Mo Salah kutimkia Saudia kuungana na Benzema Al-Ittihad. Hii bandu bandu hatari kumaliza gogo

Ngoja afuate kiinua mgongo chake.

Hii niliiona mapema haswa kipindi cha friendly matches kuna dogo alikuwa akiingia sub kuchukua namba yake anakasirika mno.

Mwisho wa siku Liverpool ni Liverpool tu, nakumbuka come back ya Barcelona yeye na mane hawakuwepo ila kiliwaka mno.....

Respect 🤜 Mo kwa nguvu yako...
 
Inaweza kuwa mzaha mzaha..lakini ikaja shangaza huko mbele!!! EPL inabidi ibadilike kwenye malipo ya mishahara..Dunia sasa hivi inaonesha mabadiliko kila sehemu..ukibaki unajiamini we ni bora siku zote na na hautaki kubadilika..kupotea ni rahisi
Hapana dunia inawachezaji wengi mno waliobora, sema selection ilikuwa ndogo mno hadi kutoboa kwenda ulaya umekiona cha moto, ilikuwa inafikia wachezaji wengi kudanganya umri maana muda mwingi wametumia kutafa kuzamia ulaya.

Ila hivi sasa ni muda wa vipaji kung'aa maana nchi zimeongezeka siyo ulaya tu bali hadi uarabuni tena pote kuna pesa ya kukufanya kuishi maisha bora, hao waarabu ni upepo wa ghafla tu ila watarudi relini baada ya kuona vipaji vilivyojaa hapa duniani.
 
Boli inalipa sana.

Bongo tuendelee kulala na kuwashabikia wenzetu.

RSL naiona ikijitangaza sana kwa kuchukua mastaa wa Europe.

Sasa hivi kila kitu kuwahusu wachezaji waliotoka Europe na kwenda RSL lazima kitangazwe.
 
Wazungu wana kitu kimoja, pesa kwao sio kila kitu japo watu walikuwa wanakimbilia hapo kwa sababu ya pesa kabla ya kuja kwa hawa waarabu.

watazame bundesliga, pamoja na epl kuwakimbiza lakini wamemaintain sera yao ya kutomkabidhi majority share mwekezaji jambo ambalo lingeongeza investment na kukimbizana na epl.

wamewaondoa qatar airways pamoja na pesa zao. N.k

wamemkimbiza messi na neymar psg.

na zaidi soko la ndani bado linatosha kuilipa ligi zao.

so haya makeke ya waarabu sidhani kama yatawaangusha.
 
Miaka ya 50's hadi 70's ligi bora ilikuwa Brazil, kuanzia 70's kuja 2007 ligi bora ilikuwa Italy, 2007 hadi 2017 ligi bora ilikuwa Spain, 2018 hadi 20... ligi bora ni Epl.

Kwa hoja hiyo, usishangae baada ya miaka 10 ligi bora ikawa ya Saudia.
 
Inaweza kuwa mzaha mzaha..lakini ikaja shangaza huko mbele!!! EPL inabidi ibadilike kwenye malipo ya mishahara..Dunia sasa hivi inaonesha mabadiliko kila sehemu..ukibaki unajiamini we ni bora siku zote na na hautaki kubadilika..kupotea ni rahisi
Hilo unalosema haliwezekani.

Labda hizo club za EPL nazo zinunuliwe na hahao Saudi Arabia ambao kwa sasahivi wanaimililki New Castle na timu ikaongeza uwezo mkubwa zaidi wa kifedha right away.

Haya ni mambo ya investments zaidi. Saudi wako kwenye “promotion”
 
Miaka ya 50's hadi 70's ligi bora ilikuwa Brazil, kuanzia 70's kuja 2007 ligi bora ilikuwa Italy, 2007 hadi 2017 ligi bora ilikuwa Spain, 2018 hadi 20... ligi bora ni Epl.

Kwa hoja hiyo, usishangae baada ya miaka 10 ligi bora ikawa ya Saudia.
Waliziua ligi nyingine kwa kisingizio cha kuleta FFP, kwa sababu ligi ya uingereza ilikuwa na udhamini mkubwa ligi nyingine taratibu zikaanza kushuka Ila waarabu wamesaidia kubadili uelekeo.
 
Hapana dunia inawachezaji wengi mno waliobora, sema selection ilikuwa ndogo mno hadi kutoboa kwenda ulaya umekiona cha moto, ilikuwa inafikia wachezaji wengi kudanganya umri maana muda mwingi wametumia kutafa kuzamia ulaya.

Ila hivi sasa ni muda wa vipaji kung'aa maana nchi zimeongezeka siyo ulaya tu bali hadi uarabuni tena pote kuna pesa ya kukufanya kuishi maisha bora, hao waarabu ni upepo wa ghafla tu ila watarudi relini baada ya kuona vipaji vilivyojaa hapa duniani.
Ila me naona ligi nyingi zikiwa bora katika mabara tofauti tutapata radha bora zaid kama zamani ...

Kombe la dunia la zamani tulikuwa tunaona vipaji vipya bora kabisaa ambavyo hatujawahi kuviona tofauti na sasa...yaan ligi ya uingereza,ufaransa,italy, Germany na spain inabeba wachezaji woooote watakao chezea ligi ya timu zao za taifa katika mabara mingine yaliyoshiriki hamna kitu kipya..

Ila ikitokea ligi nje ya hizi za ulaya zikawa bora nazo tutafurahia sana ushindani na vipaji vipya kuchomoza
 
Wao wazungu nao kufika hapo wamemwaga pesa na mipango mingi.

Miaka ya 50 mpaka 70hivi ligi ya brazil ilikuwa moto mnoo.
Pele yupo kwao brazil lakini anavuta mpunga mrefu.
Copa libertodes ilianza miaka kadhaa kabla ya uefa.

Hivyo kama waarabu wakiwa namioango mizuri na hizo fedha zao, wanaweza kufanikiwa huko mbele ya safari
 
Miaka ya 50's hadi 70's ligi bora ilikuwa Brazil, kuanzia 70's kuja 2007 ligi bora ilikuwa Italy, 2007 hadi 2017 ligi bora ilikuwa Spain, 2018 hadi 20... ligi bora ni Epl.

Kwa hoja hiyo, usishangae baada ya miaka 10 ligi bora ikawa ya Saudia.
Hii umejibumbia au umetoa kwenye source gani? Tupe chanzo/source za hii taarifa
 
Waarabu sidhani kama wana mikakati ya muda mrefu. Wasije wakakata moto haraka kama wachina.

Nao walikuja kwa kasi sana naona sahivi wamekata moto.
Kitu usichokijua kuhusu wachina. Wao plan yao ni miaka 50 walichokua wanakifanya kipindi kile ni kujaribu kuwahamasisha vijana kuupenda mpira wao kwa kuwasajili mastaa kutoka ligi kubwa hivyo ni hamasa kwa watoto na vijana wanaochipukia. Kwahiyo kwa sasa bado wanaendelea na project yao na ni mapema sana kusema wamefeli.
 
Back
Top Bottom