Mnyonge mnyongeni haki yake mpeni.

Karibuni

New Member
Jan 13, 2013
4
0
Ku tokana na matatizo yaliyojitokeza katika chuo cha madini napenda kuwataarifu kuwa vijana hawa pamoja na kuwa na moyo wa uvumilivu na busara machozi yao yalikua yanaonyesha dalili za kukauka kama sio kuisha yamebadilika na kua machozi ya damu. Hali hii inatokea pale majibu yanayotolewa na mwenyekiti wa bodi wa chuo hicho baada ya kuwaita viongozi wa serikali na kuwapa majibu ambayo hayakuonesha utu bali yalikua yakiwakandamiza wanafunzi hao.Wanachuo hao walitegemea matokea yao kubadilika na kuwa mazuri au ya kuridhisha baada ya kuahidiwa na mwenyekiti wa bodi yao yatashughulikiwa kwa kwena tume ,ila hakuna chochote kilichofanyika .Baadhi ya hoja wanafunzi walizozitoa na kuhaidiwa zitafanyiwa kazi na mwishoni hakuna kitu kilichofanyikaau kubadilika ni;
· Mitihani kutungwa nje ya azimio la masomo yao · Mitihani kusahihishwa na walimu wasiokidhi(wasio na sifa)
· Kufanya mitihani kwa muda wa kusadikika.
· Mitihani kusahihishwa “BAR” hoteli iliyoko Morogoro. Licha ya hoja hizo kuwa na mashiko vijana hawa wanatishiwa na wameambiwa wasiotaka kufanya mitihani ya supp watakua wamejiondoa wenyewe chuo yani tayari watakua wamedisko. Ila hoja ya msingi ni moja kama matatizo yote haya inasemekana yanajirudia Je akili hizi hizi zilizoleta matatizo hayo zinawezaje kuyamaliza matatizo hayo?Watanzania wenzangu na wanataaluma ya madini hebu tuwasaidie hawa vijana wa Kitanzania vijana maskini wanaonyanyaswa na watu wasiokua na huruma, kwani hii ni sawa binti au mwanamke ambaye anatoa mimba bila kujua thamani ya mimba au mtoto yule anayeamua kumuua kwa makusudi .


Kibwetere Maji.
 
Acha kupotosha ukweli waliofeli ni halali yao chuo hakiandai wahuni wa kubebwa kila muhula.
 
Wewe ndio muhuni kwani hujui ukweli, hawa vijana hawana shida tena wengine wako vizuri kuliko waalimu wao, Wewe ni kibaraka tu au hujui bifu waliowekewa hao vijana ni kuhusu nini funguka..............................
 
Back
Top Bottom