Mnyika kukata rufaa hukumu ya Spika

Mnyika kukata rufaa hukumu ya Spika

Tatizo la maji ni la Dar es Salaam na Tanzania nzima, acha ubinafsi. Sehemu nyingi Dar watu hawajui maji ya bomba kwenye nyumba zao. Mhe. Nyika ni jembe na mtetezi wa watanzania. Acha atetee umma wa watanzania, yeye siyo DAWASCO! Anafanya kazi yake, sasa kama watendaji wanamuangusha unataka atumie posho yake kukuletea wewe maji?
Siyo posho, afuatilie sisi ndo waajiri wake
 
Mkuu sina nia ya kumtetea Mnyika,bali nina nia ya kukuamsha wewe na wa-Tz wenye mawazo kama wewe usingizini mtambue nani mnayepaswa kumwonyesha kuwa mna hasira juu ya kero sugu ya maji, pamoja na kero nyingine mbali mbali wakati mnachunwa ngozi mkiwa hai kutokana na kodi mnazotozwa kila upande!! Tafakari!!!

Posho ya Mhe. Unayemtetea inalipwa na kodi ya nani?
 
Hivi wale wabunge ambao hawana kesi wala si machachari kama Mnyika wapewapelekea maji wapiga kura wao? Je mbunge wenu wa kwanza ambae hakuwa machachari kama Mnyika aliwaletea maji?

Hatufukui makaburi, tunasonga mbele
 
anna makinda kaamua kuilinda serikali tu,,tuhuma za maswi na muhongo dhidi ya kamati ya bunge ni za kweli wala hazina ubishi......
 
Twende mbele turudi nyuma, hivi ushahidi wa rushwa ni nini? Si ninaweza kubisha mpaka kuche kuwa sikutoa/pokea? Au siku hizi risiti zinatolewa?
 
Je Mhe. Mnyika hiyo rufaa yako itatumalizia wana Ubungo tatizo la Maji Au la. Ohhh usitulaumu 2015 wewe kalia ya kujitafutia umaarufu wakati sisi wapiga kura wako tuna kero kibao na huzishughulikii. Rufaa hizo 2015 zitakupigia kura.

Kuna maslahi ya nchi yanayogusa majimbo yote kwa ujumla wale. Mnyika yuko sawia kabisa kuangalia maslahi ya nchi kwa upana wake na matunda ya anayoyafanya Ubungo pia yatafika. Ukianza u-Ubungo tutakuwa hatuna bunge bali ubinafsi,sawa tu na mtu kupendelea familia yake kimaslahi,alisogea mbele kidogo inaluwa kiukoo,hivyo hivyo inakuwa ki-Ubungo! Sawa matatizo yapo Ubungo,hata mimi ni mkazi wa Mbezi, matatizo mengine ni ya kisera zaidi na kama ni kutetea mambo mengi ya msingi mbona anatetea sana siku zote? Habari ya maji ameshaongea sana bungeni,barabara kutoka kimara kuunganisha na segerea,marambomawili segerea, mbezi msakuzi na nyinginezo wewe unakuwaga wapi humsikilizi mbunge wako?
 
Je Mhe. Mnyika hiyo rufaa yako itatumalizia wana Ubungo tatizo la Maji Au la. Ohhh usitulaumu 2015 wewe kalia ya kujitafutia umaarufu wakati sisi wapiga kura wako tuna kero kibao na huzishughulikii. Rufaa hizo 2015 zitakupigia kura.
Ngoja nikupe darasa ili ufala ukutoke

Imekuwa jambo la kawaida kwa wananchi kuwaomba viongozi wao, hasa wabunge wawasaidie kugharamia miradi ya maendeleo. Mazoea haya hyametufanya tusahau majukumu halisix ya wawakilishi wetu na pengine jukumu letu la kuwawajibisha pale wanapokwenda kinyume na wajibu wao.
Wabunge wamesahau majukumu yao ya msingi, badala yake wanajitwika majukumu ya serikali. Hali hii pia inasababisha wananchi tusahau vigezo muhimu vya kuchagua viongozi na kutumbukia kwenye mkumbo wa kuchagua viongozi matajiri-ambao nao wanaitumia fursa hiyo vilivyo kuimarisha utajiri wao pamoja na kuulinda.


Ieleweke kuwa sio wajibu wa wabunge kulipia/kugharamia miradi ya maendeleo majimboni mwao. Wabunge wengi wamekuwa wakitoa ufadhili mbalimbali katika majimbo yao, na kusahau majukumu yao ya msingi ya kuwawakilisha wananchi na kuwasilisha mawazo yao Bungeni ili yapatiwe ufumbuzi na kuisimamia, kuishauri na kuikosoa serikali katika kutoa huduma za jamii na kufanya miradi ya maendeleo.Y
Aidha, mfuko wa jimbo ambao, wabunge wa upinzania na chama tawala, CCM walisahau tofauti zao na kuupitisha kwa kishindo umekuwa nao ukitumika kama mali ya mbunge na katika kutafuta wema kwa wapigakura, wamekuwa wakiahidi mambo kadhaa huku wakiacha kuwaweka wazi wapigakura. Mwishowe wananchi wanaamini hizo ni huruma za mbunge wao.
Hali hii hakika umetupeleka pabaya kwani umesababisha na unaendelea kusababisha yafuatayo:
Mosi, hali ya wabunge kulipia miradi ya maendeleo kunavuruga utaratibu wa mchakato mzima wa mipango ya maendeleo. Tunazo sera nzuri za kusaidia jamii kuibua miradi ya maendeleo na fursa za hiyo miradi kuweza kugharamiwa. Hivyo wabunge wanapochukua jukumu la kugharamia miradi hiyo, kunafanya wananchi wanakosa imani/hawaoni umuhimu wa kufuata mchakato uliwekwa kwa ajili ya kuwaletea maendeleo na badala yake wanatupia jukumu hilo kwa wabunge.
Pili, hali hii inapunguza uwajibikaji wa pande zote mbili hasa uwajibikaji wa wananchi. Mradi unaogharamiwa na wabunge, unakuwa mradi wa mbunge. Hivyo wananchi wanakosa umiliki wa miradi hii kitu ambacho kinafanya miradi hii isiwe endelevu, na zaidi isiwanufaishe wananchi kwa upana wake.
Wakatiw mbunge kwa upande wake anashindwa kutumia nafasi yake ya uwakilishi kwa kujenga hoja kwa lengo la kupata fedha kwa ajili ya kugharamia miradi ya wananchi. Hatima yake ni kwamba serikali haioni umuhimu wa kutenga fedha kwa ajili ya miradi ya wananchi kwani mbunge anazo hela na hataki ibainike kwamba serikali/wananchi wanaweza kuendeleza miradi yao wenyewe.
Pia, mwenendo huu wa wabunge husababisha migongano kwenye Serikali za Mitaa; hii hutokea pale panapokuwepo fedha ambazo tayari zimeshatengwa kwa ajili ya miradi husika, ambapo fedha hizo zinaweza kuishia mikononi mwa wajanja. Wajibu wa mbunge katika hili ni kuwahamasisha wananchi kushiriki katika utekelezaji wa miradi hii na kusimamia matumizi ya fedha ya miradi hii.
Tatu, wabunge kugharamia miradi ya maendeleo inachochea hali ya utegemezi ndani ya jamii zetu. Serikali kupitia sera ya ugatuzi wa madaraka inalenga kuijengea jamii utamaduni wa kujitegemea kwa kuitaka jamii ishiriki moja kwa moja katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo ikiwa ni pamoja na kuchangia gharama. Sasa mbunge anapofadhili hii miradi, inafanya wananchi wajijengee utamaduni wa kusubiri kufanyiwa kila kitu. Na ndiyo hali ilivyo sasa kwani mara nyingi wenye fedha ni rahisi kupata madaraka.
Nne, wananchi wanajikuta wanapima viongozi wao kwa ufadhili waliotoa badala ya kutathmini utekelezaji wa majukumu yao kama wabunge. Hii inasababisha watu wasiokuwa na uwezo wa kifedha kukosa nafasi za uongozi hata kama wanao uwezo wa kuongoza vizuri. Hali imesababisha wananchi wengi kukosa uwakilishi na kuongezeka kwa matatizo makubwa ya uongozi mbovu, ufisadi, rusha na hali ngumu ya maisha huku wachache wakiendelea kunufaika na rasilimali za nchi hii.
Tano, wabunge wanaelemea katika kutafuta fedha za kugharamia miradi ya maendeleo badala ya kufanya majukumu yao ya msingi. Hii imesababisha wabunge kutoonekana majimboni kwa sababu inawabidi watafute mbinu mbalimbali za kupata fedha badala ya kutumia muda wao kutimiza majukumu yao ya msingi.
Badala ya kuwapigania wananchi ili kuwakwamua kutoka hali waliyonayo, wabunge wamejikuta wakipigania maslahi yao binafsi mfano wa sasa wa wanavyopambana kufa na kupona kuhalalisha kupanda kwa posho kwa madai ya kuwa wanatoa hela nyingi kwa wapiga kura kufadhili shughuli mbalimbali za maendeleo. Amenena mtu mmoja kuwa wanatumia fedha za walipa kodi kuwahonga wapiga kura.
 
SABABU ZA AWALI ZA KUKATA RUFAA DHIDI YA UAMUZI WA SPIKA WA TAREHE 9/11/2012 WENYE
MWELEKEO WA ‘FUNIKA KOMBE'

Baada ya habari kutolewa jana na leo juu ya uamuzi wa Spika kuhusu tuhuma kwamba baadhi wa wabunge na wajumbe wa kamati ya Nishati na Madini walijihusisha na vitendo vya rushwa katika kutekeleza kazi zao za kibunge, nimeulizwa na baadhi ya wanahabari na wananchi kwa simu na kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii sababu za kusimama bungeni tarehe 9 Novemba 2012 mara baada ya Spika kutoa uamuzi huo na kutaka kuomba muongozo.

Nalazimika kutoa ufafanuzi huu nje ya bunge baada ya mkutano wa bunge kuahirishwa bila Spika kunipa fursa ya kusema jambo hili bungeni kwamba nilitaka muongozo wake kwa mujibu wa Kanuni ya 5(1) na 5 (2) kuwa nakusudia kukata rufaa dhidi ya uamuzi wake kutokana na kuwa na maudhui kadhaa yasiyozingatia katiba ya nchi, sheria mbalimbali za nchi, kanuni za kudumu za bunge, maamuzi ya awali ya maspika wa Bunge pamoja na mila na desturi za mabunge mengine yenye utaratibu wa kibunge unaofanana na utaratibu wa bunge letu.

Hata hivyo kwa kuzingatia kuwa rufaa huchukua muda kusikilizwa nilitaka niombe muongozo wake kabla ya Mkutano wa Bunge kuahirishwa kwa kuwa katika uamuzi wake hakueleza hatma ya Kamati ya Nishati na Madini ilivyovunjwa, hivyo Spika anapaswa bado kuueleza umma, iwapo kamati hiyo inarejeshwa au inaundwa kamati nyingine au kuelekeza kamati nyingine ya kudumu ya Bunge inayopaswa kuisimamia Serikali wakati huu ambapo nchi inakabiliwa na matatizo mengi kwenye sekta za nishati na madini yenye athari kwa maisha ya wananchi wakiwemo wa Jimbo la Ubungo.

Kwa nafasi yangu ya Waziri Kivuli wa Nishati na Madini nasisitiza kwamba Spika anapaswa kurejea barua niliyomwandikia tangu mwezi Oktoba, ambayo mpaka sasa haijapatiwa majibu, pia arejee hoja niliyoiwasilisha bungeni na kuungwa mkono ya jambo lililohusu haki za bunge na miongozo niliyoomba bungeni kuhusu masuala ya nishati kwa nyakati mbalimbali katika mkutano wa Bunge uliomalizika na kutoa kauli kwa umma.

Kwa kuwa katika uamuzi wake Spika wa Bunge ameeleza kwamba Waziri wa Nishati na Madini Prof. Sospeter Muhongo na Katibu Mkuu wake Eliackim Maswi wametoa maelezo yasiyokuwa kweli kwa nyakati mbalimbali, uwepo wa kamati ya bunge kwa ajili ya kuisimamia Wizara hiyo kwa niaba ya bunge ni suala linalohitaji uamuzi wa haraka.

Aidha, katika uamuzi wake Spika zaidi ya kutoa onyo kali kwa Katibu Mkuu na Wabunge hakutoa onyo kwa Waziri wa Nishati na Madini wala hakueleza chochote iwapo alipokea ushauri kutoka kwa Kamati Ndogo ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge kuhusu ukiukwaji wa kanuni uliofanywa na Spika mwenyewe bungeni wakati wa kadhia nzima.

Kwa mujibu wa Kanuni za Bunge Spika anaweza kutoa taarifa bungeni wakati wowote na taarifa yake haijadiliwi hivyo sehemu kubwa ya taarifa ya tarehe 9 Novemba 2012 ilikuwa ni maelezo kuanzia sehemu ya kwanza mpaka sehemu ya pili.

Uamuzi wa Spika unapatikana sehemu ya tatu ya maelekezo hususan kifungu cha 6.12 ya kwamba "tuhuma husika hazikuweza kuthibitishwa" na baadaye kufuatiwa na uamuzi wa Spika kuhusu watoa tuhuma katika vipengele (a), (b), (c) na (d).

Nakusudia kukata rufaa ili taarifa kamili ya Kamati Ndogo ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge iweze kuwasilishwa kwa ukamilifu wake kwenye kamati husika ya kudumu ya Bunge na hatimaye taarifa kamili kuwasilishwa na kujadiliwa bungeni ili ‘mbivu na mbovu' zijulikane na masuala yanayohitaji kufanyiwa uchunguzi wa ziada na vyombo vingine vya nje ya Bunge yaendelee kwa hatua zaidi badala ya uamuzi huu wa ‘funika kombe'.

Yapo masuala ya ziada ambayo binafsi niliyaeleza mbele ya kamati ndogo chini ya kiapo ambayo sitakiwi kuyaeleza nje ya bunge kwa mujibu wa kanuni na sheria husika , hata hivyo taarifa kamili ikiingia bungeni kutakuwa na uhuru wa majadiliano kwa mujibu wa Ibara ya 100 ya Katiba ya Nchi.

Aidha, nitakata rufaa kwa kuwa kiwango cha ‘adhabu' kilichotolewa kwenye uamuzi wa Spika hakilingani na ‘makosa' ambayo yameelezwa kuwa na uzito wenye kuathiri "kwa kiasi kikubwa hadhi ya Bunge kama taasisi na heshima ya wabunge waliohusishwa".

Spika amefanya uamuzi wake chini ya Kanuni ya 5(1) na 72 (1) lakini hakuzingatia kuwa kanuni ya 72 (3) inaeleza kuwa iwapo mbunge ameshindwa kuthibitisha ukweli Spika amepewa fursa ya kumsimamisha mbunge huyo kuhudhuria vikao vya Bunge visivyozidi vitano.

Aidha nitakata rufaa kwa kuwa waliodaiwa kutoa kutoa tuhuma bila ushahidi walipaswa kujieleza kwa tuhuma hizo kabla ya kuhukumiwa kwa misingi ya kanuni za haki ya asili zilizopo pia katika katiba ya Nchi na kwa kuzingatia matakwa ya kanuni za kudumu za Bunge; hata hivyo Spika amefikia uamuzi wa moja kwa moja wa kutoa adhabu ya ‘onyo kali' kinyume na masharti ya kanuni ya 5 (1).

Ikumbukwe kwamba Spika katika maelezo yake amesisitiza kuwa Kamati Ndogo ilipewa hadidu rejea moja tu, "Kuchunguza na kumshauri Spika iwapo tuhuma kwa baadhi ya wabunge na wajumbe wa Kamati ya Nishati na Madini kujihusisha na vitendo vya rushwa ni za kweli au hapana".

Hivyo basi baada ya kuchunguza kwa mujibu wa hadidu rejea hiyo na kamati kuwasilisha ripoti yake, Spika alipaswa kama kuna ukiukwaji mpya wa kanuni uliobainika kutokana na uchunguzi huo, kuanzisha mchakato wa adhabu.

Binafsi niliitwa kwa maandishi kuisaidia kamati ndogo katika uchunguzi wake kutokana na maoni niliyowasilisha bungeni ya kwamba "….Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inafahamu kwamba kuna kampeni kubwa inafanywa ndani na nje ya Bunge ili uamuzi wa Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati ubatilishwe kwa maslahi ya Makampuni yaliyokosa zabuni kuiuzia TANESCO mafuta ya kuendesha mitambo ya kufua umeme…".

Sijawahi kuandikiwa au kuitwa popote kutakiwa kujieleza kwa ‘kuisemea tuhuma bungeni bila ya kufanya utafiti kupata ukweli' na maelezo hayo niliyoyatoa bungeni hayakukiuka kanuni yoyote ya bunge kama ambavyo nitathibitisha wakati nitakapokata rufaa.

Kwa upande mwingine nitakata rufaa kwa kuwa adhabu aliyopewa Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Eliakim Maswi hailingani na ukubwa wa makosa anayodaiwa kuyafanya, ikiwa ni kweli amevunja haki za bunge kwa kuzusha tuhuma za uongo dhidi ya wabunge kwa ajili ya kujihami dhidi ya baadhi ya wajumbe wa kamati ya Bunge ya Nishati na Madini waliokuwa wanahoji kuhusu utendaji wa Wizara yake.

Kwa kosa hilo ikiwa maelezo ya Spika kuhusu matokeo ya uchunguzi wa Kamati ni sahihi, anapaswa kufunguliwa mashtaka kwa mujibu wa Sheria ya Kinga, Madaraka na Haki za Bunge na kupewa adhabu ya zaidi ya onyo ikiwemo hata faini au kifungo au walau kutakiwa kuwajibika.

Kadhalika, Spika ameeleza kuwa mbinu aliyotumia ni pamoja na kutaka kuwalipa fedha wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini shilingi milioni mbili kwa kila mjumbe, madai haya ni ya jaribio la kufanya ufisadi wa fedha na matumizi mabaya ya madaraka kama ilivyokuwa kwenye kashfa ya Katibu Mkuu aliyemtangulia David Jairo hivyo Spika alipaswa kupendekeza kwa mamlaka ya uteuzi wake kuchukua hatua za kinidhamu na kisheria.

Uamuzi wa Spika ‘kufunika kombe' hauna tofauti na maamuzi yaliyotangulia ambayo yamesababisha mpaka sasa Serikali haijawasilisha bungeni ripoti ya utekelezaji wa maazimio ya Bunge kufuatia uchunguzi uliofanywa na kamati teule ya Bunge.

Ni vizuri ikakumbukwa kwamba katika hotuba yangu bungeni kwa niaba ya Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni tarehe 27 Julai 2012 nilisisitiza kwamba "ili ukweli wa kina uweze kujulikana Kambi Rasmi ya Upinzani inapendekeza kuwa bunge liazimie kuunda Kamati Teule ya Bunge kuchunguza masuala yote ya ukiukwaji wa sheria, matumizi mabaya ya madaraka na tuhuma za ufisadi katika utekelezaji wa mpango wa dharura wa umeme na ununuzi wa mafuta wa ajili ya mitambo ya umeme."

"Uchunguzi huo uhusishe pia mkaguzi mkuu kufanya ukaguzi wa kiuchunguzi (Forensic Audit) kwa malipo yaliyofanywa na makampuni ya BP (Sasa PUMA Energy), Oryx na Camel Oil ili kubaini iwapo kuna vigogo zaidi wa serikali waliojinufaisha kwa kisingizio cha dharura ya umeme. Izingatiwe kwamba masharti ya ibara ya 27(2) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inamtaka kila mtu "… kutunza vizuri mali ya Mamlaka ya Nchi na ya pamoja (na) kupiga vita aina zote za uharibifu na ubadhirifu….".

Mchakato huu ungewezesha kupata ukweli wa ziada kibunge kuliko utaratibu uliotumiwa na Kamati Ndogo na Spika.

Nitaeleza masuala ya ziada nitakayoyakatia rufaa na kauli yangu kuhusu maelezo na uamuzi wa Spika juu ya Waziri na Waziri Kivuli wa Nishati na Madini.

John Mnyika (Mb)
10/11/2012



​
 
[TABLE="width: 879"]
[TR]
[TD="bgcolor: #ffffff"][TABLE="width: 599"]
[TR]
[TD]Mnyika: Spika amefunika kombe
• AKATA RUFAA, ADAI ADHABU ZILIZOTOLEWA NDOGO

na Mwandishi wetu​
[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
[/TD]
[TD="width: 140, bgcolor: #FFFFFF"][/TD]
[/TR]
[TR]
[TD][TABLE="width: 599"]
[TR]
[TD]
MBUNGE wa Ubungo na Waziri Kivuli wa Nishati na Madini, John Mnyika, ameamua kulivalia njuga suala la tuhuma za wabunge na wajumbe wa Kamati ya Nishati na Madini kujihusisha na vitendo vya rushwa, akisema kuwa uamuzi wa Spika Anne Makinda umeacha makando kando mengi, ikiwemo ukiukwaji wa katiba ya nchi, hivyo anajipanga kuukatia rufaa.


Alisema kuwa uamuzi wa Spika Makinda uliotangazwa juzi bungeni, umefanyika kwa namna ya ‘funika kombe', hivyo rufaa yake inalenga kutaka taarifa kamili ya Kamati Ndogo ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge iwasilishwe kwa ukamilifu wake kwenye kamati husika ya kudumu ya Bunge na kujadiliwa bungeni ili ‘mbivu na mbovu' katika usimamizi na uendeshaji wa sekta ya nishati zijulikane, kisha uchunguzi wa kina ukihusisha vyombo vingine nje ya Bunge, ufanyike.


Alifafanua kwa kurejea hotuba yake aliyosoma bungeni kwa niaba ya kambi rasmi ya upinzani bungeni wakati wa Bunge la bajeti lililopita, akisema kuwa alitoa angalizo tangu awali kuwa ili ukweli ujulikane ilipaswa kuundwa Kamati Teule ya Bunge kuchunguza masuala yote ya ukiukwaji wa sheria, matumizi mabaya ya madaraka na tuhuma za ufisadi katika utekelezaji wa mpango wa dharura wa umeme na ununuzi wa mafuta kwa ajili ya mitambo ya umeme.


Alisema ni muhimu kufanyika kwa uchunguzi wa namna hiyo, ukihusisha pia Mkaguzi Mkuu kufanya ukaguzi wa kiuchunguzi kwa malipo yaliyofanywa na makampuni ya BP (Sasa Puma Energy), Oryx na Camel Oil ili kubaini iwapo kuna vigogo zaidi wa serikali waliojinufaisha kwa kisingizio cha dharura ya umeme, kwa kuzingatia masharti ya ibara ya 27(2) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.


Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari jana, siku moja tu baada ya Spika Makinda kutoa uamuzi wake bungeni juu ya tuhuma za wabunge kujihusisha na rushwa, Mnyika alisema kuwa atakata rufaa kwa kuwa kiwango cha ‘adhabu' kilichotolewa na Spika hakilingani na ‘makosa' ambayo yameelezwa kuwa na uzito wenye kuathiri "kwa kiasi kikubwa hadhi ya Bunge kama taasisi na heshima ya wabunge waliohusishwa".


Akitolea mfano, Mnyika alisema kuwa ikiwa ni kweli Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Eliakim Maswi kuwa amefanya makosa ya kuvunja haki za Bunge kwa kuzusha tuhuma za uongo ili kujihami dhidi ya wabunge waliokuwa wanahoji utendaji wake, basi adhabu aliyopewa hailingani na ukubwa wa makosa anayodaiwa kufanya.


"Kwa kosa hilo ikiwa maelezo ya Spika kuhusu matokeo ya uchunguzi wa kamati ni sahihi, anapaswa kufunguliwa mashtaka kwa mujibu wa Sheria ya Kinga, Madaraka na Haki za Bunge na kupewa adhabu ya zaidi ya onyo ikiwemo hata faini au kifungo au walau kutakiwa kuwajibika.


"Kadhalika Spika ameeleza kuwa mbinu aliyotumia (Maswi) ni pamoja na kutaka kuwalipa fedha wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini shilingi milioni mbili kwa kila mjumbe, madai haya ni ya jaribio la kufanya ufisadi wa fedha na matumizi mabaya ya madaraka kama ilivyokuwa kwenye kashfa ya Katibu Mkuu aliyemtangulia, David Jairo, hivyo Spika alipaswa kupendekeza kwa mamlaka ya uteuzi wake kuchukua hatua za kinidhamu na kisheria.


"Baada ya uamuzi wa Spika kuhusu tuhuma kwamba baadhi wa wabunge na wajumbe wa kamati ya Nishati na Madini walijihusisha na vitendo vya rushwa katika kutekeleza kazi zao za kibunge, nimeulizwa na baadhi ya wanahabari na wananchi kwa simu na kwenye mitandao ya kijamii sababu za kusimama bungeni tarehe 9 Novemba 2012 mara baada ya Spika kutoa uamuzi huo na kutaka kuomba muongozo.


"Nakusudia kukata rufaa kwa sababu uamuzi wake una maudhui kadhaa yasiyozingatia katiba ya nchi, sheria mbalimbali za nchi, kanuni za kudumu za Bunge, maamuzi ya awali ya maspika wa Bunge pamoja na mila na desturi za mabunge mengine yenye utaratibu wa kibunge unaofanana na utaratibu wa bunge letu," alisema Mnyika na kuongeza;


"Kwa kuzingatia kuwa rufaa huchukua muda kusikilizwa, nilitaka niombe muongozo wake kwa kuwa katika uamuzi wake hakueleza hatma ya Kamati ya Nishati na Madini, hivyo Spika anapaswa kuueleza umma iwapo kamati hiyo inarejeshwa au inaundwa kamati nyingine au kuelekeza kamati nyingine ya kudumu ya Bunge inayopaswa kuisimamia serikali wakati huu ambapo nchi inakabiliwa na matatizo mengi kwenye sekta za nishati na madini yenye athari kwa maisha ya wananchi."


Aliongeza kusema kuwa, kwa kuwa katika uamuzi wake Spika Makinda alieleza kwamba Waziri wa Nishati na Madini, Prof. Sospeter Muhongo na Katibu Mkuu wake Maswi wametoa maelezo yasiyokuwa kweli kwa nyakati mbalimbali, uwepo wa Kamati ya Bunge kwa ajili ya kuisimamia wizara hiyo kwa niaba ya Bunge ni suala linalohitaji uamuzi wa haraka kutokana na hali ya nchi juu ya sekta ya nishati kuwa tete bila usimamizi wa kibunge.


Aidha, katika taarifa yake hiyo, Mnyika ameonekana kushangazwa na kitendo cha Spika Makinda kutoa onyo kali kwa Katibu Mkuu na wabunge kadhaa, lakini hakutoa onyo kwa Waziri wa Nishati na Madini wala hakueleza chochote iwapo alipokea ushauri kutoka kwa Kamati Ndogo ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge kuhusu ukiukwaji wa kanuni uliofanywa bungeni wakati wa kadhia nzima.


Akikumbushia hadidu rejea moja tu iliyopewa Kamati Ndogo iliyofanya uchunguzi ya "Kuchunguza na kumshauri Spika iwapo tuhuma kwa baadhi ya wabunge na wajumbe wa Kamati ya Nishati na Madini kujihusisha na vitendo vya rushwa ni za kweli au hapana", hivyo, kwa mujibu wake, baada ya uchunguzi na kuwasilisha ripoti yake Spika alipaswa kuanzisha mchakato wa adhabu, kama kulibainika kuwepo kwa makosa ya ukiukwaji wa kanuni.


Alisema kuwa uamuzi wa Spika ‘kufunika kombe' hauna tofauti na maamuzi yaliyotangulia ambayo yamesababisha mpaka sasa serikali haijawasilisha bungeni ripoti ya utekelezaji wa maazimio ya Bunge juu ya sakata la aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Jairo, kufuatia uchunguzi uliofanywa na Kamati Teule ya Bunge.


Source; Tanzania Daima
​
[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
 
While Speaker of the National Assembly, Anne Makinda, may have played a ‘smart' card to save the government from further political humiliation in Parliament, there's still serious doubt on the ‘graft report' tabled on Friday.


As some legislators hail the Speaker's verdict against the embattled Permanent Secretary, Eliakim Maswi, analysts and some Members of Parliament are now calling for a thorough investigation to establish what really transpired.


In a detailed statement, the Energy and Minerals shadow minister John Mnyika has cast serious doubts on the ‘graft report' tabled at the close of the 9th session of Parliament on Friday saying that's why he rose to seek the ‘speaker's guidance' but was shut down unheard.


They lied to Parliament thus concluded the Parliamentary Standing Committee on Ethics, Privileges and Powers against Energy and Minerals Minister Professor Sospeter Muhongo and Permanent Secretary Eliakim Maswi.


But Mnyika says key steps were overlooked or what passed as a ‘report' was in fact an ‘Executive Sum' of an edited version of the entire report yet to see the light of day.


The Committee's ‘report' read by Speaker of Parliament Anne Makinda yesterday cleared Members of Parliament and other members of the dissolved Parliamentary Standing Committee for Energy and Minerals from corruption charges or any wrongdoing.


The MPs were cleared after the sub -committee of the Parliamentary Standing Committee on Ethics, Privileges and Powers led by Brigadier General Hassan Ngwilizi probed the corruption charges leveled against them and submitted its findings to the speaker.


The report has also found Minister Muhongo and the Permanent Secretary Maswi guilty after leveling the allegations against the MPs but without evidence to substantiate them.


During the debate for the budget of the Ministry of Energy and Minerals on July 27-28th this year Minister Muhongo claimed that some MPs who belonged to dissolved parliamentary committee on energy and minerals had business ties with Tanesco, which subsequently rendered an issue touching on conflict of interest when discharging their functions .


Maswi on his part had alleged through his letter to the Clerk to the National Assembly with reference No.SAB.88/223/01/28 dated July 31, 2012 that a CCM Special Seats MP Sarah Msafiri Ally had asked for Sh 50million as bribe so that she could share out to fellow MPs to facilitate smooth sailing of the the ministry's issues in Parliament.


According to the sub-committee's findings, both ministerial leaders failed to adduce evidence to substantiate their claims.
When called to substantiate his claims, the minister is reported to have simply said whatever would be said by anybody over the matter would remain ‘mere allegations'.


The documents which the sub-committee scrutinized, in its search for truth over claims that some MPs, including Munde Tambwe and Sarah Msafiri Ally, had a contract to supply tyres to Tanesco, also proved inherently false -- the two MPs had no company that rendered such service to the power utility firm.


Mnyika says he has since been put to task by keen journalists and the general public on social media, as well as by phone, all of them asking him why he stood on a "point of order" on 9th November 2012 soon after the Speaker had made her ruling – to seek for the Speaker's guidance on such ruling.


The shadow minister now feels constrained to offer such clarification outside Bunge because he couldn't get the same from within the House – where he most needed to do it – but the Speaker moved a move to adjourn the 9th Parliamentary without availing Hon. Mnyika opportunity to seek the Speaker's guidance as provided for under Standing Orders 5 (1) and 5 (2) mainly to appeal against the Speaker's ruling.


Mnyika says he sought to appeal to the ‘speaker's guidance' on grounds that her ruling was clouded by circumstances suggesting several legal requirements had been violated – including the country's constitution, the parliamentary standing orders, past best practices as well as past decisions reached in Parliament sessions in other countries held under similar circumstances like ours, among others.


However, since appeals of this nature take time before they are heard, Hon. Mnyika says he then sought the Speaker's guidance on the future of the disbanded Standing Committee on Energy and Minerals before the adjournment of parliament's 9th session; even then the Speaker still needs to tell the public whether the disbanded committee would be reinstated, or whether another committee would be formed, or whether another Parliamentary standing committee would be directed to play the role of ‘watchdog' over government affairs at this time when the country faces a host of problems in the energy and minerals sectors – all with direct adverse effects on the lives of the people


In his capacity of shadow minister for energy and minerals, Hon. Mnyika drew the speaker's attention to an earlier communication (October) – to which the speaker had yet to respond to date. In addition, he also seeks response to several similar issues touching the two sectors, also raised in the House during the just ended Bunge session – all of which also needed to be addressed for the benefit of the general public.


And since the Speaker has told Parliament that Energy and Minerals Minister Prof. Sospeter Muhongo and his permanent secretary Eliakim Maswi had made unsubstantiated allegations at various occasions, the need for the (physical) presence of a parliamentary standing committee to oversee the affairs of the ministry calls for immediate (urgent) action.


Beyond ‘stern warning' to the permanent secretary, Hon. Mnyika says the Speaker falls short of doing the same against the Minister, nor did she offer any explanation whether she had received advice on the same from the Parliamentary Standing Committee on Ethics, Privileges and Powers.


According to Parliamentary standing orders, the Speaker can make a statement at any time without necessarily subjecting it to debate, so much of the statement made on 9th November 2012 fell under this category.


The Speaker's ruling was therefore based on Sections 6.12 under which she ruled that "the relevant allegations (of corruption among MPs) could not be substantiated" which was subsequently following by the Speaker's decisions under sections (a), (b), (c) and (d).


"I intend to appeal (against these rulings) so that the entire report by Parliamentary Standing Committee on Ethics, Privileges and Powers is presented in its fullness (for fresh deliberation) before a relevant standing committee of parliament … and later tabled in plenary before the House," Hon. Mnyika concludes.


One CCM legislator who once served as cabinet Minister speaking on condition of anonymity told the Guardian on Sunda:
"This scandal is still alive and kicking…Speaker may have saved the executive, but very soon the full truth would come out about what really transpired.


"What Speaker did was double standards…She recommends disciplinary actions against the PS, but does nothing to the Minister." The CCM legislator told the Guardian on Sunday in Dodoma."

Source; The Guardian on Sunday
 
Je Mhe. Mnyika hiyo rufaa yako itatumalizia wana Ubungo tatizo la Maji Au la. Ohhh usitulaumu 2015 wewe kalia ya kujitafutia umaarufu wakati sisi wapiga kura wako tuna kero kibao na huzishughulikii. Rufaa hizo 2015 zitakupigia kura.


Mkuu tukiwa na wananchi wenye mitazamo kama yako hii kwamba mbunge kazi yake ni kutetea jimbo lake, basi nchi hii haitasonga!

Kazi ya wabunge si kwenda bungeni kukomaa na matatizo ya majimbo yao tu. Na hapa ndo ujinga wa wabunge na wananchi wengi ulipogandia. Ukiwa mbunge wewe ni mwakilishi wa wananchi wote, tetea haki hata kama kwa kufanya hivyo kutakufanya ukose ubunge msimu unaofuata.

Kwa mitizamo kama hii itabidi mambo ya gesi yazungumzwe na wabunge wa Lindi na Mtwara tu!.

Wabunge wachumia tumbo wao akili yao na misimamo yao uongozwa na siasa za uchaguzi unaofuata badala ya haki na uzalendo kwa nchi yao!
 
Hatufukui makaburi, tunasonga mbele

Bila ya shaka kusonga mbele kikondoo mkiwa mumeinamisha vichwa chini bila ya kuuliza mambo yanayotekea katika safari yenu, ambayo ndio hasa yanayowakosesha maji.
 
Back
Top Bottom