Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 4,393
- 14,500
Rais na Mwekezaji wa Simba SC ametangaza mabadiliko makubwa ya kiuongozi ndani ya klabu hiyo, akibaki na nafasi yake ya Rais lakini akikabidhi Uenyekiti wa Bodi kwa kiongozi mpya kutokana na majukumu yake mengine na kutokuwepo mara kwa mara nchini.
Kupitia taarifa rasmi, amesema ni muhimu Simba ipate mwenyekiti ambaye yupo karibu na shughuli za kila siku za klabu. “Nitaendelea kubaki kama Mwekezaji na Rais wa Simba SC, lakini nafasi ya Mwenyekiti wa Bodi sasa inakabidhiwa kwa kiongozi mpya,” ameeleza.
Kwa mamlaka aliyopewa chini ya Katiba na Kanuni za Kampuni (MEMARTS) ya Simba Sports Club Company Limited, Ibara ya 41, amemteua Crescentius Magori kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Simba SC.
Aidha, ametangaza wajumbe wapya wa Bodi upande wa Mwekezaji ambao ni, Barbara Gonzalez aliyewahi kuwa Mkurugenzi Mtendaji (CEO) wa Simba mwaka 2020, na kuwa kama CEO wa kwanza mwanamke katika historia ya klabu hiyo
Safu ya Wajumbe wa Bodi ni:
• Barbara Gonzalez
• Hussein Kitta
• Azim Dewji
• Rashid Shangazi
• Swedi Mkwabi
• Zuly Chandoo
• George Ruhango