Lituye
JF-Expert Member
- Dec 27, 2015
- 1,864
- 5,697
Tafadhali salamu zetu mashetani zikufikie popote ulipo Ndugu Mnyoshaji nchi yetu hii ya kusadikika.
Tangu utuambie unanyoosha hii nchi mambo tunaona yanazidi kupinda tuu wala hayanyooki ndugu mnyoshaji.
Bei ya Sukari inazidi kupaa, Sembe na dona bei hazishikiki tena machozi ya wanachuo waliokosa Ada yanatulowesha Abiria tunao kaa nao ktk siti za vyombo vya usafiri kila siku.
Halafu hali ya usalama kwa mashetani Wa nchi hii ni mbaya. Kuna aina ya Mashetani mabaya yamezuka hivi karibuni hapa ktk kaya yetu.
Mashetani haya mabaya yakikuvagaa mwilini unajikuta upo ktk mfuko wa Sandarusi ukiwa na mawe mazito ndani ya mto fulani ukipumua kwa shida sanaa.
Ulituomba tukuombee Dua Ndugu mnyoshaji sisi mashetani tukaomba usiku na mchana, tukaweka mpaka mikono ya Baraka ktk ile sanamu yako lakini mambo tunaona magumu. Sasa sijui tukuwekee miguu huenda ahueni ikapatikana.
Ndugu Mnyoshaji hebu jaribu kuwa na huruma japo kidogo kwa sisi mashetani japo tuachiepo hata ka Uhuru ka kukutana na kutoa maoni yetu huku tukipiga miayo ya njaa.