Hakika,
Mohamed Said na
FaizaFoxy wanapaswa kukubali.
''HATUKUPATA KUSOMESHWA HISTORIA HII"
Aisha ''Daisy'' Sykes mtoto wa Abdul Sykes aliandika makala ya kumkumbuka baba yake ''Abdul Sykes Nimjuaye'' ilipotimu miaka 50 toka afariki mwaka wa 1968.
Ilikuwa makala ndefu iliyochapwa matoleo matatu katika gazeti la Raia Mwema October, 2018.
Hapo chini ni hitimisho la makala hayo:
''Juma moja kabla ya kifo chake nilimuuliza baba swali ambalo jibu alilijua lakini katika hulka yake ya kawaida ya kutopenda kujikweza hakutaka achukue sifa zote kwa ule ukweli na matokeo yake.
Wakati ule nilikuwa mwanafunzi Chuo Kikuu Cha Afrika ya Mashariki, Dar - es- Salaam na mwalimu wangu wa Historia Dr. John Iliffe kwa kutambua kuwa natoka familia ya Sykes waasisi wa mwamko wa siasa katika Tanganyika na mchango wa wazee wangu katika kuunda TANU na kupigania uhuru wa Tanganyika alinitaka niandike mafanikio ya Watanganyika wa kizazi kile pamoja na historia ya babu yangu Abdallah Kleist Sykes.
Dk. John Iliffe alinitia moyo nifanye utafiti na kuandika historia hii na nilikubali kufanya hivyo.
Nilikuwa na swali kuhusu nani khasa walikuwapo katika mkutano na kushiriki wa kuibadili TAA kuwa TANU.
Baba akashauri kuwa tuombe miadi na Rais wa Tanzania Mwalimu Nyerere ili anipe ukweli niliokuwa nautafuta na kusadikisha mambo mengine yanayohusiana na historia hiyo.
Hivyo tukaenda Msasani kuonana na Mwalimu Jumamosi moja asubuhi.
Kama ilivyotegemewa Mwalimu alifurahi sana kutuona maana ilikuwa muda mrefu watu hawa waliokuwa marafiki wakubwa sana kupata kuonana.
Mwalimu alitoa ushirikiano mkubwa sana kwangu kupata ukweli kutoka kwake katika yale niliyotaka kujua kutoka kwake.
Hii ndiyo ilikuwa siku yao ya mwisho kuonana.
Allah amghufirie madhambi baba yangu na amuingize peponi.
Amin."