Mohammed Entreprises vs BOT vs Foreign... kisa? Dili la BILIONI 180 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mohammed Entreprises vs BOT vs Foreign... kisa? Dili la BILIONI 180

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by the circus, Jul 11, 2012.

 1. t

  the circus Member

  #1
  Jul 11, 2012
  Joined: Oct 24, 2011
  Messages: 71
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Na Jabir Idrissa; MwanaHalisi

  [​IMG]


  UBALOZI wa Libya jijini Dar es Salaam umekana mahusiano yoyote na kampuni ya Mohammed Enterprises (MeTL) na mshirika wao Massoud Mohamed Nassr.

  Hatua hii inaziba mwanya wa kampuni hiyo kujipatia sehemu ya dola 121.9 milioni (sawa na kiasi cha Sh. 180 bilioni) ambazo inadaiwa ni deni la Tanzania kwa Libya linalotokana na mkopo wa mafuta.

  Fedha hizo zilitarajiwa kuchotwa kwa mtindo wa EPA wa kununua madeni yaliyoshindikana kutoka benki Kuu ya Tanzania (BoT).

  Tayari ubalozi umeiarifu serikali kuhusu suala hilo na nakala ya barua yake kupelekwa mahakama kuu ambako mashauri mawili yamefunguliwa na MeTL.

  Taarifa kutoka ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali jijini Dar es Salaam zimeeleza kuwa hata ofisi hiyo tayari imetaarifiwa kuhusu suala hilo.

  Nyaraka ambazo MwanaHALISI limepata zinaonyesha kuwa mfanyabiashara maarufu wa chakula nchini, Gulamabbas Hassanali Fazal Dewji anataka kujipatia mabilioni ya shilingi kutokana na kile kilichoitwa kuuziana madeni sugu kati ya serikali za Tanzania na Libya.

  Vyanzo madhubuti vya habari vimelieleza gazeti hili kuwa serikali imezuia malipo ya mabilioni ya shilingi ambazo mfanyabiashara huyo amekuwa akijitahidi kuyadai kupitia kesi mbili alizofungua katika Mahakama Kuu ya Tanzania.

  Dewji ambaye ni mkurugenzi wa kampuni ya Mohammed Enterprises (T) Limited (MeTL), anadai zaidi ya dola 20 milioni kupitia kesi Na. 127 ya 2009 na kesi Na. 110 ya 2010.

  Wakati kesi Na. 127 ambayo MeTL ilimshitaki raia wa Libya aitwaye Massoud Mohamed Nassr au Masoud M. Nasser, iliamuliwa 26 Mei 2011, kesi Na. 110 haijasikilizwa.

  Katika uamuzi wa kesi ya awali inayodaiwa kuhusu mkataba wa kuuziana deni, Jaji Augustine Mwarija aliamuru pande husika zigawane mapato pamoja na riba yaliyotokana na uuzaji wa dhamana za serikali zinazoshikiliwa na Benki Kuu ya Tanzania (BoT).

  Mapato hayo yanafikia Sh. 6,640,550,960 ambapo uamuzi wa Jaji Mwarija unaelekeza kuwa MeTL itaingiziwa kwenye akaunti yake Sh. 3,320,275,480.

  Lakini, kulingana na nyaraka zilizopatikana, hata mapato hayo si halali na serikali imezuia malipo.

  Serikali ya Libya, ambayo MeTL imeishitaki kama mdaiwa wa kwanza katika kesi Na. 110, imekataa kutambua mpango wa kuuziana deni la dola 121,900,000 ambalo linadaiwa kutokana na Tanzania kushindwa kulipa mkopo tangu mwaka 1983.

  Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe ameiambia MwanaHALISI kwamba wizara yake haitambui makubaliano ya MeTL na Nasser na haioni uhalali wa madai yao.

  Membe ambaye alizungumza na gazeti hili ofisini kwake Dar es Salaam juzi Jumatatu, alisema wizara yake tayari imemjulisha Mwanasheria Mkuu wa Serikali kuwa serikali ya kigeni haiwezi kushitakiwa na Mtanzania kwa mikataba ambayo haikuidhinishwa.

  “Serikali ya nje haiwezi kushitakiwa bila ya kuwa na nyaraka za serikali zilizosainiwa na watu wenye kutambuliwa katika mikataba. Huyu hajalipa fedha na hana mkataba… (kama ni) deni lazima linunuliwe na serikali na kuna masharti ya kulipa,” alisema.

  Akigusia maelezo yaliyotolewa na ubalozi wa Libya nchini, waziri Membe alisema ni maelezo sahihi na kwamba msimamo wa serikali ni kutokuwepo sababu yoyote wala uhalali wa kuishitaki serikali ya Libya katika suala hilo.

  Alisema Mlibya anayedaiwa kufunga mikataba ya kuuziana deni na MeTL linalohusu mafuta ambayo serikali ya Libya iliiuzia Tanzania, hakuwa na hata sasa hana mamlaka ya kuiwakilisha serikali ya Libya katika jambo lolote na “hakuwa na mkataba wowote kati ya serikali ya Libya na MeTL.”

  MeTL imeishitaki Libya kama mdaiwa wa kwanza katika kesi Na. 110. Ubalozi wa Libya unasema hautambui mpango wa kuuziana deni la dola 121,900,000 uliobuniwa na MeTL kutokana na Tanzania kushindwa kulipa deni lake linalotokana na Libya kuiuzia serikali ya Tanzania mafuta kwa mkopo.

  Ubalozi wa Jamhuri ya Kisoshalisti ya Watu wa Libya jijini Dar es Salaam, imeeleza kwamba haitambui makubaliano ya aina yoyote kati ya serikali ya Libya na MeTL au anayejiita mwakilishi wa serikali ya Libya.

  Akijibu takwa la kuitwa shaurini mahakama kuu, ofisa wa ubalozi wa Libya anaeleza waziri wa mambo ya nchi za nje Tanzania kuwa serikali yake haijawahi kuipeleka Tanzania mahakamani.

  Katika hati yake ya maelezo yenye Kumb. N/REF 7/2/2250 ya tarehe 20 Mei 2011, ambayo nakala yake ilipepekwa mahakamani, ubalozi wa Libya unasema, katika mahusiano yake ya nje ya nchi – yawe ya kisiasa au kiuchumi – huwa inashughulika na serikali wala si mtu au taasisi binafsi hasa suala lenyewe linapohusu deni kwa biashara ya mafuta.

  “Libya, katika suala hili (la kuuza mafuta), inazingatia muktadha wa udugu na Tanzania, unaotokana na uhusiano mzuri wa kisiasa tulionao. Tunaamini Libya haistahili kushitakiwa na kampuni hii kutokana na suala hili,” inasema hati hiyo.

  Serikali ya Libya, unaeleza ubalozi wake, haijapata kusaini au kuidhinisha mkataba wowote wa kibiashara na kampuni inayodai katika kesi tajwa.

  Inasema, “Ni muhimu ukafahamu kuwa mamlaka inayostahili kuiwakilisha serikali ya Libya katika Tanzania ni ubalozi wa Libya na si yeyote mwingine; iwe kwa kusaini mikataba au kuiidhinisha pale inapotokea…”

  “Ubalozi wa Libya unaiomba mahakama tukufu kutoendekeza madai haya dhidi ya Libya. Tuna matumaini makubwa ya busara na hekima kutumika katika kutenda haki kuhusu kesi hii,” ameeleza wakala wa serikali ya Libya.

  Maelezo ya serikali ya Libya yaliwasilishwa kwa Msajili wa Mahakama Kuu ya Tanzania kwa barua ya wizara ya mambo ya nje tarehe 30 Mei 2011 yenye Kumb. Na. GA 226/336/78 iliyosainiwa na Abdallah M. Mtibora kwa niaba ya katibu mkuu wa wizara hiyo.
   
 2. P

  Precise Pangolin JF-Expert Member

  #2
  Jul 11, 2012
  Joined: Jan 4, 2012
  Messages: 12,196
  Likes Received: 1,977
  Trophy Points: 280
  Hawa wahindi wameshaona hapa ni sehemu Yao ya kuvunia Mihela wanatakiwa wagukuzwe
   
 3. N

  Njoka Ereguu JF-Expert Member

  #3
  Jul 11, 2012
  Joined: Apr 7, 2012
  Messages: 822
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 35
  Huyu anajitapa kujenga mashule kule singida na kucheza ngoma za kinyiramba kumbe ni mchafu anataka kuleta EPA nyingine wakati hata ile ya kwanza hatujasahau.

  Ana bahati hapo ni Tanzania ingekuwa nchi nyingine ambazo maslahi ya nchi yako mbele ungefanywa mpango wa kufuatilia hata hizo alizo nazo sasa na kumfilisi tu. Wahindi wanakaa kuangalia mianya ya kunyonya tu ili warudi kwao matajiri wakati sisi tunakufa njaa hapa na wanafanya hivyo bila ya huruma yoyote. Huyo mwanasheria naye aliyesimamia hiyo kesi anahitaji kuchunguzwa maana alifanya maamuzi kwa shinikizo la fedha.
   
 4. Mzee wa Rula

  Mzee wa Rula JF-Expert Member

  #4
  Jul 11, 2012
  Joined: Oct 6, 2010
  Messages: 8,177
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  Hii ni mwanahalisi ya lini? Stori hii niliisoma muda mrefu kabla hata Gadafi hajafa.

  Kajamaa kajizi kweli lakini naamini hakapo peke yake.
   
 5. KOMBAJR

  KOMBAJR JF-Expert Member

  #5
  Jul 11, 2012
  Joined: Nov 15, 2011
  Messages: 5,848
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Gullam Mjanja sasa huyo mzee na ili kuweza kuweka mambo yake sawa ameishika hii serikali kila kona,kwanza kitendo cha mwane Mo kuwa bungeni siyo accidental ni mkakati wa kibiashara na kuna mawaziri na wakurugenzi wengi katika idara mbali mbali wapo kwenye payrol yake kila friday wanaenda kukinga mshiko hiyo ili mambo yake yaeendee vizuri.

  Haitoshi ni mcheza rafu mzuri sana kwenye nyanja ya biashara. Its high time sasa watanzani wakawaelewa watu hawa.
   
 6. D

  Dabudee Senior Member

  #6
  Jul 11, 2012
  Joined: May 30, 2012
  Messages: 156
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  "Mwalimu usinibaini wajinga ndio waliwao; nikipata mbili moja yako, moja Yangu"
   
 7. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #7
  Jul 11, 2012
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,316
  Likes Received: 1,784
  Trophy Points: 280
  Kama anataka kutengeneza kashfa nyingine, what measure is taken to prevent it? Hivi Tanzania hatuna uwezo wa kufanya biashara bila kujihusisha na wizi?
   
 8. Kakulwa P

  Kakulwa P JF-Expert Member

  #8
  Jul 11, 2012
  Joined: Feb 8, 2012
  Messages: 200
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mpango wa kambi ya CCM 2015 kama ilivyokuwa KAGODA. Wahindi ni jamii hatari sana kwa utapeli. Hapo huwezi kusikia jeshi la Polisi kuingilia maana wakuu wanahusika kikamilifu.
   
 9. C

  CHUAKACHARA JF-Expert Member

  #9
  Jul 11, 2012
  Joined: Jun 3, 2011
  Messages: 12,200
  Likes Received: 3,810
  Trophy Points: 280
  Amini aliwafukuza mkalaumu, alikuwa kichaa, kumbe aliona mbali. Wahindi sio wenzetu, waondoke na kuna siku wataondoka tu! Kama sisi hatuwezi kuwa na biashara, ardhi india vipi wao ? Najua wapo hapa kwa historia, lakini historia sasa inakwenda mwisho, wataondoka!
   
 10. m

  majebere JF-Expert Member

  #10
  Jul 11, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 4,520
  Likes Received: 567
  Trophy Points: 280
  Je wakiondoka nani atawalisha CDM, hebu kamuulize Mzee Slaa kama anakubaki mfadhili wao afukuzwe.
   
 11. M

  Maga JF-Expert Member

  #11
  Jul 11, 2012
  Joined: Nov 11, 2010
  Messages: 325
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 35
  Hivi nchi hii imelogwa na nani? Hawa wahindi wanatuendesha wanavyotaka, wanyama wetu maporini wanatuibia tumekaa kimya, sasa hadi vihela vyetu navyo wanatuibia tunawaangalia tu!!!!!

  Watanzania inabidi tujenge katabia kaa kuwa na utaifa ndani ya mioyo yetu. Wenzetu wa Kenya huwezi kufanya ujinga kama huu mtu akakuangalia tu.

  Lakini hapa kwetu mtu anapewa vimilioni viwili vitatu anaona kaapata kinoma anaachia mabilioni yanaondoka huu ni ushenzi uliopitiliza. CCM na watu wake woote washenzi kabisa, 2015 they have to go
   
 12. m

  majebere JF-Expert Member

  #12
  Jul 11, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 4,520
  Likes Received: 567
  Trophy Points: 280
  Hebu jaribu kuchunguza matajiri wakubwa Kenya ni kina nani.Kenya inaendeshwa na wahindi kama ulikua hujui.
   
 13. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #13
  Jul 11, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,869
  Likes Received: 6,220
  Trophy Points: 280
  aaaah mbona wamembania? shamba la bibi hili kila mwenye meno anakula..... au hakuna mgao?
   
 14. lukindo

  lukindo JF-Expert Member

  #14
  Jul 11, 2012
  Joined: Mar 20, 2010
  Messages: 7,887
  Likes Received: 6,072
  Trophy Points: 280
  Tanzania nakupenda kwa moyo wangu wote ...eti (nakukumbusha) huyu sio mhindi bali ni mwana-ccm na mbunge!
   
 15. N

  Ndinani JF-Expert Member

  #15
  Jul 11, 2012
  Joined: Aug 29, 2010
  Messages: 5,413
  Likes Received: 734
  Trophy Points: 280
  Hizi hela zitatolewa tu na gavana wa BOT Ndullu na kuwapa ccm karibu na uchaguzi wa 2015!! Watch my words!!
   
 16. C

  CHUAKACHARA JF-Expert Member

  #16
  Jul 11, 2012
  Joined: Jun 3, 2011
  Messages: 12,200
  Likes Received: 3,810
  Trophy Points: 280
  CDM is moving from private dependency to peoples dependency-peoples power will finance CDM
   
 17. B

  Blessing JF-Expert Member

  #17
  Jul 11, 2012
  Joined: Apr 21, 2009
  Messages: 271
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0

  Aisee na kweli hiyo ni NORMAR wana JF. Hawa Wahindi ni watu WABAYA sana mimi naturally siwapendi kabisa. Ila DAWA ya hawa MAHINDI WAFISADI ni kuwachoma tuu kabisa. Never make that mistake kuwarudisha kwao kwa sababu because wanarudi tena kwa jina lingine na passport lingine AISEE hawa WAHINDI jamani achana nao kabisa. Mtu uko Tanzania ana Passport ya INDIA, PAKISTAN, LONDON, CANADA, USA na TANZANIA. Sijui Uhamiaji wanafanya lini kuhusu issue hii ya wahindi nchini. AISE WE SHOULD NEVER LEAVE ANY STONE UNTURNED.

   
 18. B

  Blessing JF-Expert Member

  #18
  Jul 11, 2012
  Joined: Apr 21, 2009
  Messages: 271
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0

  This people called INDIANS are not worth staying among us actually what IDDI AMIN did in UGANDA was the right thing for this INDIANS. In actual fact, Iddi Amin sent them out but we have to burn them alive. I HATE THEM and would not like to see them at any cost at all in TAnzania. Acha hata kama hawa MAFISADI wanataka kuwatetea pia tunawachoma nao pia ndani to live Tanznaia a Country free of Corruption.
   
 19. s

  slufay JF-Expert Member

  #19
  Jul 11, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 1,372
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Shamba la bibi wajukuu wanajichotea" bibi mwenyewe amezungukwa na maprofesa wa fani zote i.e lawyers,accountant, economist, nk lakini ka vile hawajui wanachofanya ( sijui tuweke darasa la saba)
   
 20. m

  majebere JF-Expert Member

  #20
  Jul 11, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 4,520
  Likes Received: 567
  Trophy Points: 280
  Uliona nini kilimkuta Idi amini baada ya kufukuza wahindi, halafu umesahau kuwa ni sie ndio tulitumwa kumtoa? Wanajeshi wetu walikufa kwaajili ya wahindi. Hiyo ndio power ya wadosi mkuu.
   
Loading...