Mnyika: Serikali iache usiri miundombinu ya gesi

babalao 2

JF-Expert Member
Apr 6, 2012
5,398
3,243
MBUNGE wa Jimbo la Ubungo John Mnyika, ameitaka Serikali kuweka wazi mradi wa miundombinu ya gesi asilia ambayo itahusisha ujenzi wa mitambo ya kusafishia gesi asilia katika mikoa ya Lindi na Mtwara pamoja na ujenzi wa bomba kuu la kusafirishia gesi hiyo kutoka Mtwara hadi Dar es Salaam.

Mnyika ambaye pia ni Waziri Kivuli wa Nishati na Madini alisema hayo katika taarifa yake aliyoitoa jana Dar es
Salaam kwa vyombo vya habari.

Alisema Serikali ilipaswa kuwasilisha bungeni na kuweka wazi kwa umma mkataba wa mradi husika ili
Bunge lishauri na kuisimamia Serikali kuanzia katika hatua za awali ili kuhakikisha maslahi ya Taifa yanalindwa
na wananchi wananufaika kutokana na fursa za uwekezaji huo mkubwa.

Mnyika alisema Julai 27, mwaka huu, alitoa pendekezo la Serikali kuweka wazi mradi huo, lakini haikuzingatia na
badala yake Rais Jakaya Kikwete alifanya uzinduzi wa mradi huo Novemba 8, mwaka huu, huku akidai
kuwapo usiri, jambo linalozua malalamiko katika maeneo ya mradi husika hususani Mtwara.

"Serikali irejee katika mapendekezo niliyotoa bungeni na itoe maelezo ya sababu za bomba hilo kujengwa kutoka Mtwara mpaka Dar es Salaam na ieleze kwa uwazi manufaa ya mradi huo na miradi mingine
inayopaswa kutekelezwa katika mikoa ya Kusini kwa maendeleo ya wananchi husika," alisema Mnyika.

Alisema katika hotuba hiyo, pia alizungumzia ujenzi wa mitambo miwili ya kusafishia gesi asili ya Mnazi Bay na
SongoSongo kama sehemu ya mradi huo; ambapo Serikali inapaswa kueleza ni miradi ipi inayoambatana na mradi huo iliyopangwa kuwanufaisha wakazi wa Lindi na Mtwara ikiwemo kuharakisha utekelezaji wa mradi wa
kuzalisha umeme wa megawati 300 Mtwara na 230 wa Somanga Fungu (Kilwa).
 
Back
Top Bottom