MO Dewji akanusha kuzungumza kuhusu pesa za tetemeko la ardhi Kagera

Ghazwat

JF-Expert Member
Oct 4, 2015
23,718
66,267
3ac58399e04ec750529b63389a9385e4.jpg
Mkurugenzi Mtendaji wa Makampuni ya Mohammed Enterprises Tanzania Limited (MeTL Group) Mohammed Dewji amekanusha taarifa ambazo zimesambaa katika mitandao mbalimbali ya kijamii kuwa amefanya mahojiano na kituo cha Radio cha Times FM kuhusu pesa zilizochangishwa katika tetemeko la ardhi la Kagera lililotokea mwezi Septemba, 2016

Dewji amesema hajafanya mahojiano na kituo chochote cha habari kuhusu tetemeko la Kagera na habari hiyo haina ukweli wowote zaidi ni mbinu ambayo imetumiwa na baadhi ya watu kwa ajili ya kuchafua jina lake na kampuni yake ya MeTL Group ambayo mpaka sasa ina wafanyakazi zaidi ya watu 28,000

Aidha Dewji amesema ana imani na Serikali ya awamu ya tano na kuwatoa hofu watanzania kuwa ataendelea kushirikiana na Serikali kusaidia jamii yenye uhitaji ikiwa ni sehemu ya ahadi yake ya kutumia nusu ya utajiri wake kusaidia watu wenye uhitaji

"Nitumie nafasi hii kuwajulisha watanzania wenzangu kuwa hii habari ambayo inasambazwa na watu katika mitandao ni ya uongo na haina ukweli wowote, sijafanya mazungumzo na Media yoyote na mimi nilichangia pesa kwa nia nzuri, nina imani na Serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais Dk. John Magufuli kuwa inafanya kazi kwa faida ya watu wote bila kufanya ubaguzi". amesema Dewji.

Chanzo: Dewji blog
 
MO Dewji akanusha kuzungumza kuhusu pesa za tetemeko la ardhi Kagera
 
Nitaifutilia Hii Thread Hadi Mwisho Wake Kama Nilivyofanya Kwa Ile Ya Jana!
 
Huyu jamaa nae anapenda kuongelewa kwenye Media kapotezwa sana na Bahkresa, Forber ndiyo wanambeba jamaa huku Azam anafanya maajabu Mo amebaki kwenye social network
 
Kwani yeye hasomi alama za Nyakati? Shivji alipohojiwa alijibu nini?

Sizonje sio MTU WA mchezo mchezo
 
Huyu jamaa nae anapenda kuongelewa kwenye Media kapotezwa sana na Bahkresa, Forber ndiyo wanambeba jamaa huku Azam anafanya maajabu Mo amebaki kwenye social network

Halafu hili suala la kukumbusha kumbusha kwamba kawajili Watanzania elfu ishirini na nane - kwa nini anapenda penda sana kuyarudia rudia - Bakheresa mbona hana kawaida ya kusema/jisifia kwa hilo.
 
tofauti na Mada. msaada mwenye no ya huyu kaka MO Tafadhari anisaidie. mambo mambo nataka nikajifunze mwenzenu..
 
Huyu jamaa nae anapenda kuongelewa kwenye Media kapotezwa sana na Bahkresa, Forber ndiyo wanambeba jamaa huku Azam anafanya maajabu Mo amebaki kwenye social network
Hahah afu Interview zake hua ananifurahisha sana hii sentence hua lazima aiseme"sijui mzingo wa dunia ni km 52,000 sisi Co. Yetu inatengeneza majora ya nguo kuzunguka mara 2 ya dunia" hahah angalia interview zake Kwenye mkasi,CNBS kokote pale lazima aseme hio sentence.Sijui hua hajiamini.
 
Bakhresa aliahidi 100mil,Mengi ye 110mil,sijui wana hali huko.Hahah
 
Back
Top Bottom