Mohamed Said: BAKWATA Kibaraka (kipindi maalum)

Mohamed Said: BAKWATA Kibaraka (kipindi maalum)

Kibanga Ampiga Mkoloni

JF-Expert Member
Joined
Aug 9, 2007
Posts
19,114
Reaction score
9,280
BAKWATA KIBARAKA KIPINDI MAALUM KILICHORUSHWA NA RADIO KHERI, RADIO QUIBLATAIN NA RADIO IMAAN 1 OKTOBA 2012

Mpenzi msomaji kipindi kilirushwa mubashar (live) na Radio Kheri (Dar es Salaam), Radio Quiblatain (Iringa) na Radio Imaan (Morogoro) tarehe 1 Oktoba 2012.

Chanzo cha mwandishi kufanya kipindi hiki maalum kuhusu BAKWATA ni kutokana na propaganda zilizokuwa zikipepewa na viongozi wa BAKWATA wenyewe na vyombo vya habari kuwa Waislam walikuwa wanataka kuipindua BAKWATA na kumteka Sheikh Mkuu wa BAKWATA.

Propaganda hii ilikuwa ikiongozwa na sheikh mmoja kutoka ofisi za BAKWATA Mkoa wa Dar es Salaam.

Mwandishi baada ya kushinikizwa sana na Waislam aliridhia kufanya kipindi hiki maalum ili ukweli kuhusu ukibaraka wa BAKWATA ufahahamike kwa wananchi wote.


 
Huyu Mohammed Said ni mfano wa mpiga domo asiyechoka.
Lakini hafanyi chochote cha maana kusaidia uislamu na waislamu.

Sijui kachangia au kuhamasisha ujenzi wa hospitali au shule ngapi.
Binafsi kasomesha watoto wangapi wa kiislamu.

Aache hizo.
 
Ilikuwa zama zile wakimchezea JK sio hizi.
 
Hahaha dah walahi haya Makaburi ,Sheikh wa mkoa wa Makonda sasa hivi atakuwa anaukumbuka msemo wa Jk mwanaharamu hata ukimuweka kwenye chupa atatoa hata kidole ...
 
nasubiri BAKWATA wamjibu na huyu!
Wajahidina watu wa ajabu imani hiyo ilipoingia nchini walianza mapinduzi ya kupora uongozi na misikiti ya bakwata kwa nguvu.Bakwata wakashtaki serikalini kuwa tunavamiwa serikali ikawaambia wajahidina wasajili baraza lao na wajenge misikiti yao sababu imani walizo nazo tofauti na za bakwata.Kwa mbwembwe wakaanzisha baraza lao lakini hadi Leo limebuma halina waislamu wengi lakini pamoja na kupewa Uhuru kuanzisha dhehebu lao kutwa unakuta wanaongelea bakwata wakati hawako chini ya bakwata si waendelee na mambo ya kufuga ndevu na kuvaa visuruali vifupi na yeboyebo miguuni?
 
Huyu Mohammed Said ni mfano wa mpiga domo asiyechoka.
Lakini hafanyi chochote cha maana kusaidia uislamu na waislamu.

Sijui kachangia au kuhamasisha ujenzi wa hospitali au shule ngapi.
Binafsi kasomesha watoto wangapi wa kiislamu.

Aache hizo.

Anatetea udini tu huyu babu hajambo kwa udini
 
Wajahidina watu wa ajabu imani hiyo ilipoingia nchini walianza mapinduzi ya kupora uongozi na misikiti ya bakwata kwa nguvu.Bakwata wakashtaki serikalini kuwa tunavamiwa serikali ikawaambia wajahidina wasajili baraza lao na wajenge misikiti yao sababu imani walizo nazo tofauti na za bakwata.Kwa mbwembwe wakaanzisha baraza lao lakini hadi Leo limebuma halina waislamu wengi lakini pamoja na kupewa Uhuru kuanzisha dhehebu lao kutwa unakuta wanaongelea bakwata wakati hawako chini ya bakwata si waendelee na mambo ya kufuga ndevu na kuvaa visuruali vifupi na yeboyebo miguuni?
usipende kuzungumzia vitu usivovijua kwa kinywa kipana
 
Back
Top Bottom