Mnyika kuzindua kanda ya Kusini rasmi

Mnyika kuzindua kanda ya Kusini rasmi

CHADEMA

Political Party
Joined
Apr 13, 2013
Posts
495
Reaction score
2,539
Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kitakuwa na kikao cha Kanda ya Kusini ambacho hotuba ya ufunguzi itatolewa na NKMB JJ Mnyika, leo kuanzia saa 10.00 asubuhi Ukumbi wa, karibu na Maisha Club. kesho pia atafanya mkutano mkubwa hapo Mtwara Mjini kuanzia saa 8 mchana.
Ziara hiyo ni mwendelezo wa maboresho ya Kanda za Chama ikiwa ni maandalizi kuelekea uchaguzi Mkuu..

Ziara ya kanda ya Kusini itakuwa inahitimisha ziara za maboresho ya kanda nane za Tanganyika zilizo anza tangu mwezi Februari ikiwa ni azimio la Kamati kuu la kuziboresha kanda nane za kichama za Tanganyika kabla kuelekea Zanzibar na kuboresha kanda mbili za upande wa visiwani.

Vikao vya kanda ya Kusini vitakuwa vitatu.

1. Kikao cha Kamati tendaji ya kanda

2. Kikao cha baraza la uongozi la kanda.

3. Kikao cha wadau wa kanda ya Kusini

Vikao Kama hivyo vimeshafanyika kwenye kanda nyingine saba za Tanganyika ambazo ni.

1. Pwani (DSM na Pwani)

2. Serengeti (Shinyanga, Mara na Simiyu)

3. Kati (Dodoma, Singida na Morogoro)

4. Kaskazini (kilimanjaro , Tanga, Arusha na Manyara)

5. Juu Kusini (Mbeya , Iringa, Njombe, Rukwa na Ruvuma)

6. Victoria (mwanza , Kagera na Geita)

7. Magharibi (Kigoma , Tabora na Katavi ).

Mfumo wetu wa kanda umekuwa mfumo bora wa kuishii sera yetu ya majimbo na falsafa ya ugatuzi wa madaraka (decentralization).

Kila kanda ya kichama imewezeshwa kwa kuwa na makao makuu ya kisasa pamoja na Gari na pikipiki mpya zaidi 50 ili kuwezesha kazi za kisiasa kwenye kanda husika.
 
Twende mwanakwetu Mnyika, twende commander.....

Peoples power
 
Mmechelewa, Mtwara twasubiri kuipokea ACT Wazalendo, Chadema ni chama cha kaskazini
 
Chadema hamtuonei huruma? Huku Lissu na Lema, kule Bavicha, pale Jj mnyika, hapa Mawazo
 
Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kitakuwa na kikao cha Kanda ya Kusini ambacho hotuba ya ufunguzi itatolewa na NKMB JJ Mnyika, leo kuanzia saa 10.00 asubuhi Ukumbi wa, karibu na Maisha Club. kesho pia atafanya mkutano mkubwa hapo Mtwara Mjini kuanzia saa 8 mchana.
Ziara hiyo ni mwendelezo wa maboresho ya Kanda za Chama ikiwa ni maandalizi kuelekea uchaguzi Mkuu..
Kikao cha chama kinaanza saa 10 asubuhi?!
 
Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kitakuwa na kikao cha Kanda ya Kusini ambacho hotuba ya ufunguzi itatolewa na NKMB JJ Mnyika, leo kuanzia saa 10.00 asubuhi Ukumbi wa, karibu na Maisha Club. kesho pia atafanya mkutano mkubwa hapo Mtwara Mjini kuanzia saa 8 mchana.
Ziara hiyo ni mwendelezo wa maboresho ya Kanda za Chama ikiwa ni maandalizi kuelekea uchaguzi Mkuu..
Kazi makini kwa viongozi makini kama @myika natarajia mafanikio makubwa ongereni chadema
 
Twende mwanakwetu Mnyika, twende commander.....

Peoples power

Kamanda vipi?.Mbona unaonekana una raha sana,mnaenda kuvunja ngome za CUF kwa mwamvuli wa UKAWA.Mimi nawatakia kila la kheli lakini nchi hii inahitaji WAZALENDO zaidi.Tukimaliza ziara ya mikoa kumi,Tunakuja kaskazini kuhubili uzalendo na kutoa majawabu ya matatizo yanayo ikumba nchi yetu.Watanzania wa sasa ni waelewa huwa wanapima mambo kabla yakufanya uamuzi,Nachowasihi mnadi sera zenu huko mtwara mtawafanyia nini wananchi na mtaunda serikali ya aina gani baada ya kuingia IKULU.Nawatakia kila la kheli MAKAMANDA lkn mkumbuke kutenda yale mnayohubili.
 
Mihemko ya CCM na vimada wao ACT inafurahisha sana ... Watanzania si wajinga tena .... Wanajua majukumu ya ACT ni kudhoofisha upinzani nchini ..
 
wakati wao wakiomba tubomoke,watabomoka wao,Chadema ni mpango wa mungu...go go go Chadema,watakiona cha moto mwaka huu.
 
Back
Top Bottom