingwa wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara, Mataji ya Kombe la FA na safari mbalimbali za kimataifa kwenye michuano ya CAF.
Tetesi zinaeleza kuwa Mohamed Hussein huenda akatua Yanga SC baada ya kuondoka Simba, huku akihusishwa na ofa ya kuvutia iliyowekwa mezani na mabingwa hao wa kihistoria.
Kwa mujibu wa vyanzo vya kuaminika, Yanga SC inadaiwa kumpa Mkataba wa Miaka Miwili wenye masharti yafuatayo:
===
Farewell to the PRIDE (Group of Lions)
Takribani miaka 11 ya Furaha, huzuni, Shangwe, vifijo, nderemo na masikitiko ndani ya Mbuga.
Kwa uaminifu mkubwa, weledi wa kiwango cha juu, Kuvuja jasho kuipigania nembo ya klabu ndio ulikuwa msingi na malengo.
Wahenga walisema kila lenye mwanzo halikosi mwisho na leo nawaaga rasmi.
Haya ni maamuzi yaliyolenga Maendeleo yangu binafsi, maslahi yangu binafsi na weledi wangu uliotukuka.
Nichukue fursa hii kuwashukuru viongozi, benchi la ufundi na operation staffs wote wa klabu ya Simba SC kwa kipindi chote cha kuhudumu ndani ya klabu.
Kipekee niwashukuru mashabiki kwa kuwa nami kipindi chote, kama mnavyonipenda na mimi nawapenda pia na nina imani mtaendelea kuniumga mkono.
Naishukuru Management Yangu ikiongozwa na Carlos Carlos kwa ushirikiano mkubwa wa kipindi chote.
Former Captain,
MOHAMED HUSSEIN

- Pesa ya usajili: Shilingi milioni 300
- Mshahara: TSh. Milioni 25 kwa Mwezi
- Gari: Harrier Anaconda mpya
- Tiketi za ndege: Vacation ya kifahari Dubai