Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 5,303
- 18,458
Humu kwenye Uzi mwingine nimechangia hoja kwamba MO anadai bilioni 100 kama mtamwambia aondoke na nikaenda mbali zaidi kwamba endapo wanachama wa simba idadi yake ni milioni 10 basi Kila mmoja achange bk 30, (30,000), ili kumurudishia huyu mwamba lakini mbali ya kutoa hizo pesa kasahau kutuaambia faida itokanayo na mauzo ya jezi na dhamamana za simba sc pia pesa zinazo tokana na mashindano mbalimbali"Kutoka 2018 hadi leo nimewekeza Billioni 45 kwa ajili ya mshahara, usajili, maandalizi ya timu na mahitaji mengine ya uendeshaji. Pia nimechangia Shillingi Billioni 20 kama sehemu ya ununuzi wa hisa ya asilimia 49 ndani ya Simba Sport Club, na mara nyingi nimekuwa nikitoa msaada nje ya mfumo rasmi kila palipojitokeza uhitaji wa dharura kuanzia mwaka 2017-2024 nimetumia takribani Billioni 24 katika misaada ya dharura na hivyo kufanya jumla ya mchango wangu kwa Simba SC kufikia Billioni 87. Hivyo kusema MO hatoi hela ni kauli ya kupotosha yenye muelekeo wa chuki." Mohamed Dewji
Huko Simba hamna uwazi wa mapato na matumizi?Rais wa Heshima wa Klabu ya Simba SC, Mohammed Dewji (Mo), amesema dhamira yake ya kuijenga Simba kuwa klabu bora barani Afrika haijabadilika, huku akibainisha kuwa tayari amewekeza zaidi ya Sh bilioni 87 ndani ya klabu hiyo tangu mwaka 2017.
View attachment 3406124
Akizungumza kwa njia ya video leo jijini Dar es Salaam, Mo Dewji amesema licha ya changamoto mbalimbali za msimu uliopita, Simba imeonyesha uimara mkubwa na kufikia mafanikio ya kihistoria, ikiwemo kucheza fainali za CAF mara mbili - jambo ambalo halijawahi kufanywa na klabu nyingine kutoka Tanzania.
"Simba bado ipo kwenye hatua ya ujenzi. Roho ya ushindi haijawahi kuyumba. Tunajipanga upya kwa msimu ujao na kipaumbele kitakuwa kwenye usajili wa kimkakati na kuimarisha benchi la ufundi," amesema Mo.
Ameongeza kuwa mbali na uwekezaji wa mishahara, maandalizi ya timu na matumizi ya uendeshaji, pia ametoa mabilioni kama msaada wa dharura kwa klabu, jambo ambalo halipaswi kupotoshwa au kubezwa.
"Tangu mwaka 2017 hadi sasa, nimetumia Sh bilioni 22 kwa mahitaji ya dharura pekee. Kauli kwamba Mo haitoi hela ni upotoshaji wenye malengo ya chuki," alisisitiza.
Mo pia ametoa wito kwa wanachama na mashabiki wa Simba kuachana na maneno ya chuki na badala yake wajikite katika mshikamano, kushirikiana na kujenga klabu kwa pamoja.
"Nimewekeza muda, jasho, damu na fedha Simba. Sio kwa sababu nyingine, bali kwa mapenzi ya dhati kwa klabu hii na kwa taifa letu. Doto yangu haijabadilika," amesema.
Anavyowachukulia wanasimba ni kama wanasiasa wanavyowachukulua watanzania.MO ni mnyonyaji halafu hata kama ni tajiri ni among rhe low IQ people.
Ukimsikiliza kwa makini analazimisha umuhimu na inaonekana yeye ndo anaisaidia simba (one way) kila siku anataja matumizi (expenditures) hajawahi kusema hata siku moja Simba imemuingizia shiling ngapi (income au revenue)
Katika hali ya kawaida ni mfanyabiashara gani atafanya biashara zaidi ya miaka mi 5 kwa hasara?the guy is so naive anatupna sijui mazuzu sisi
Hebu na nyie basi waandishi muwe professional hebu muulizeni simba imemuingia Tsh hadi leo?
Faida yoyote ile duniani una calculate kwa kuchukua
Mapato(income au sales) kutoa matumimizi
Club kubwa kama simba lazima iingize mapato makubwa kuliko matumizi asituchezee
Hakuna mfanyabiashara anaweza kusema hivyo ๐Yale matangazo na mabango mengine kwenye jezi yamemsaidiaje kibiashara?
Ni kweli Simba inamzalishia hasara lakini kuna faida pia, awe mkweli.
๐ ๐ ๐ Rais wa heshima wa SimbaAnaongea kwenye video live chumbani kwake ili waandishi wasimhoji,kwenye press huwezi kumwona,unawekaje jasho,damu,fedha kwa biashara ambayo haikuingizii faida na kuacha hutaki,akawadanganye wajinga
๐คฃ๐คฃ๐คฃAnaongea kwenye video live chumbani kwake ili waandishi wasimhoji,kwenye press huwezi kumwona,unawekaje jasho,damu,fedha kwa biashara ambayo haikuingizii faida na kuacha hutaki,akawadanganye wajinga
He is very crafty๐ ๐ ๐ Rais wa heshima wa Simba