SOFTWARE Mobile Phones and Computers Services (MOCOS)

mocoservices

Member
Feb 24, 2023
45
144
MOCO Services ni Wabobezi wa kurekebisha vifaa vya mawasiliano SIMU na Kompyuta. Tupo Mkoani Mbeya, Mwanjelwa, Barabara ya Juakali.

Tumejikita katika ufundi wa "hardware pamoja na software". Ofisi yetu inatumia vifaa vya na teknolojia ya kisasa ili kukidhi mahitaji na matarajio ya wateja wetu.

MOCOS Tunafanyaje kazi?
Kwa kuzingatia umuhimu wa muda wa wateja wetu na shughuli zao, MOCOS inatumia njia maalumu ya kuwasikiliza wateja wake popote walipo. Kwa wateja walio mbali, na vifaa vyao vina shida ya hardware MOCOS itawasaidia kuwaunganisha na mafundi wenye weledi karibu na maeneno yako. Pia, kama mteja yupo tayari kutuma kifaa chake ili kifanyiwe kazi ofisini kwetu, tuna mkaribisha kwa mikono miwili, anuani yetu nitaambatanisha kwenye andiko hili. Kwenye hardware tunatumia spare parts orijino kabisa ili kuhakikisha simu yako inarudi katika ubora wake wa awali. Tuna vioo orijino, mifumo ya caji na orijino, spika n.k

Kwa upande wa "SOFTWARE" teknolojia imetusaidia sana kufanya kazi za wateja wetu popote walipo bila kuja ofisini kwetu isipokuwa kwa matatizo machache tu ambayo yanahitaji operesheni maalumu au uunganishaji maalumu na kompyuta. Matatizo mengi ya "software" tunaweza kuyatatua papo hapo ulipo bila kupiga hata hatua moja ya mguu wako.

Ili kufanikisha kukusaidia hapo ulipo uwe na vitu vifuatavyo:
  1. Computer (tunapendekeza windows pc)
  2. internet yenye kasi walau 750kbps
  3. USB cable inayoendana na simu yake
  4. Simu yenye hitirafu ya software
  5. Uelewa wa kutumia kompyuta kidogo.
  6. Uwezo wa kufuata maelekezo ya namna ya kuunganisha simu na kompyuta katika njia ambayo inaruhusu kufanyiwa kazi.
  7. Kama simu yako ni iPhone ukiwa na MacBook/iMac pia sawa.
Ni Matatizo gani ya Software tunatatua hapo ulipo?
  1. Network unlocking kwa simu karibia zote
  2. Password, PIN, Passcode, Pattern reset kwenye android
  3. Kutoa lock screen bila kufata vitu (kwa simu zinazowezekana, uliza kwetu)
  4. kutoa lock ya account ya Google (frp), Huawei ID, Oppo ID n.k
  5. Kutoa Samsung Account
  6. Kutoa Blackberry ID
  7. Kubypass iCloud ID kwa iPhone zinazowezekana (5s-X)
  8. Kuflash simu zinazoshindwa kuwaka hdi mwisho, zenye virus n.kTop
Hizo ni baadhi ya huduma za kisoftwre ambazo tunaweza kukusaidia hapo ulipo.

Namna ya kuwasiliana nasi
Namba ya Simu: 0767 379 327
website: https://www.mocos.repair/contactus

ILANI: MOCOS haifanyi kazi kwenye simu zilizoibiwa au kupotea, ndugu mteja kabla ya kuja kwetu kutaka huduma (baadhi ya huduma hapo juu) utatakiwa kuthibitisha uhalali wa umiliki wa simu husika.

Aidha MOCOS inakukumbusha kutunza simu yako vyema ili kuepuka gharama zisizo za lazima.

Ahsante na Karibu sana.

Screenshot_20230302-163541_Gmail.jpg
20230302_173400.jpg
Screenshot_20230302-174057_One_UI_Home[1].jpg
6C776F8F-DE86-4638-98EC-5244A664D047.jpeg
10ca439b-b2f3-44d7-a6f7-f94de945ab95.jpg
130cb1d3-5cb1-46a1-b5a0-39c6da462cee.jpg
camphoto_684387517.jpg
camphoto_1804928587(1).jpg
camphoto_1804928587.jpg
e68361ea-7d7f-4606-a18d-7cd5bf1502f9.jpg
 
After Thought 1.
Ili kupata urahisi wa mawasiliano kati yako na sisi, MOCOS tumetengeneza mfumo ambao utasaidia sana kuokoa muda wako.
Watu wengi wana haribikiwa na vitu vyao na wanapata shida na usumbufu kwa kutokujua ni wapi watapata fundi mzuri na gharama za spare parts pamoja na matengenezo.

Kwa kutumia website yetu Wasiliana Nasi Hapa utaweza kuzungumza nasi moja kwa moja hivyo kuokoa muda wako adhimu na gharama ambazo ungeweza kupoteza kuzunguka kumtafuta fundi.

Muda ni mali, naomba share na ndugu, jamaa na marafiki kuhusu njia hii rafiki na rahisi ya kuwasiliana na fundi atakaye kusaidia kukutatulia changamoto za kiufundi kwenye kifaa chako cha umeme, kama vile simu, computer, Tv au Music system.
Hapa chini ni muonekano wa fomu amabyo unatakiwa kuijaza, nasi tutapata ujumbe wako na ndani ya muda mfupi tutawasiliana nawe na kukushauri cha kufanya au hata kukupa ufumbuzi wa suala lako la kiufundi.

1677784113647.png
 
Simu za software zikiwazingua mnicheki wakuu
G977U Verizon locked, utanifanyia shilingi ngapi? na Security chip damaged ya Mate 20 pro utanifanyia shilingi ngapi?
 

Attachments

  • 6C776F8F-DE86-4638-98EC-5244A664D047.jpeg
    6C776F8F-DE86-4638-98EC-5244A664D047.jpeg
    140.5 KB · Views: 14
Google Pixel 3a
Locked Verizon
Android Version 11

Successful Unlocked
Sasa inaweza tumia mitandao yote.

Kama una shida kama hiyo usisite kuwasiliana nasi

WhatsApp 0767379327
IMG20230304164533~2.jpg
IMG20230304165013.jpg
 

Attachments

  • IMG20230304164533.jpg
    IMG20230304164533.jpg
    47.7 KB · Views: 14
Maji Maji Maji Jinsi Yanavyo Sababisha Simu/Computer Kufa au Kuharibika.

Maji ni uhai, kila mtu anajua hilo. Na maji yamekuwa kimiminika muhimu sana kwenye maisha yetu, tunayanywa, tunayaoga, tunapozea mitambo n.k

Maji hayohayo yakienda kusiko yanaleta uharibifu mkubwa. Anyway mimi ni fundi simu, computer, Tv na Music System kwa hiyo nisiwachoshe na stori ndefu.

LEO TUZUNGUMZIE MAJI KWENYE SIMU.
Kwa uzoefu wangu wa muda mrefu kwenye ufundi wa vifaa tajwa, maji yanaongoza kuua au kuleta uharibifu kwenye sakiti za vitu hivyo.
Wote tunajua kuwa maji ni kipitisha kizuri cha umeme, pia maji yakiungana na chuma na hewa yanazaa kitu kinaitwa Ferric Oxide (kutu) kwa hiyo;

1. Maji yanapitisha umeme
2. Maji+Chuma(Fe)+Oxygen (O2)=Ferric Oxide (2Fe2O3.XH2O(s) (kutu)

Vitu hivyo viwili vinaharibu simu, maji yatapigisha shot sakiti (short circuit) kwa sababu yanapitisha umeme na kuunga njia za umeme ambazo hazipaswi kuungana.

Ferric Oxide (kutu) itasababisha vitu vyenye uchuma (Fe) kulika.

Ushauri Wangu Simu Ikiingia Maji.
1. Zima simu mara moja, kama battery la kutoka toa battery. Hii itasaidia kupunguza flow ya umeme kwenye njia ambazo sio.
2. Kwa maji yanayoonekana nje, futa kwa kitambaa safi.
3. Peleka simu yako kwa fundi mzuri aliye jirani nawe, kama humjui wasiliana nasi, tutakuunganisha naye ili aikaushe maji.
4. Usishawishike kuiwasha na kuitumia kwa sababu tu inawaka. Usippziba ufa utajenga ukuta.

Kuna zile simu ambazo zina water resistance, ni nzuri ila kuwa na uhakika na kitu kimoja, simu yako ni factory sealed, kama ni hizi "refurbished" utalia ndugu yangu. Na ninashauri usijaribu simu yako ilowe kwa bahati mbaya tu.

Hapa Chini ni Samsung A52 iliingiwa na maji na ikawa inashindwa kuchaji. Simu imefika ofisini kwetu na tumeiweka sawa.
Kama unatatizo kama hilo, tupo kwa ajili ya kukupa ushauri mzuri zaidi juu ya kutatua tatizo kwa namna bora.

Sisi Tupo;
Barabara ya Juakali, Mwanjelwa
Mbeya
0767379327

Na mtandaoni tuko kila sehemu ya Tanzania, fuata kiungo hiki kuwasiliana nasi moja kwa moja kwa kujaza fomu mtandaoni

View attachment 2542097
IMG_20230308_190912.jpg

View attachment 2542101
 
Hello wanajukwaa, hapa ni matangazo madogomadogo,, ili pia nadhani mods hawana shida na elimu ambayo nitawapa watu kabla ya tangazo langu la biashara yangu.

Bila kuwachosha, leo tunanyooka na Samsung, tatizo moja linaweza beba matatizo matatu ndani yake:
  1. Custom Binary Blocked by FRP lock
Hili ni tatizo ambalo huwa linatokea kwenye simu za Samsung, kwa uzoefu wangu nimeona kuanzia Android 6 na kuendelea, ingawaje FRP lock yenyewe ilianzia kwenye Android 5. Baadaye Samsung kwenye Android 6 waliongeza feature hiyo ili ikitokea simu imewekwa "unofficial firmware/custom rom" na ikatokea mazingira simu ikaformat basi ifunge system na kukuletea ujumbe "Custom Binary Blocked by FRP LOck". Nadhani unajiuliza FRP Lock nini? FRP nia aina ya ulinzi ambao Google walianzisha kwenye simu za Android ili kuweza kusaidia pindi simu ikipotea. Iko hivi, kwenye simu unaweza google account yako, ukiweka tu maanake si tu itakuwezesha kudownload apps toka Google Store, bali pia ni ulinzi wa simu yako.
Ikitokea simu yako ukapoteza au kuibiwa na ikaflshiwa au kufomatiwa basi simu itahitaji account ambayo ilikuwa inatumika awali kwenye simu ili kuthibitisha uhalali wa kuendelea kutumia simu husika.

Tambua kwamba, na mara nyingi sana simu ikileta custom binary blocked by frp, ni kwamba bootloader yake ilikuwa wazi na ikafungwa tena hivyo kutokana na BINARY kuwa "unofficial" simu inablock na kushindwa kuendelea kuwaka, simu zenye shida hiyo huwa haziwaki mpaka mwisho.
photo_2023-03-09_21-55-56.jpg

2. IMEI status NG (Not Genuine)
Kipengele kingine ni hiki IMEI Status Not Genuine (NG), hapa pako direct sana. Kumbuka kuwa kila simu ina utambulisho wake wake wa pekee ambao ni kama unuani, ambao ndo IMEI namba. Kwa simu za Samsung ikitokea IMEI namba zikabadilishwa na zikawekwa zingine tofauti na ambazo zilekwa na Global System For Mobile Phone (GSM) na Samsung na yakatokea mazingira simu ikajiupdate au ikawekwa file jipya au ikafoamtiwa basi simu husika itabadilisha hadhi (status) ya IMEI kutika OK kwenda Not Genuine na ikiwa katika hali hii haiwezi kukamata network kwa sababu simu inashindwa kutambua IMEI namba.
Kwa simu za Samsung ili kujua hadhi ya IMEI ya Simu yako tumia kodi hii *#0011# italeta maelezo mengi yanahusiana na network, wewe nenda moja kwa moja kwenye IMEI STATUS au kwenye simu zingine IMEI CERT STATUS
photo_2023-03-09_21-55-50.jpg

3. Current Binary: Custom
Kwa kawaida simu inatakiwa iwe official, yaani current binary iwe official. Ukikuta simu iko CUSTOM washa full, maanake kwa namna moja au ingine imechezeshwa aidha;
  • simu ilikuwa na shida fulani wakaunlock bootloader ili kufanya simu ipokee file lisilo rasmi. Kwa mfano Samsung S8+ (G955N) ni version ya korea ya single laini lakini unaweza modify kwa kuweka file lisilo rasmi na ikawa ya laini mbili.
  • Huenda simu imebadilshwa utambulisho wake (IMEI namba), hii ni kwa sababu ili uweze kufanikisha zoezi hilo kwa njia za "bei rahisi" ni lazima ufungue bootloader na upate root prevalence kutoka kwenye, though kuna namna unaweza fanya bila kuathiri bootloader na hii inafanyika nadhani na Samsung official wenyewe, au upate access ya software zao.
NOTE: kwa sheria za Tanzania ni kosa la jinai kubadilisha IMEI namba, ni kosa kutumia simu ambayo IMEI namba iliyonayo sio yake. kwa hiyo unaponunua simu hasa mtaani kuwa makini sana.
photo_2023-03-09_21-55-53.jpg


Turudi kwenye Biashara sasa, hapo nimeelezea tatizo la Custom Binary Blocked by FRP Lock na nimeambatanisha na matatizo ambayo huwa yanaambatana na tatizo hilo moja.
Kama wewe ulinunua simu na baadae ikapata shida kama hiyo, ofisi yetu ipo tayari kukusaidia kwa gharama nafuu kabisa. Gharama sitaweka hapa kwa sababu simu zina tofautina, kwa hiyo utanitafuta kwa njia za mawasiliano hapo chini kisha tutazungumza sharti tu;
  1. Simu isiwe ya wizi
  2. isiwe ya kuokota
  3. iwe ni Samsung
  4. Uje na Receipt ya kuthibitisha uhalali wa umiliki, au uwe tayari kaundikishana na ukiri kwamba simu ni yako kweli kwenye maandishi kwenye ofisi za serikali za mtaa.
  5. Kama IMEI namba si zake, basi unatakiwa uwe na IMEI namba halisi za simu husika. IMEI namba huwa zinaandikwa kwenye box la simu au kwenye receipt uliandikiwa wakati wa kununua, au ukifungua ndani kwenye kibandiko cha battery.
NOTE: Kama huwezi timiza masharti usinitafute, au kama IMEI namba huna kuna mamlaka husika unaweza saidiwa TCRA Tanzania

Aidha natoa rai kuwa makini na ununuzi wa simu za mtaani, unapaswa kuzingatia vitu vingi sana unaponunua simu ya mtumba (ya kutoka dubai) au kwa mtu tu binafsi mtaani. Kwa usaidizi sisi tuko tayari kukusaidia kupata simu au kukusaidia kukagua simu unayotaka kuinunua bure kabisa. anuani na mawasiliano vipi mwisho wa andiko hili.

Namna ya Kutupata Sisi

Moco Services
Barabara ya Juakali, Mwanjelwa, Mbeya.
Simu: 0767379327
WhatsApp: GUSA HAPA
Website: TEMBELEA HAPA
 
Service Update
Google Pixel 6 Network Unlock

Kama unasimu umenunua nje, au hapa na ikajifunga mtandao, sisi tupo kukusaidia.

Tunafanya kazi kwenye simu aina zote (iphone ni kuanzia X)

Samsung Zote
Oppo Double Line tu
Google Pixel Zote
Motorola Zote

Hatutatui matatizo hayo tu, tunatatua matatizo mengine mengi, ni suala la wewe kuwasiliana nasi ili tujue changamoto yako na namna ya kukusaidia.

0767379327
htts://mocos.repairView attachment 2552595
IMG20230315152323.jpg
 
Back
Top Bottom