MO haidai Simba hata shilingi moja, inamdai yeye

n kwa sababu hajafikisha target anayoitaka yeye kama yeye. Labda kuna mambo ya mkataba yanamfanya asiachie. Na pili hakuna cku tajir atasema mwaka huu nimepata faida nyng kwan wafanyakaz watadai labda kuongezewa mishahara na yeye labda hayupo tayar.
Babu yake, baba yake, baba mdogo na yeye wote wameing'ang'ania kuidhamini simba. Hivi hatushituki? Wanapata nini?
 
Hii figa ya 500b umeipata wapi hii?
Simba ni dude kubwa sana, unaweza kulitumia hata kwenye siasa kupata Urais wa nchi. Unaweza kulitumia hata kuuza madawa ya kulevya na pembe za ndovu ukatajirika. Hebu fikiria mashabiki wa simba kama wakiamua kunywa maji na vinywaji vya mo tu na kuacha maji na juice nyingine zote. Simba inashiriki mashindano ya CAF ikimtangaza mo kila kona ya Afrika na dunia.

Kupitia Simba mo alikaa meza moja na Rais wa FIFA. Ni milage kubwa sana ya mabilioni ya fedha.
 
Babu yake, baba yake, baba mdogo na yeye wote wameing'ang'ania kuidhamini simba. Hivi hatushituki? Wanapata nini?
hyo ni biashara ya familia. Hapo kuna director, had watchman. Mo hana pesa za kufanya kaz yeye kama yeye wameamua kushirikiana hapo wanagana faida tu. Simba watulie pesa iko benki.
 
Hii figa ya 500b umeipata wapi hii?
Kukaa tu meza moja na Rais wa FIFA ni bei gani? Ingemgharimu bei gani kupata milage ile ya kidunia? Je, milage ile ilimuingizia mo kiasi gani kwenye biashara zake kimataifa?.

Kaka unapohesabu hasara na faida usiangalie fedha/cash ya moja kwa moja tu.
 
Haiishi tu Mo kuidai simba billions of shilings! Yeye na familia yake ndiyo wamiliki halali wa timu ya simba. Kama huamini muulize Mangungu.
Deni linazidi kukua ipo siku. Wanasimba wataamka na kukuta simba ni ya mo na mo ni wa simba 💯
 
Mkuu kavulata madawa ya kulevya hapana😃😃😃. Bado tunamkumbuka aliyekua Kocha wetu wa makipa Muharam Sultan anasota gerezani mwaka wa tano sasa kwa tuhuma za kujihusisha na biashara ya dawa za kulevya

Nakubaliana na wewe kua Simba (na hata Yanga) ni dude kuubwa na ina ushawishi mkubwa kiasi hata watu wanaweza kupitia huko kutimiza agenda zao ziwe za kisiasa, kijamii au kibiashara

Ndio maana unaona hata serikali haiwezi kukubali kuziachia hizi timu zimilikiwe na mtu mmoja ili asije akazitumia tofauti

Kama huamini angalia mchakato wa transformation kwenye Simba kama utakamilika kwa muundo unaopendekezwa sasa.

Hicho kitu hakitatokea sababu serikali haikubali mtu amiliki dude linalobeba sapoti ya zaidi ya watu milioni 20 au 30 wakiwemo viongozi wa juu wa nchi, taasisi za ulinzi na usalama nk

Hata Mwakyembe alipokua Waziri wa Michezo aliwahi kuyasem haya.
 
UKo sahihi sana. Hata hivyo kubali tu kuwa timu hizi zimetumika sana kuingiza madawa ya kulevya nchini na kuvusha nyara za serikali nje ya nchi hasa pale zinapokwenda na kurudi kutoka pre-seasons nje ya nchi, kwakuwa hazikaguliwi sana pale airport. Ndani ya mipira na vifaa vya michezo vyao huwa kunawekwa na mambo mengine. Kuna wakati pia wanazitumia kuchezea kamali na kuvuna mapesa mengi kwenye beting. Wahindi sio wajinga hivyo, ndio maana wanazing'ang,ania hizi timu zama na zama, Vizazi na vizazi wamo tu.

Kuna wakati akina Abbas Ngulamali na Azim Dewji wanaahidi zawadi kwa wachezaji za TV au magari lakini wao wanaingiza makontena na makonteza bila ushuru wakidai ni zawadi za wachezaji walizowaahidi.
 
Kama Mo anaona kwamba simba inampa hasara kwanini bado anaendelea kuwepo ! Sehemu unapata hasara afu unaeendelea kubaki mimi nahisi huyu mo ni mswahili swahili sana
 
Matangazo aliyoweka katika jezi Kwa mwaka analiia shs ngapi?
 
Hivi kuna kampuni hapa Tanzania inayoweza kuilipa Simba bilioni 30 kwa mwaka kutangaza biashara?
 
Ndugu tutajie kampuni yoyote inayoweza kuzilipa Simba au Yanga bilioni 30 kwa mwaka kutangaza biashara zake.
 
Bila MO simba ni sawa na Maji Maji
 
Mbumbumbu ndiyo waliwao. Toka nizaliwe sijawahi kuona watu wanadhulumiwa timu ya mpira.
 
Jidanganye.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…