Mnyika na Mkutano wa mtandao kutoa maoni juu ya SSRA na NSSF | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mnyika na Mkutano wa mtandao kutoa maoni juu ya SSRA na NSSF

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by ukweli2, Aug 5, 2012.

 1. u

  ukweli2 Member

  #1
  Aug 5, 2012
  Joined: Nov 18, 2011
  Messages: 67
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 15
  Habari za j2 wadau

  Kutoka kwa John Mnyika>>>>>....Leo saa saba hadi tisa alasiri,mkutano wa mtandaoni kutoa maoni juu ya suala la SSRA na NSSF! Mjadala utakuwa ktk: mnyika.blogspot.com!

  Mnyika: Nalazimika kukusanya maoni kwa hatua ya sasa kupitia njia ya mtandao kutokana na udharula wa hoja husika

  Source: Mnyika on Twitter
   
 2. King Kong III

  King Kong III JF-Expert Member

  #2
  Aug 5, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 25,153
  Likes Received: 2,402
  Trophy Points: 280
  Mnyika yupo JF aje na huku achukue maoni.

  1.Fao la kujitoa liwepo kwa sababu mifuko ya hifadhi za jamii ya tz haifanyi kazi kama huko usa wanapotaka kufatisha hyo sheria ya kuzuia kuchukua fao la kujitoa....Wao Social Security inawalinda incase ukipoteza ajira unakuwa unalipwa

  2.Mifuko ya hifadhi za Jamii iwe inawapa bonus ya faida wanayopata kwenye uwekezaji.

  3.Katika kipindi ambacho mtu anafanya kazi aruhusiwe kukopa fedha zake kwa riba nafuu (5%) @lst nusu na awe anakatwa kila mwisho wa mwezi.

  4.Serikali isiwe na mamlaka ya kuiingilia hyo mifuko kwani ssra ipo,na hao wakurugenzi wapunguziwe mishaara na posho!! Haiwezekani mkurugenzi analipwa mil25 p.m na posho hadi 1.5m kwa siku,come on!!!
   
 3. G

  Gagnija JF-Expert Member

  #3
  Aug 5, 2012
  Joined: Apr 28, 2006
  Messages: 6,316
  Likes Received: 618
  Trophy Points: 280
  Mmeshindwa kufanya kazi ya uwakilishi tuliyowatuma, mmebaki kuitisha mikutano mtandaoni. Siku sheria inapitishwa mlikuwa mmelewa?
   
 4. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #4
  Aug 5, 2012
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  ndugu swala hili wewe ulilisikia kwa mara ya kwanza..je ulilisikia likijadiliwa? je kipengele cha kuzuia kuchukua pensheni ulisikia kikijadiliwa..kwanini hata wafanyakazi pamoja nakufatilia bunge hawa kupiga kelele kipindi hicho...kifupi tuna serikali ya kihuni
   
 5. King Kong III

  King Kong III JF-Expert Member

  #5
  Aug 5, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 25,153
  Likes Received: 2,402
  Trophy Points: 280
  Mkuu usimlaumu mnyika mie nilisikiliza bunge april na kwa jinsi ile hoja ilivyoletwa pale yani nilikua naona full neema lkn kumbe kile kitanzi cha fao la kujitoa hakikuwekwa wazi.
   
 6. G

  Gagnija JF-Expert Member

  #6
  Aug 5, 2012
  Joined: Apr 28, 2006
  Messages: 6,316
  Likes Received: 618
  Trophy Points: 280
  Mnyika alitakiwa kupiga kelele kwa kuwa kama mbunge alipewa huo mswada kabla ya kujadiliwa. Nitajie mfanyakazi mmoja tu aliyepewa huo mswada tofauti na wabunge ambaye ulitaka apige kelele. Kama kifungu cha kuzuia kuchukua mafao ya kujitoa hakikuwepo kwenye mswada, basi sheria hiyo itakuwa batili, lakini kama vilikuwemo hakuna mbunge anayeweza kukwepa lawama.
   
 7. Nduka

  Nduka JF-Expert Member

  #7
  Aug 5, 2012
  Joined: Dec 3, 2008
  Messages: 8,479
  Likes Received: 761
  Trophy Points: 280
  Hivi taaluma ya Mnyika ni nini?
   
 8. Lambardi

  Lambardi JF-Expert Member

  #8
  Aug 5, 2012
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 10,314
  Likes Received: 5,605
  Trophy Points: 280
  Hoja ya Mnyika ina mashiko sana sana hao NSSF PSPF kwanza wapungize mamlaka ya kuamua lolote kwenye pesa zetu!pia hao wakurugenzi walipwe mishahara stahiki sio kulipwa kama wao ndio wanatengeneza hizo pesa,wao wanasubiri mwisho mwezi ziingie kutwa wako semina na safarini!tunataka uwezo wa kuchukua pesa zetu!na waliopo kazini waweze kukopesha nusu ya ile pesa yao.....itasaidia sana
   
 9. makusanya

  makusanya JF-Expert Member

  #9
  Aug 5, 2012
  Joined: Jun 7, 2011
  Messages: 551
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 45
  kwani ndugu yangu hiki anachofanya Mnyika hapa ni nini?au uwakilishi wa wananchi we unautafakari vipi?si kukusanya maoni ya wananchi na kwenda kuwasemea pale bungeni ama?pole sana kama hata wewe great thinker umeshindwa kulitambua hilo basi tanzania bado tuna wajinga wengi kuliko hata viongozi wetu wanavyofikiri.

  Matokeo ya shule za kata hizo
   
 10. makusanya

  makusanya JF-Expert Member

  #10
  Aug 5, 2012
  Joined: Jun 7, 2011
  Messages: 551
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 45
  we inafikiri itakusaidia nini kwenye hii hoja??au ujaona chakujadili kabisa?
   
 11. makusanya

  makusanya JF-Expert Member

  #11
  Aug 5, 2012
  Joined: Jun 7, 2011
  Messages: 551
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 45
  we unafikiri itakusaidia nini kwenye hii hoja??au ujaona chakujadili kabisa?
   
 12. G

  Gagnija JF-Expert Member

  #12
  Aug 5, 2012
  Joined: Apr 28, 2006
  Messages: 6,316
  Likes Received: 618
  Trophy Points: 280
  Na riba ya mikopo hiyo isizidi mara mbili ya ile inayotolewa na mifuko kwa waanachama. Kwa mfano NSSF wanatoa riba ya 1.8 kwa mwaka, hivyo nikikopa nilipe riba isiyozidi 3.6 na bonus wanazojilipa wafanyakazi wa mifuko zifutwe.
   
 13. Nduka

  Nduka JF-Expert Member

  #13
  Aug 5, 2012
  Joined: Dec 3, 2008
  Messages: 8,479
  Likes Received: 761
  Trophy Points: 280
  Suala la mifuko ya hifadhi ni la kitaaluma sana, linahusisha sheria, uchumi, sayansi ya jamii, acturial n.k. Kujua taaluma ya Mnyika ni muhimu kwani tunaweza kumshauri kwa kuangalia mawazo yake yamebebwa na muelekeo gani kitaaluma. Ukiongea na Lissu ni dhahiri utagundua orientation yake ni sheria na mawazo yake yatakuwa yame base huko. Hivyo hivyo kwa Zitto ambaye ni mchumi na Slaa ambaye ni padri.
   
 14. T

  Tewe JF-Expert Member

  #14
  Aug 5, 2012
  Joined: Jan 11, 2008
  Messages: 744
  Likes Received: 183
  Trophy Points: 60
  Sitaki hata kuisikia pspf, nilifanya kazi miaka mitano nikaamua kuacha nilipouliza pesa niliyokua nakatwa nikaambiwa sijafikia mudawa kustahafu sasa nachukia ajira za serikali kuliko za kihindi
   
 15. k

  kukukakara JF-Expert Member

  #15
  Aug 5, 2012
  Joined: Jul 31, 2012
  Messages: 455
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 45
  Mnyika anafanya vema juu ya hili.
  schemes za Nssf na PsPf michango yake haipangwi kutegemea umri wa mtu (Mortality rate) kama ilivyo ktk endoment schemes za life insurance ambazo hulazimisha mipaka ya benefits kama early witdrawals na maturity. Schemes hizi zina faidika sana kwa kuwa na backing ya ulazima kisheria tofauti na life insurance, kwa jinsi hii hazpawi kuwa na mashaka ya kushiwa(overdrawing) endapo kila member atachukua anachostahili tu. Kinachoonekana ni mashaka juu utoshelezaji wa jukum hili'kwa members na matumizi mengine ya fund hizi kama unprudent investiments na hasa mikopo kwa wafanyabiashara na serikali. Je daraja la kigamboni litarudisha lini pesa ili mfanyakazi alipwe ... Ndio maoni yangu
   
 16. King Kong III

  King Kong III JF-Expert Member

  #16
  Aug 5, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 25,153
  Likes Received: 2,402
  Trophy Points: 280
  Mchumi wa dalaja la kwanza!
   
 17. Nduka

  Nduka JF-Expert Member

  #17
  Aug 5, 2012
  Joined: Dec 3, 2008
  Messages: 8,479
  Likes Received: 761
  Trophy Points: 280
  Kwa hyo taaluma ya Mnyika ni nini?
   
 18. Polisi

  Polisi JF-Expert Member

  #18
  Aug 5, 2012
  Joined: Nov 22, 2010
  Messages: 2,087
  Likes Received: 39
  Trophy Points: 145
  Atueleze kwanza wakati hii sheria inafanyiwa marekebisho bungeni mwezi Aprili alikuwa wapi? Kwanini hakuiinga kipindi hicho?
   
 19. A

  Asha Abdala JF-Expert Member

  #19
  Aug 5, 2012
  Joined: Mar 21, 2007
  Messages: 1,134
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0

  We Polisi, si uende huku ulipoelekezwa kwenye mkutano ukamuulize hilo swali akujibu? Ndio nyinyi mnaalikwa kutoa maoni mnakacha mikutano halafu wengine wakifanya maamuzi kwa niaba yenu mnalalamika na kupinga baadaye.

  Asha
   
 20. Zipuwawa

  Zipuwawa JF-Expert Member

  #20
  Aug 5, 2012
  Joined: Nov 28, 2010
  Messages: 3,052
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 145
  Nini cha ajabu kufanya mkutano kwenye mtandao katika karne hii ya science na technology?
   
Loading...